Swahili Service

JINSI YA KUPINDUA LAANA ZA SIRI

MFULULIZO: JINSI YA KUFANYA VITA VYA KIROHO

SOMO: NEHEMIA 13:2; 2 WAFALME 2:13-21; HESABU 22:1-41

 

Laana zilizo ngumu zaidi kuvunja na kupindua ni laana za siri. Watu wanaojua kwamba wako chini ya laana wanakombolewa upesi, lakini wasio jua kwamba wako katika laana wanakuwa na shida kupindua laana zao. Laana za siri zinaweza kuendelea hata wakati mtu ameokoka kwa kutofahamu kwamba hizi laana ziko.

Laana za siri ndizo laana mbaya zaidi na shetani anazitumia zaidi kama silaha ya kuharibu hatima ya mtu. Hivyo ni jambo la busara kutambua hizi laana na kuzivunja au kuzipindua.

Kinyume cha laana ni baraka unapolaani mtu unatamka mabaya juu yake, hivyo maumivu na jeraha zinakuja juu ya huyo mtu.

Kumlaani mtu ni kumfunga huyo mtu kama jinsi mchawi anavyofanya..

Kulaani mtu ni kufanya vita juu ya huyo mtu.

Laana ni maneno yanayoletwa pamoja kumtesa mtu na kumkwaza katika njia na mapito ya maisha yake.

Laana ni kikwazo kisichoonekana, kizuizi kinacho zuia baraka za Mungu kumfikia aliye laani wao.

Katika Nehemia 13:2, Mungu anazo nguvu na uwezo wa kugeuza, kubadili na kupindua laana kuwa baraka.

Tena katika 2 Wafalme 2:13-21 upako wa Mungu unapokuja juu ya laana ya siri adui lazima kushindwa.

Hebu omba maombi yafuatayo:

  1. BWANA tuma nguvu zako za uponyaji kwa misingi ya maisha yangu.
  2. BWANA tuma moto wa uponyaji kwa misingi ya maisha yangu. Nguvu za Mungu kuponya zinapofika katika misingi ya maisha ya mtu, mtu huyu anaponywa mpaka kichwa chake.
  • Shida nyingi tulizo nazo maishani zinakuja kwa sababu ya laana za siri.
  • Shida ya Yeriko ililetwa na wanadamu na shida ya mwanadamu ni dhambi ya kutotii.
  • Wengi walilelewa kanisani sasa wanaishi kama shetani.
  • Mwanadamu amejaribu mambo yote bila furaha.
  • Msingi wa Yeriko ulikuwa salama, lakini laana ilipoingia Yeriko pakawa mahali pa shida- Yoshua 6:26.
  • Ishara kuu ya laana ni kwamba mtu anakuwa mtu na masumbuko, mashida na kukosa amani.
  • Mtu wa laana anasumbuka sana, wakati baraka zake na kufaulu kuko karibu, janga na shida zinaanza kudhibiti maendeleo yake.
  • Ikiwa ni laana ya kutoendelea na masomo , mitihani inapokaribia, magonjwa na taharuki na changamoto zinatokea.
  • Laana zinakuwa na matokeo mabaya yanayoendelea kwa muda mrefu zaidi.
  • Laana inaweza kuendelea kizazi baada ya kizazi.
  • Laana juu ya Yeriko ilizidi kwa miaka ya 500.
  • Mtu wa Mungu (Elisha) alipovunja ile laana, baraka zilirudi mara moja, hivyo laana juu yako itamalizika mara moja leo, katika jina la Yesu Kristo.
  • Laana zinakuwa kama ukuta wa ulio kuzuia pepo ndani.
  • Mapepo ndio walinzi na meneja wa laana ndani ya watu.
  • Laana zote kutoka kwa Mungu zinakuja kwa sababu ya kutotii na kuasi.
  • Mungu ndiye aliyetoa laana ya kwanza juu ya Adamu na Hawa- Mwanzo 3.
  • Kila dhambi huleta laana kwa sababu mshahara wa dhambi ni mauti- Mithali 26:2.
  • Laana bila sababu haiwezi kudumu, laana inatafuta mahali pa kutua, kumea na mbolea ya laana ni dhambi.
  • Kung’oa laana lazima kutubu dhambi kwa ukamilifu.
  • Hakuna laana bila pepo au daimoni inayofanyisha hio laana kazi.
  • Panapo laana hapana maendeleo maana pepo wa hio laana anafuatia kuharibu kila baraka.
  • Laana haijui mipaka inafuata mtu popote aendapo- Kumbukumbu 28.
  • Laana zinaondolewa na Yesu Kristo- Wagalatia 3:13-14.
  • Laana bila sababu inamrudia aliyeituma.

LAANA ZA KUJILAANI

  • Mke kumwacha bwana wake na kuolewa na tajiri. Mume kumwacha mke wake na kuoa mke kijana.
  • Kuoa wake wengi ni laana kwa maana mtu anaoa mwanamke ambaye angeolewa na mtu mwingine.
  • Laana ya mtu kulala na wake za watu wengine.
  • Wanawake wanao peleka vijana shule, au kazini ili kuwatumia baadaye.
  • Au vijana wanaotumia wanawake kama Sponsor baadaye kuwatoroka-laana.
  • Wanawake au wanaume wanaooa maskini na kuwatumia na kuwacheka wanapokea laana.
  • Kila tendo la ngono nje ya ndoa ni laana.
  • Laana juu ya (LGBTQ) ni dhahiri.
  • Laana ya kuwatumia watoto wako kwa uasherati au kujinufaisha mwenyewe- Mambo ya Walawi 19:29.
  • Pornography na usherati ni laana juu ya mtu binafsi.
  • Pesa na mali ya wafu huleta laana.

LAANI YA KUKOSA HESHIMA KWA WAZAZI

  • Laana za wazazi zinafanya kazi kama jinsi saratani (Cancer).
  • Mtu anayeishi kwa laana ya wazazi wake anakuwa ni kama jinsi jangwa, mbingu zinafungwa na ardhi yake kunakuwa kama chuma- Marko 11:13-21.
  • Laana zinakuja kwa sababu ya kutotii Mungu, baraka zinakuja kwa sababu ya kutii- Kumbukumbu 28.

MAOMBI

  • Ninakataa kunywa kutoka ka kisima cha shida- katika jina la Yesu.
  • Ninachukua mamlaka juu ya laana zilizowekwa juu ya maisha yangu- katika jina la Yesu Kristo.
  • Ee Bwana vunja kila laana juu yangu, ninaamua kukutii kutoka leo-katika jina la Yesu Kristo.
  • Ninaamrisha kila pepo aliyewekwa juu yangu kuendelesha laana juu yangu- toweka katika jina la Yesu Kristo.
  • Kila laana juu ya maisha yangu, jamii yangu, kazi yangu badilika kuwa baraka – katika jina la Yesu Kristo.
  • Kila laana juu ya akili na mwili wangu vunjika- katika jina la Yesu Kristo.
  • Kila laana ya umaskini, kushindwa, kunyanyaswa, sifa mbaya na laana ya kujitesa na kujiua – vunjika katika jina la Yesu Kristo.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *