SOMO: ZABURI 121:1-3
Kila mmoja wetu anahitaji msaada katika kila eneo ya maisha.
- Kwa mwili- ulinzi
- Kiroho- kuelekezwa.
- Kifedha- utauwa na ufanisi
Tunahitaji msaada wa Mungu kwa maana peke yetu hatuwezi- Yohana 15:5.
Msaada wetu u katika Mungu ambaye hawezi kushindwa. Bila Wewe Bwana siwezi. Hebu tuone.
UKUU WA MSAADA WA MUNGU (superiority of divine help)
- Msaada wa Mungu haukomi na ndio mali ya dhamani zaidi kwetu kama wanadamu.
- Msaada wa Mungu unakupigania mbele ya nguvu za giza hapa duniani.
- Msaada wa Mungu ni dhamani zaidi kuliko msaada wa mwanadamu, system au serikali.
- Mungu ndiye msaada wako- Zaburi 46:1-5.
- Mwanadamu kwa kawaida anapungukiwa, system nazo zinaanguka, mwanadamu anabadilika lakini Mungu hawezi kubadilika.
- Mungu ndiye msaada wa karibu- Zaburi 46:1.
- Wanadamu hawatakuwako wakati unaowahitaji zaidi.
- Lakini Mungu yu karibu nawe kila wakati unapomhitaji!!
- Mungu ni msaada dhabiti kwa mwanadamu- Malaki 3:6.
- Watu walio kusaidia hapo Mwanzo wanaweza wakachoka, wakavunjika moyo na kukuacha, lakini msaada wa Mungu haukomi.
- Mungu ndiye msaada wa faraja zaidi kwa mwanadamu- Wafilipi 4:19.
- Mungu ni tajiri kutosha, Mungu ni mkarimu zaidi kunisaidia bila shida kwake.
- Mungu ndiye msaada anayeelewa zaidi na mwanadamu- Yohana 6:6, Warumi 16:27, 1st Timotheo 1:17.
- Watu wengine wanapenda kukusaidia lakini wamechanganyikiwa, hawajui jinsi ya kukusaidia.
- Lakini Mungu yuaelewa na shida yako na anao ufahamu jinsi ya kukusaidia.
UMUHIMU WA MSAADA WA MUNGU (The necessity for divine help)- Zaburi 127:1
- Unahitaji msaada wa Mungu ili usifanye kazi bure, maana huna nguvu zako mwenyewe.
- Unapojua siri ya msaada wa Mungu, hutajipigania wala kufanya kazi bure.
- Si kila mshindi anapitia shida nyingi kupata ushindi wake.
- Msaada wa Mungu ndio unaojenga watu.
- Kila mshindi katika ufalme wa Mungu amesaidiwa na Mungu- Hivyo kazi yako ni bure bila Mungu.
- Watu wengine wana shahada za juu zaidi kuliko wewe lakini hawajabarikiwa kama wewe.
- Hakuna mtu amabaye amejimudu peke yake (self made men become self-destroyed men).
- Tajiri mjinga katika Luka 12:16-21, alikuwa mjinga kwa sababu aliona ni yeye mwenyewe kwa nguvu zake alijipatia mavuno.
- Mungu alimwita mjinga kwa sababu hakumpa Mungu shukrani, alisema (mimi, mimi).
- Hatuwezi kwenda mbali bila Mungu.
- Baraka za Mungu pekee ndizo zinadumu milele.
- Mungu anapofanya jina lako kuu, basi mshukuru kwa msaada wake kwako.
- Mfalme Daudi alipostawi sana, alienda nyumbani mwa Mungu mara kadha kila siku kushukuru Mungu- Kumbukumbu 32:15-18.
- Huna nguvu duniani bila Mungu, unahitaji msaada kutoka juu.
- Kila maendeleo duniani yanawezeshwa na msaada wa Mungu.
UWEPO WA MSAADA WA MUNGU (The availability of divine help).
- Mungu yuko tayari na anapenda kuwasaidia wote wamwaminio na kuomba msaada wake.
- Msaada wake unapatikana katika kila eneo ya maisha.
- Ushindi vitani- 1 Sam.7:9-12.
- Ukombozi katika bonde la mauti- 1 Mambo ya Nyakati 15:26.
- Tunahitaji msaada wa Mungu katika janga zinazoua watu wengine. Kusimama mahali wengine wameanguka, kuwa hai mahali wengine wamekufa.
- Nguvu za kufaulu.
- Nguvu za Mungu zinatupa kufaulu katika maisha haya- 1 Wafalme 18:46; Danieli 11:32; Zaburi 89:19.
- Ukombozi kutokana na aibu na dhuluma na haya- Isaya 50:7-9.
- Ustadi na udhabiti unatoka kwa Mungu.
Basi tufanyeje kupokea msaada wa Mungu kila wakati?
- Tukae katika maombi, moyo safi na imani- Waebrania 4:16.
- Ungama udhaifu na umaskini wako kwa Mungu- Mithali 3:5-8.
- Tuwe watu wa shukrani kwa Mungu kila saa- 1 Sam. 7:11-12.
MWISHO
- Gundua kwamba unahitaji msaada wa Mungu.
- Usimpe Mungu kisogo, Yeye ndiye msaada wako.
- Mshukuru Mungu kwa msaada wake leo.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
