Swahili Service

JINSI YA KUTOKA KWA SHIMO LA KORONA

MFULILIZO:  YESU KRISTO NI WA THAMANI SANA

SOMO:   I PETRO  5:5-10

Tangazo lifuatao liliwekwa kwa dirisha ya duka la nguo London, Uegereza. “Tumekuwa kwa Biashara ya nguo kwa miaka zaidi ya 100. Tumewapendeza wateja wetu na pia kuwauzunisha,tumetegeneza pesa, lakini pia tumepoteza pesa, tumepitia majanga mengi, uchumi, kodi ya serikali, wengine wametufitini, wengine wametuibia na wengine    wametundanganya. Tumekaa kwa hii biashara, kusubiri kuona kitakacho tokea kesho.”

Wenye hii duka walijua maisha yana shida zake, lakini walijitoa kuendelea mbele, huku wakiwa na tumaini kwamba, kesho itakuwa  bora kuliko jana.

Wakristo wanao sababu kubwa kuvumilia nyakati ngumu. Kama jinsi wakati viwanda vimefungwa, riziki zetu ziko katika hatari. Viini vya korona vimetangazwa karibu nasi. Lakini Mungu ametuakikishia katika neno lake, nyakati nzuri ziko mbele yetu. Wenye haki watapata huruma zake Mungu. Je, wewe huko katika shimo la korona virus – basi jipe moyo katika neno na imani dani yake Kristo Yesu.

Hebu tuone:-

I.  NYENYEKEA KWA MAPENZI YA MUNGU (I PETRO 5:5-6) (SURRENDER YOUR WILL TO GOD)

  1. Chukua nafasi ya kunyenyekea
  • Tunaishi wakati kila mtu anafanya mapenzi yake mwenyewe.
  • Lakini kila mwana wa Mungu ajifundishe kumpa Mungu nafasi ya kwanza katika maisha (Wakolosai 1:18)
  1. Chukua nafasi ya mtumwa
  • Tukavae utu wa mtumwa
  • Yesu Kristo alijitoa kama mtumwa kwa wanafunzi wake (Yohana 13:4-16)
  • Mapenzi yake yakawe mapenzi yetu na mipango yake ikawe mipango yetu (Waefeso 6:6)
  1. Tukakubali mpango wa Mungu kwetu
  • Tunaponyenyekea Bwana atatukweza

II.  TUMA FADHAA ZAKO KWA MUNGU (I PETRO 5:7) (SEND YOUR WORRY TO GOD)

  1. Kumtwika fadhaa zetu zote ni kumwachia fadhaa zote kabisa.
  • Kristo ni mwenye nguvu na uwezo wa kubeba fadhaa zetu zote.
  • Ikiwa Kristo aliubeba ulimwengu wote na dhambi za dunia mzima. Basi yeye atakubeba wewe.
  1. Fadhaa zetu zote
  • Tusiwache fadhaa yeyote hata zile ndogo sana
  1. Tumpe fadhaa zetu zote na kwa ujasiri (Waebrania 4:15)
  • Mpe afya yako, nyumba yako, biashara na kazi yako.
  • Mpe na korona yote na janga zote, maana yeye ni tabibu wa karibu (Zaburi 91)

III. JIPE NGUVU KATIKA MWENENDO WAKO NA MUNGU (STRENGTHEN YOUR WALK WITH GOD) (I PETRO 5;8-9)

  • Tuwe makini zaidi juu ya ibilisi shetani
  • Je, ni nani anaye penda kukuweka katika shimo?
  • Tumehakikishiwa ushidi juu ya adui shetani
  1. Uwe makini zaidi juu ya uwepo wa shetani
  • Shetani yupo, yesu Kristo anaamini shetani yupo
  • Biblia inaamini shetani yupo
  • Mungu Baba anaamini kwamba shetani yupo
  • Hapa, Biblia inamwita “mshitaki wenu” adui ibilisi
  • Huyu ibilisi ni yeye aliyemshitaki Ayubu (Ayubu 1:6-12, 2:1-7)
  • Huyu shetani, ibilisi ni yeye yule, ni mzee wa kazi, ni wa miaka nyingi kuliko wewe na mimi
  1. Uwe makini juu ya nguvu za shetani
  • Shetani, ibilisi anafananishwa na simba
  • Simba anatumia nguvu nyingi sana (Mara14-21) kuliko mwanadamu
  • Hatumwezi shetani kwa nguvu zetu
  • Hata malaika mkuu Mikaeli akupigana na ibilisi (Yuda 9)
  • Simba ni hatari na wenye kutisha, kuguruma kwa simba kunasikika kilometa 8
  • Simba ananguruma zaidi usiku hili kuleta hofu.
  • Hofu inashindana na imani yetu.
  1. Uwe makini juu ya werevu wa shetani
  • Mpinge shetani – simama wima (Yakobo 4:7, I Yohana 5:4, I Yohana 4:4)

VI.  TAZAMA KAZI YA MUNGU (I PETRO 5:10) (SEE THE WORK OF GOD)

  1. Neema ya Mungu inatosha (II wakorintho 12:9)
  2. Dhiki itakuwako pamoja nasi (Yohana 16:33) Ayubu 14:1, Waebrania 13:5, Mathayo 28:20, Wafilipi 4:19)
  3. Utukufu wa Mungu ni wetu (ufunuo 21:27, 31:4, Warumi 8;18, II Wakorintho 4:17)
  • Tunaenda mahali ambapo shida za korona hazitapatikana.

MWISHO

  • Je, maisha yako, yako ndani ya shimo ya korona, hau ukosevu? Mjie Kristo sasa.
  • Kuna nguvu katika damu na jina la Kristo
  • Mpe Kristo mkono wako leo, Anaweza.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

1 thought on “JINSI YA KUTOKA KWA SHIMO LA KORONA”

  1. Thanks for message God bless you our dear pastor.may our good Lord keep you safe & never lack the desires of your heart.you really inspire me.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *