MFULULIZO: MAISHA NA NYAKATI ZA ELISHA
SOMO: 2 WAFALME 6:1-7.
Mtu wa Mungu anaweza kufaulu katika maisha yake kama ataamua kwa nguvu za Mungu kuvunja zile vikwazo. Na kukata vizuizi vinavyotoka kwa ufalme wa giza.
Katika kifungu hiki tunaona manabii walitambua mapungufu na vikwazo vyao kwa huduma yao kwa MUNGU.
Wakati mwingine tunapoona kufaulu katika maisha ya watu tunalia kwa wivu. Kwa nini haya yote haifanyiki kwangu? Kwa nini sipati baraka kama yao?
Tusipojiadhari tunapata kuchomeka na wivu na uchoyo juu ya wengine, kiasi tunaweza kuwachukia watu. Chuki nayo inatufanya kukosa kufanya kazi ili tupate mafanikio kma yao. Maisha hamna haki.
Mungu yuko na kitu spesheli kwa ajili ya kila mmoja wetu kulingana na utofauti weti.
Sis wote ni tofauti mmoja kwa mwenzake. Hakuna mtu mwingine duniani aliye kama wewe!! Mungu ametuumba tofauti. Tukiwa na talanta na uwezo tofauti. Hivyo usijilinganishe na mwenzako.
Vikwazo vyako na mapungufu yako ni tofauti na yale yangu.
Tunahitaji kujifunza kutokana na mapungufu na vikwazo vyetu.
Kifungu hiki kwanaanza na wana wa manabii wakitambua upungufu wa mahali walipoishi kuwa padogo zaidi kiasi pakawa kikwazo kwa kazi yao kwa Mungu.
Wana wa manabii wanamwomba nabii Elisha ruhusa ya kupanua mahali pale pa huduma yao.
Kiunabii kila mmoja wetu anahitaji kupanuliwa, vikwazo kuondolewa tukamtumikiwa Mungu kwa uwezo wetu wote.
Sasa ndio wakati wetu kukpanua ufalme wa Mungu tuliopewa. Hebu tuone jinsi ya kutoa vikwazo na mapungufu yetu.
UAMUZI WAO-WANA WA MANABII.
- Walitambua kamba kwa miaka mingi walikuwa katika mapungufu.
- Waliamua kuvunja kabisa vikwazo vyao na kupanua maisha yao.
- Tunahitaji kulia sana hozi yetu kuzidishwa kama kama Yabesi katika 1 Mambo ya Nyakati 4:9-10.
- Lakini kuzidisha hozi ni lazima kuwa na maono makuu juu ya Mungu wetu.
- Mungu ametupa kila kitu kinachoitajika kwa uungu na uzima.
- Mahali unapoishi kiroho panaweza kukupatia mapungufu makuu.
- Tunahitaji kupenda sana kupanuliwa na kuinuliwa, tusiishi katika mapungufu katika sehemu zote za maisha.
- Ni mapenzi yake Mungu kupanuliwa katika kila sehemu na kuzidishiwa katika yote.
- Lakini huwezi kuzidishiwa kama hamna tamaa na uamuzi wa kuishi katika makuu na baraka zaidi.
- Mungu wetu Yehova hana vikwazo na mapungufu yeyote.
- Ni mapenzi yake sisi sote tukaishi katika nguvu tele tele katika kila eneo ya maisha-Yohana 10:10.
- Kama hutaishi katika uzima tele basi tunaitaji kujua ni kwa nini-Yohana 8:36.
- Basi, sisi zote tukapate kuamua kuwa huru kutokana na vikwazo na mapungufu, huku tukipenda sana kuzidishwa hozi zetu bila kikwazo.
KUJIKAKAMUA KWAO-WANA WA MANABII.
- Katika maisha tafuta sana kujihusisha na watu walio na maono makuu, watu wanao mvuto wa kwenda mbele.
- Shetani anawalenga watu wale wanabeba neema kuu na kibali cha Mungu.
- Jinsi unavyofahamu Mungu ndivyo atakavyo jidhihirisha kwako.
- Hivyo usiwache kushindwa na kutofaulu kwako katika maisha kukuzuia kwenda mbele.
- Ukijikakamua kufikia baraka zake Mungu, Mungu atavunja vizuizi vyote mbele yako-Mika 7:8.
- Mungu wetu-Yehova hana vikwazo au mapungufu ya wakati, nafasi au hali.
- Mungu hana mipaka hivyo yeye anajibu maombi juu ya kila swali ya maisha yako.
- Jinsi ya kufurahia baraka zake:-
- Weka imani yako ndani ya Mungu pekee usimtegemee mwanadamu.
- Shinda kila shaka juu ya ahadi za Mungu kwako.
- Uwe na roho ya kuvumilia.
- Kumbuka Mungu hawezi kukukataza baraka zake.
- Mungu anafanya kazi yake wakati wake, si wakati wa mwanadamu.
- Mungu anakamilisha mapenzi yake juu yetu kwa ukamilifu wa wakati wake.
- Uwe mtiifu kwa Bwana. Yeye ndiye anaye mipango yote kwa kila swali ya maisha yako.
VIKWAZO VYAO WANA WA MANABII.
- Walipokuwa wakikata miti ya kupanua makao yao na kazi ya Mungu boriti ya chuma ya shoka ilianguka katika maji ya mto wa Yordani.
- Hiki kilikuwa kikwazo kikubwa kwao na zaidi ya hayo shoka lenyewe lilikuwa la kuazima.
- Ndoto zao zilitoweka mara.
- Mmoja wa wana wa manabii alilia kwa sauti kuu.
- “Ole wangu Bwana wangu kwani kiliazimiwa kile.”
- Elisha aliuliza “kilianguka wapi?” yule mwana wa nabii akamwonyesha.
- Elisha alikata kijiti akakitupa majini na lile chuma boriti ya shoka likaelea majini!!
- Muujiza huu watufundisha:-
- Mungu anao mpango kwa shida na matatizo yetu.
- Kama jinsi Mungu alivyowasaidia wana wa manabii, atatufanya vivyo hivyo.
- Tunapofika mwisho wa mawazo na nguvu zetu, Mungu atausika, hivyo kunao usaidizi na tumaini kwetu.
- Unapofika mahali pa kupoteza, dunia, shetani na mwili, watakueleza kwamba Mungu hajili na haoni shida zako.
- Lakini Mungu anao yote-Mithali 15:3; 2 Mambo ya Nyakati 16:9.
- Shida zako ni nafasi ya Mungu kukutendea mema-Waebrania 4:15; 1 Petro 5:7.
- Kwa chochote umeitwa na Mungu kufanya, chochote utakachopatana nacho katika njia ya maisha-jifunze kumwangalia na kumtazama Mungu kwanza.
MWISHO
- Mungu atatumia majaribu kutuleta mahali pa kumtegemea.
- Kuvunja mapungufu na vikwazo vya maisha utahitaji uaminifu, nia na kujikakamua.
- Lazima kukata shetani na vikwazo vyake anavyoweka katika njia na safari yako ya imani.
- Leo ni siku njema kuvunja vile vikwazo vya maisha yako.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
