Swahili Service YESU KRISTO YUARUDI TENA

KITI CHA ENZI – KIKUBWA, CHEUPE

UFUNUO 20:11-15

Kuna vitu kadha kuhusu kiti cha enzi Kikubwa, cheupe cha hukumu. Watakatifu na wenye dhambi wanaitaji kuelewa. Waliokufa wote tangu dunia  kuumbwa watafufuliwa toka kaburini na bahari wapokee hukumu kulingana na matendo yao      yalioandikwa katika vitabu vya Mungu.

Kiti hiki cha enzi ni kikubwa na ni cheupe kuonyesha utakatifu wa Mungu, hekima na ukuu wake aliye mzee wasiku (the ancient of days) (Danieli 7:9-10). Inchi na mbingu zikakimbia uso wake na mahali pao hapakuonekana.

Inchi hii na mbingu hizi lazima kupita hili inchi mpya na mbingu zipate kuja. Bahari, mauti na     kuzimu ndio makao ya wafu wenye dhambi.

Cha maana zaidi ni kujua kwamba hukumu hii ni ya kutisha sana mno. Hivyo, somo yetu     inatueleza juu ya kiti cha enzi, kikubwa na cheupe, hukumu hii itafanyika Yesu Kristo ajapo na baada yake kutawala miaka 1000 hapa duniani. Elewa kwamba wenye dhambi, wenye kumkataa Yesu Kristo, waliokufa watakaa makaburini yao muda mrefu sana!! Hukumu hii ndio ya kutisha na kuhuzunisha zaidi ya hukumu zote.

Hukumu hii ni juu ya wote waliomkataa Yesu Kristo Masihi wa Mungu aliye juu ya yote na wote. Huu utakuwa wakati wa kila mtu aliyekataa kuokoka atasimama mbele ya korti ya mbinguni, mbele ya kiti hiki cha enzi, kikubwa na cheupe hakuna rufaa, hakuna mawakili, hakuna kupimwa akili, hakuna mistrials, hakuna ongo, kama jinsi ya korti za Kenya, hakuna kabila lako na wakuu wa mashitaka hau maprosecuta, hakuna mauchawi ya kuchelewesha kesi na mafile kupotea, hakuna kesi kutajwa na kuamua siku ya kusikizwa kesi, kama jinsi hapa kwetu duniani. Lakini ushahidi utatolewa na mbingu, ukweli utasemwa na hukumu kutolewa hapo hapo.

Hebu tuone hukumu hii ya mwisho:-

  1. KITI CHA ENZI KIKUBWA CHEUPE NI TISHO KUBWA SANA
  2. HIKI NI KITI CHA ENZI (UFUNUO 20:11)
  • Hiki ni kiti cha mamlaka na ukuu wote.
  • Hiki ni kiti cha Mungu muumba mbingu na inchi.
  • Mbele ya kiti hiki cha enzi, hakuna mahali pa kujificha.
  • Mbele ya kiti hiki cha enzi hamna upuzi hau ujinga, hau udhuru.
  • Hiki ni kiti cha enzi cha Kristo.
  1. KIINI CHA NGUVU NA UWEZO
  • Aliyeketi juu ya kiti hiki cha enzi ni Yesu Kristo mwenyewe na Yohana alimtizama akaona ni Yesu Kristo!!
  • Yohana aliona alama za misumari, aliona Jeraha zake za msalabani, aliona mbavu zake jinsi alichomwa mkuki.
  • Huyu Yesu Kristo wengi walimkataa, sababu ya dini zao, zizizo na wokovu. Madharau yao, laana zao, matusi yao, walikataa kumwamini, lakini sasa, huyu Yesu Kristo ndiye hakimu wao. (Yohana 5:22)
  • Katika kiti cha enzi kikubwa, cheupe ni Yesu Kristo na Mungu Baba.
  • Kuja kwa Yesu Kristo kwanza, kulikuwa kama mtoto horini ya ngombe amevaa mavazi ya kitoto.
  • Sasa Yesu Kristo amevaa mavazi ya hakimu wa mbinguni.
  • Kuja kwa kwanza alilala katika hori, sasa ameketi juu ya kiti cha enzi, kikubwa cheupe.
  • Hapo kwanza Kristo alivaa taji ya miiba sasa amevaa taji za mbinguni!! Kifalme.
  • Hapo kwanza alibeba fimbo ya mchungaji mkononi, sasa amebeba nyundo ya hakimu mkuu!!
  • Hapo mwanzo alikuja kama kondoo wa kuchijwa, sasa amekuja kama simba wa kabila ya Juda.
  • Hapo kwanza alikuja kama mwokozi, sasa amekuja kama hakimu mkuu na mhukumu za dunia yote!!
  1. ISHARA ZA NGUVU ZOTE.
  • Hiki kiti cha enzi, kikubwa, cheupe sio tu kiti na nguvu zake lakini pia ni ishara ya uweza, mamlaka na nguvu zote. Kwa maana “inchi na mbingu zilikimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana” (V.11)
  • Je, wewe uliye mkataa na kukataa wokovu wake na njia zake kutakuwaje na hayo maisha yako?
  • Wenye dhambi waliomtemea mate uso na kungoa ndufe zake, watamtazama kwa kutishwa sana.
  • Siku hio tengemeo ya wengi, mali zao, fedha zao, benki zao, mijengo na magari yao yatakuwa yamepita na kukimbia uso wa yeye akaetiye katika kile kiti cha enzi.
  • Kila mpaka, mwamba, mlima, mto, nyumba, nyota, mwezi, zitakuwa zimepita.
  • Danieli aliwaona watu wa haina mbili katika hukumu. Kundi moja ilikuwa ikitumika mbele ya kile kiti cha enzi, kundi linguine lilisimama mbele ya kiti cha hukumu.
  • Waliookoka tayari watakuwa wamehukumiwa kazi zao, sasa wanaohukumiwa ni wenye dhambi.
  1. PILI, KITI CHA ENZI, KIKUBWA CHEUPE NI MWITO WA MWISHO MBELE ZA MUNGU. (UFUNUO 20:12-13)
  • Biblia inasema kwamba kunamahali tatu makao ya wafu wenye dhambi.
  1. Bahari
  2. Mauti
  3. Kuzimu
  • Haijalishi mahali pa mauti ya mtu, iwe ni baharini, motoni, majivu, kufufuliwa ni lazima.
  • Watu wengine wanataka kuchomwa maiti yao (crimination), lakini katika majivu hayo iliyotupwa katika mito hau katika bahari zote za dunia, utafufuliwa wewe!!
  • Kuna dini nyingi hivi leo, wanaofundisha kuwa kifo ndio mwisho ya mambo yote.
  • Wengine wanasema kama mtu anakufa, akaingia jihanamu yeye anayeyuka na kwa hewa na huo ndio mwisho wake.
  • Lakini Biblia inasema, “kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake.
  • Bahari ikawatoa wafu wake ndani yake.
  • Mauti nayo ikawatoa wafu wake wakasimama mbele ya hicho kiti cha enzi.
  • Haijalishi utakufia wapi na kuzikwa wapi, na kuchomewa wapi, lazima kufufuliwa wewe tu!!
  • Watakatifu, wakristo waliookoka wakifufuliwa wamepewa miili mpya kama jinsi mwili wa utukufu wa Kristo.
  • Lakini wenye dhambi watapewa miili ya milele utakayopata maumivu na kutengana na Kristo milele na milele, bila tumaini yeyote milele.
  • Hakutakuwa na mahali pa kujificha bahari imekwisha, mbingu zimepita, kuzimu imetupwa katika ziwa la moto – utaenda wapi we       usiyeokoka?
  • Ikiwa maisha yako yakale bado haijafunikwa chini ya damu ya Yesu Kristo, basi hukumu ipo kwako.
  • Hivyo ndungu na dada yangu kiti cha enzi kikubwa, cheupe ni cha kutisha na mwisho, kwa maana kesi ya Mungu haina rufaa. Utafanya nini na ukweli huu?

III. TATU, KITI CHA ENZI, KIKUBWA,    CHEUPE NI MAHALI PA UKWELI WOTE.

  • Mungu atakuwa na ushahidi wakutosha na wakweli kabisa.
  • Yohana anasema “nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi.”
  • Kutakuwa na watu wa tabaka mbali mbali.
  • Kutakuwa na watu wa ukuu tofauti tofauti.
  • Wafamle na waombaji, masikini na matajiri , wasomi na wasiosoma, wazuri na wambaya.
  • Hukumu hii ni hukumu kamilifu na ya kweli.
  • Biblia inasema “vitabu vilifunguliwa na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima na hao wafu wakahukumiwa sawa sawa na matendo yao.”
  • Biblia inataja vitabu saba (7) vitakavyo tumika katika hukumu ya mwisho.
  1. Kitabu cha kitambulisho chako – DNA na umbo (Zaburi 139:16) “macho yako yaliniona kabla hazijakamilika chuoni mwako ziliandikwa zote pia siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.”
  • Mungu hataweza kukusahau, hau kukufikiria wewe ni mtu mwingine.
  • Mungu anafahamu umbo lako, na viungo vyako vyote, anafahamu kila jambo juu yako!!
  1. Kitabu cha maneno yako (Mathayo 12:36, Malaki 3:16) “basi namwaambia, kila neno lisilo maana watakalolinena wanadamu, watatota    hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.”
  • Kila neno ulilosema limeandikwa katika kitabu cha maneno. Kila neno la laana, la kukashivu, la kulalamika, la uchungu na matusi, limeandikwa katika kitabu.
  1. Kitabu cha machozi (Zaburi 56:8) “umehesabu kutangatanga kwangu, uyatie machozi yangu katika chupa yako. Je, hayamo katika kitabu chako?”
  • Mungu ameandika machozi ya kila mtu uliyemfanya alie, hau kila mtu uliyevunja roho na moyo wake kwa vitendo vyako mbaya. Watu  uliowatendea machungu na kilio, Mungu     ameyaandika machozi yao katika kitabu chake!
  1. Kitabu cha matendo (Ufunuo 20:12)
  • Wafu walihukumiwa, sawasawa na matendo yao na kazi zao zilizoandikwa katika vitabu vya matendo.
  1. Kitabu cha mawazo ya siri ya wanadamu (Warumi 2:16) “katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.”
  • Mawazo ya siri, hata mbila kutenda dhambi yataukumiwa.
  • Je, utasimama wapi, kitabu hiki cha mawazo ya siri kinatisha moyo wangu, je wewe?
  1. Kitabu cha fursa na nafasi uliyopewa na Mungu (Warumi 1:18-32)
  • Kila mtu duniani amepewa fursa ya kuokoka, Mungu amenena nawe kwa njia nyingi. Kila nafasi uliyopewa imeandikwa katika kitabu.
  1. Kitabu cha uzima “na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima na hao wafu wakaukumiwa” (Ufunuo 20:12)
  • Je, jina lako limeandikwa katika kitabu cha uzima hau katika kitabu cha kuzimu na ziwa la moto?
  • NNE, KITI CHA ENZI, KIKUBWA, CHUEPE NI MAHALI PA HUKUMU YA MWISHO (UFUNUO 20:15)
  • “Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”
  • Ziwa la moto ni kubwa kuliko jihanamu na kuzimu, kwa maana Kuzimu, shetani na wote waliomkataa Kristo, na mauti watatupwa katika ile ziwa la moto!!
  • Ziwa la moto ndio mahali pa milele na milele pa waliopotea.
  • Je, wewe kweli unakubali kuingia hapo?
  • MWISHO
  • Wewe pamoja nami twaitaji kutambua kwamba leo ndio siku bora kuchangua kumwishia Kristo.
  • Je, katika vitabu vilivyo mbinguni, wewe umeandikwa katika kitabu gani?
  • Leo ni siku yako, ukikataa kuokoka hii nafasi imepotea na tayari imeandikwa mbinguni.
  • Fursa ni yako sasa
  • Ikiwa umeokoka, tafadhali jali sana matendo yako, maneno yako, mawazo ya siri katika moyo wako na machozi unayomwanga, kwa sababu ya kuwahudhi watu.
  • Amini sasa – ukaokoke.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *