Swahili Service

KUKAA KATIKA MAHALI PA SIRI

MFULULIZO: KARIBU NA MUNGU.

SOMO: ZABURI 91:1.

 

Kukaa katika mahali pa siri pake aliye juu ni mwaliko wa kupokea utimilifu wa uwepo na amani ya Mungu. Hapa ni mahali pa mawasiliano ya karibu na Mungu, hapa utapata kuongozwa na kupewa nguvu za Roho Mtakatifu-Zaburi 91:1, “Aketiye mahali pa siri pake aliye juu atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.”

Wazo la “Mahali pa siri” inaakilisha uhusiano wa karibu zaidi na Mungu. Hapa ndipo twapata usalama, amani na chakula cha kiroho. “Mahali pa siri” si mahali hapa duniani bali ni mahali pa kiroho.

Leo tunajifunza maanake “Mahali pa siri pake aliye juu, madhumuni yake kukaa mahali pa siri” na jinsi tunaweza kupalilia maisha ya ushirika wa karibu na Mungu. Hebu tujifunze:-

UFAHAMU WA “MAHALI PA SIRI.”

  • Mahali pa siri ni mahali pa kuhisi Mungu kwa njia ya kibinafsi, ni mahali pa kujificha, mahali pa kuhifadhiwa na Mungu.

Hapa ni mahali pa urafiki wa dhabiti na wa karibu zaidi na Mungu.

  • Hapa ni mahali pa ushirika na Mungu mbali na vizuizi vyovyote-Mathayo 6:6.

Hapa ni mahali pa kulindwa kutokana na adui wako wote.

  • Hapa unazingirwa na uwepo wa Mungu kutokana na dhoruba za maisha na vita vyote vya adui zako-Zaburi 91:1.

Hapa ni mahali pa Ufunuo, hapa Mungu mwenyewe anajifunua kwako kibinafsi.

    • Hapa unapata kumjua Mungu kwa karibu zaidi.
  • Hapa utajua tabia zake Mungu, mipango yake kwa maisha yako-Yeremia 33:3.

Hapa ni mahali pa kupumzika. Uwepo wa Mungu ni pumziko la amani. Hii ni amani dunia haiwezi kukupa-Kutoka 33:14.

  • Hapa, hapana wasiwasi wala kuangaika maisha.

Hapa ni mahali pa nguvu na uwezo.

  • Tunapokaa katika mahali pa siri pake aliye juu, tunapata nguvu mpya, tunabadilishwa, tunawezeshwa kiroho, kimwili na ki-hisia-Isaya 40:31.
  • Musa alifahamu siri ya kukaa karibu na Mungu, kiasi uso wake uling’ara kwa utukufu wa Mungu.

JINSI YA KUKAA KATIKA MAHALI PA SIRI.

  • Kukaa katika mahali pa siri pake aliye juu si jambo la kufanya safari moja, bali ni hali ya maisha kushirikiana na Mungu kila saa.

Kufanya maombi jambo la maana zaidi.

  • Maombi ni ufunguo wa kuingia mahali pa siri pake aliye juu.
  • Maombi ni mawasiliano na Mungu-Mathayo 6:6.

Tafakari neno lake Mungu. Neno la Mungu ndio sauti yake kwetu.

  • Kutafakari neno la Mungu kunafanya uhusiano wetu na Mungu kuwa na nguvu-Yoshua 1:8.
  1. Dumisha sifa na ibada. Ibada ni zaidi ya kuimba nyimbo, bali ni tabia inao mshukuru Mungu katika kila jambo-Zaburi 95:6-7.
  2. Jaribu sana kunyamaza na kutulia mbele zake Mungu-Hapa ni mahali pa siri pake aliye juu.
  • Mungu anaongea vyema katika utulivu-Zaburi 46:10.

Ishi maisha ya utii, maanake mahali pa siri ya aliye juu panahitaji utii wa amri zake-Yohana 14:15.

  • Mfalme Daudi alipenda sana kukaa katika nyumba yake Mungu-Zaburi 27:4.

FAIDA YA KUKAA KATIKA MAHALI PA SIRI PAKE ALIYE JUU.

  • Wale wanaokaa katika mahali pa siri pake aliye juu wanapata faida nyingi.
  1. Wanapata salama na ulinzi. Mungu anakuwa mahali pa kujificha adui, Mungu anapata kuwa ngome imara na ngao yao kutoka kwa silaha za adui-Zaburi 91:2-4.
  2. Amani na utulivu: Kukaa katika mahali pa siri pake aliye juu huleta amani ipitayo fahamu za mwanadamu katika nia zao, akili na mioyo-Isaya 26:3.
  3. Uongozi: Mahali pa siri pake aliye juu panaleta mwongozo, mwelekeo na uamuzi ulio bora-Zaburi 32:8.
  4. Kuzaa matunda na ukombozi wa kila hali:
  • Tunapokaa katika mahali pa siri pake aliye juu tunapata kuzaa matunda bora. Maisha yetu yanakuwa-Yohana 15:4-5, ukombozi wake unakuwa dhahiri zaidi-Zaburi 91:14-16.
  • Eliya nabii wa Mungu alifahamu sana “Mahali pa siri pake aliye juu”-1 Wafalme 17:1-6. Mungu alimlisha na kumhifadhi iwe ni pale Kerithi, pale Zeraphath na Karmeli.

VIZUIZI VYA KUKAA KATIKA MAHAI PA SIRI PA ELIYE JUU.

  • Hata ingawa ni mapenzi ya Mungu tukakae katika mahali pa siri pake aliye juu, kunao vizuizi vingi vya kutuzuia tusipate kuingia pale.
  1. Shughuli nyingi na vikwazo-Luka 10:40-42.
  2. Kuto kuungama dhambi zetu-Isaya 59:1-2.
  3. Kukosa imani-Waebrania 11:6.
  4. Kukataa nidhamu za kiroho na njia za neema.
  • Kutoomba, kusoma Biblia, kuingia ibada, kukosa Meza ya Bwana, kukataa ubatizo wa kibiblia, kukosa kujisafi-Yakobo 4:8.
  • Hofu na fadhaa-Wafilipi 4:6-7.
  • Martha alisumbuka sana kwa shughuli zake, akakosa baraka-Luka 10:38-42.

KUKAA KATIKA MAHALI PA SIRI PAKE ALIYE JUU.

  1. Mtumahi Bwana wakati wa dhiki na wakati usio na hakika-Isaya 41:10.
  2. Pata na kupokea nguvu kutoka kwa uwepo wake aliye juu-2 Wakorintho 12:9.
  3. Jitwike fadhaa zako kwake-1 Petro 5:7.
  4. Pata mapumziko kwake na katika ahadi zake-Zaburi 37:7; Zaburi 23:4.
  • Paulo na Sila walijipa moyo-Matendo 16:25.

MAOMBI.

  • Bwana, naomba unifundishe kukaa katika mahali pa siri pake, kila siku ya maisha yangu.
  • Baba, nisaidie kupata amani na mapumziko katika uwepo wako.
  • Roho Matakatifu, nivute kwako na unisaidie kukaa katika uwepo wako.
  • Bwana, nitolee vikwazo vyote vya kutotumia wakati nawe.
  • Bwana, nisaidie kukutegemea katika kila majira ya maisha yangu.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *