Swahili Service

KWA KILA MACHWEO KUNA MACHEO

MFULULIZO: YAKOBO; ALIFANYA MIEREKA NA MUNGU.

SOMO: MWANZO 28:1-22

 

Kwa kila machweo ya  jua kunayo macheo. Yakobo aliota ndoto inayotuweka moyo mkuu kumtegemea Mungu wakati wa magumu na nyakati za shida katika maisha yetu. Hebu tuone ndoto aliyopata Yakobo. Je, wewe unapitia katika machweo katika maisha? Pengine ulikuwa na matarajio mengi ya juu sana kwa maisha yako lakini sasa ndoto zako zimegonga mwamba. Umetazama na kumbe uko mbali sana na ahadi na sasa maisha yako katika machweo na mwisho wa siku yako. Leo niko hapa kueleza kwamba katika giza na usiku wako Mungu angali hapa. Mungu anao uwezo wa kuyageuza mambo kwa sababu kila machweo kunao macheo. Katika Mwanzo 28 Yakobo amemdanganya ndugu yake Esau urithi. Sasa Esau yuataka kumuua Yakobo. Hebu tuone:-

YAKOBO ALITOROKA KUTOKA NYUMBANI.

  • Yakobo alitoroka, maisha yake yalikuwa hatarini.
  • Yakobo alitoroka haraka sana bila kwaheri.
  • Yakobo yuko katika safari ndefu sana 800km kutoka Beer-Sheba mpaka Harani.
  • Ilikuwa safari kama jinsi babuye Ibrahimu aliyetoka Harani mpaka Beer-Sheba.
  • Harani ilikuwa mbali kiasi Esau hangeweza kumwona Yakobo.
  • Rebeka naye alikuwa na lengo, Yakobo apate mke huko kwa ndugu zake.

BARABARA YA KWENDA HARANI

  • Yakobo alikuwa haraka kutoroka nyumbani lakini hakujua yatakayo mpata njiani- Mwanzo 28:11.
  • Yakobo alipofika mahali fulani (Luzu) na jua chwea na giza likampata Yakobo.
  • Kumbuka hakuna mtu anaweza kujificha mbali na Mungu.
  • Leo ikiwa kuna mtu hapa jua lake limechwea, huwezi kwenda popote, huoni nuru yoyote ila giza tupu. Mungu anao mpango wa ajabu kwa ajili yako.
  • Huenda umepoteza kazi, umefiwa, umeachwa, umetupwa, au unakimbia adui zako, Mungu yupo karibu zaidi na wewe leo.
  • Yakobo amefika karibu na mji wa Luzu.
  • Yakobo hajui mahali alipo, amejaa hofu. Yakobo akatafuta jiwe la kuweka kichwa chake akalala usingizi.
  • Pengine Yakobo hakupata usingizi kamwe, aliwaza babaye mzee, mama mkongwe, aliwaza juu ya ndugu yake Esau, aliwaza juu ya kifo na mauti.
  • Nyota zilipotokea angani na sauti za usiku zilipoanza, Yakobo aligundua kumbe alikuwa peke yake tangu kuzaliwa.
  • Yakobo aligundua kuwa hakuwa na nyumba, pesa, alikuwa hawezi na mpweke zaidi.
  • Yakobo alipolala aliota ndoto mashuhuri zaidi katika historia ya wanadamu- Mwanzo 28:12-13.

NGAZI KUTOKA MBINGUNI MPAKA DUNIANI

  • Katika ndoto yake Yakobo aliona ngazi iliyotoka mbinguni na kusimama duniani!!
  • Ngazi hiyo ilisimama alipolala Yakobo.
  • Juu mbinguni ilipotoka ngazi hiyo, palikuwa na Mungu mwenyewe.
  • Malaika wengi walikuwa wakipanda na kushuka.
  • Mungu alikuwa bado hajanena na Yakobo hapo awali. Lakini Mungu alinene na Ibrahimu na Isaka.
  • Yakobo alishika imani ya babu na baba yake lakini hakuwa na imani ya binafsi.
  • Yakobo hakuwa na wokovu wake binafsi. Hakumjua Mungu kibinafsi.
  • Katika heka heka za maisha Mungu alijidhihirisha kwa Yakobo.
  • Mungu anaongea na sauti ndogo wakati wa raha lakini anaongea kwa sauti ya tarumbeta wakati wa shida zetu.
  • Si watu wengi katika Biblia waliona malaika, Yakobo ni mmoja wa wachache wale.
  • Malaika ni watumishi wa wale watakaoridhi ufalme wa Mungu.
  • Malaika wanafanya mapenzi ya Mungu, wanaleta ujumbe toka mbinguni.
  • Malaika wanatoa ripoti zetu mbele ya Mungu.
  • Malaika ni walinzi wetu, wanapigana vita vyetu.
  • Leo malaika wa Mungu wanakulinda wewe.
  • Juu mbinguni Mungu Baba alisimama, Yakobo mle chini, Mungu huko juu na malaika wengi sana katikati ya ile ngazi.
  • Maono na imani ya Yakobo hapo mbele yalikuwa kwamba Mungu ni mkuu sana kiasi anaishi mbali sana na watu wake- kumbe Mungu yu karibu na kila mmoja wetu- Matendo 17:24-29.
  • Yakobo alidanganya ndugu yake kwa sababu aliona Mungu yuko mbali zaidi kiasi tuchukue sheria mkononi.
  • Tunafanya dhambi kwa sababu twaona Mungu yuko mbali sana!!
  • Mwanzo 28:15- “Nipo pamoja nawe,” “Nitakulinda kila uendako,” “Nitakuleta tena mpaka nchi hii,” “Sitakuacha kamwe,” “Nitatimoiza ahadi zangu kwako.”
  • Mungu wetu yu karibu sana nasi. Ngazi yake inatembea pamoja nasi kila saa.
  • Nipo pamoja nawe, ulipomdanganya Esau, ulipokimbia popote pale.
  • Mungu (Yehovah) yu karibu na wewe kila saa.

TAFSIRI YA NDOTO YA YAKOBO

  1. Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu ilidhibitishwa- Mwanzo 28:13.
  • Ardhi- “Nitakupa nchi hii”- 28:13.
  • Uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi.
  • Utaenea pande zote.
  • Katikati yako na kupitia kwako jamii zote za dunia zitabarikiwa.
  • Niko pamoja nawe.
  1. Ahadi ya Mungu kwa Yakobo ni kama ile ya Ibrahimu- Mwanzo 12:1-3.
  2. Yakobo alipoamka kutoka usingizi wake alisema, “kweli Mungu yuko hapa, hii ndio nyumba ya Mungu (BETHELI) hili ndilo lango la mbinguni- 28:16-17.
  • Yakobo aligundua ukuu wa Mungu, uwepo wa Mungu.
  • Jua lako linapotua Mungu yupo, unapopitia dhiki Mungu yupo pamoja nawe, unapokosa kazi Mungu yupo, watoto wanapo toroka, unapokuwa mgonjwa, unaposalitiwa na watu, ndoa yako inapokuwa na shida, ndoto zinapovunjika Mungu yupo nawe.

MADHABAHU NA NADHIRI- Mwanzo 28:20-22

  • Yakobo alijenga madhabahu pale Betheli- Luzu.
  • Yakobo aliweka nadhiri.
  1. Mungu akiwa pamoja nami.
  2. Akinilinda kwa njia niendayo.
  3. Na kunipa chakula nile.
  4. Na nguo nivae.
  5. Nikirudi nyumbani kwa Baba yangu.

Basi;-

  1. Wewe Mungu utakuwa Mungu wangu.
  2. Jiwe hili litakuwa nyumba ya Mungu.
  3. Kati ya kila unipayo nitakutolea fungu la kumi.

Leo hii Yesu Kristo ndiye daraja ya kwenda mbinguni. Yesu Kristo ndiye ngazi ya mbinguni.

Yesu Kristo ndiye jibu la maombi yetu na suluhisho ya kila shida tulionayo.

 

MWISHO

  • Je, leo machweo yako yakoje?
  • Shida zako ni njia ya Mungu kukutana nawe.
  • Kila machweo yana macheo yake.
  • Mapambazuko yako ni sasa, mjie Mungu wako ahadi zake hazivunjiki daima. Ngazi ya Mungu ipo mahali uliposaza, maombi yako yanajibiwa sasa!!
  • Mwanzo mpya ni kwako sasa!!

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *