SOMO: WAGALATIA 4:1-8.
Krismasi inao maana tofauti kwa watu tofauti. Kwa watu wengine Krismasi ni wakati wa kupeana zawadi, miti ya Krismasi, maua kwa milango na Santa Claus. Kwa watu wengine Krismasi ni wakati wa hasira, hawapendi kusikia Mungu na habari za Yesu Kristo. Wengine hawapendi Krismasi kwa maana Krismasi ni Kristo na maana ya sikukuu ni Kristo Yesu. Kwa wengine Krismasi ni wakati mgumu sana kwa sababu ya umaskini, ipweke, makumbusho ya unchungu, wengine wana sababu ya kuchukia Krismasi.
Kwetu tunaompenda Yesu Kristo Krismasi ni wakati wa kusheherekea kuzaliwa kwa Mwokozi wetu Yesu Kristo hapa duniani. Ni wakati wa kuabudu, kukumbuka na kuwaza neema ya Mungu kwetu tuliookoka.
Kwetu tuliookoka Krismasi ni wakati wa furaha, amani na kushangaa ukuu wa MUNGU kutukomboa kutoka dhambi.
Watu wengi wanao shida kwamba Yesu Kristo alizaliwa na bikira-Wagalatia 4:4. Hakuna mwanaume alihusika kwa kuzaliwa kwa Kristo. Bila ubikira hatuwezi kuokoka!!
Kukataa ubikira wa Mariamu na kuwa Yesu Kristo alizaliwa na bikira ni kukata neno na ushuhuda wa Mungu. Kukataa ubikira wa Mariamu ni kukataa uungu wa Yesu Kristo. Kukataa ubikira ni kukataa Injili. Kukataa ubikira wa Mariamu ni kupotea dhambini na kuishi katika ziwa la moto yaani jehanamu.
Leo hii nataka kujibu swali “Kwa nini Yesu Kristo alizaliwa na bikira? Hebu tutazame:-
UKWELI WA BIKIRA KUZAA-Wagalatia 4:4.
“Mungu alimtuma mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke bikira.”
- Kila kuzaliwa ni muujiza. Jinsi mwanaume na mwanamke kwa kuja pamoja mtoto anazaliwa ni muujiza kweli.
- Tazama-
- Kuzaliwa kwa Isaka-Ibrahimu na Sarai-Mwanzo 21.
- Kuzaliwa kwa Samsoni kupitia kwa Manoa na mke wake-Waamuzi 13.
- Kuzaliwa kwa Samweli kupitia kwa Elkana na Hannah-1st Sam. 1.
- Yohana Batizaji kupitia Zakaria na Elizabeti-Luka 1.
- Pamoja na hayo yote, kuzaa ni kawaida, mwanaume na mwanamke wanausika.
- Lakini Yesu Kristo ni tofauti na wote. Alizaliwa na mwanamke pasipo mwanaume!!
- Yesu Kristo alifika hapa duniani bila kuhusika kwa mwanaume.
- Kuzaliwa kw Yesu Kristo ni kutimiza unabii kwa Adamu na Hawa-Mwanzo 3:15.
- Mariamu peke yake, kwa wanawake wote ndiye pekee alikuwa na mbegu “mbegu ya mwanamke.”
- Mwanamke wa kawaida anabeba yai na mwanaume anabeba mbegu.
- Kuzaliwa kwa Yesu Kristo ni kwa upweke, amezaliwa na bikira pasipo mwanaume.
- Isaya anaposema juu ya bikira ananena kwa neno ya Kiebrania “Almah”-mwanamke asiyejua mwanaume.
- Kwa bikira kuzaa ni muujiza na tena ni ishara.
- Malaika Gabrieli pia alishuhudia ubikira wa Mariamu-Mathayo 1:18-23.
- Mariamu alikuwa bikira na Mariamu alikaa bikira mpaka kuzaliwa kwa Yesu Kristo-Mathayo 1:25.
MATOKEO YA KUZALIWA NA BIKIRA-Vs. 4.
“Amezaliwa chini ya sheria.”
- Baba wa Yesu Kristo ni Mungu Baba-Luka 1:32, 35; Mathayo 1:23.
- Yesu Kristo alizaliwa chini ya sheria, “chini ya sheria” Maanake ni kwamba Kristo alijilazimisha chini ya sheria ya Musa; yaani torati.
- Yesu Kristo ni Mungu katika mwili-Yohana 1:14.
- Mtume Paulo anaeleza jinsi Mungu alifanyika kuwa mwanadamu-Wafilipi 2:5-8.
- Matokeo ya kuzaliwa na bikira ni kwamba Yesu Kristo ambaye ni Mungu alizaliwa kama mwanadamu, aliishi kama mwanadamu, alikufa kama mwanadamu.
- Yesu Kristo alikuwa na wazazi wanadamu-Luka 1:21; Wagalatia 4:4.
- Yesu Kristo alikuwa na mwili kama mwanadamu. Alikuwa na mwili, roho na nafsi-Mathayo 26:12; 26:38; Luka 23:46.
- Pamoja na kuwa mwanadamu, Yesu Kristo alikuwa Mungu-Mathayo 18:20; Waebrania 1:3.
- Yesu Kristo alikuwa MUNGU na pia mwanadamu safari moja (hypostatic union).
SABABU YA YESU KRISTO KUZALIWA NA BIKIRA-Wagalatia 4:5.
“Kusudi awakomboe hao walikuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana.”
- Bei ya ukombozi ni kubwa zaidi.
- Ilibidi Yesu Kristo achukue mahali pa mwanadamu, “Alizaliwa na mwanamke.”
- Ilibidi Yesu Kristo kuchukua laana ya mwanadamu, “Alizaliwa chini ya sheria.”
- Chini ya hukumu na sheria-Warumi 3:23.
- Sababu ya ukombozi ni kufanywa “Wana wa Mungu”-Wagalatia 4:5-6.
- Hatungekuwa wana wa Mungu bila kukombolewa kwa damu ya Yesu Kristo.
- Kufanywa wana wa Mungu “Huiothesia” ni kitendo cha Mungu cha kutufanya wana wa Mungu-Yohana 3, kuzaliwa upya.
- Sababu ya ukombozi ni kupata kumpokea Roho Mtakatifu-Vs. 6; Warumi 8:14-17.
- Tumepewa Roho Mtakatifu, Roho Analia “Abba Baba.”
- Tumepewa neema ya kufanana naye Mungu.
- Yesu Kristo hakuja tu kutukomboa kwa dhambi na utumwa wa dhambi, bali alikuja kuturejesha kwa uhusiano na Mungu Baba.
- Kwa imani ndani ya Yesu Kristo, sisi si watumwa tena-sasa ni wana wa Mungu.
- Kufanywa kuwa mwana (adoption) kulibadilisha kitambulisho na msimamo.
- Kufanywa mwana (adoption) ndio marupurupu ya Injili.
- Katika kufanywa mwana muasi alisamehewa, alikatishwa katika meza ya chakula na kupewa jina ya jamii.
MWISHO
- Kumbuka wakati wa Mungu ndio mwema.
- Yesu Kristo alikuja kutukomboa kutoka dhambi.
- Yesu alikuja pia kutufanya kuwa wana wa Mungu.
- Kama bado kuokoka, leo ni utimilifu ya wakati kwako kuokoka.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO. - September 21, 2025
- GOD GUIDES OUR DESTINIES. - September 21, 2025
- GOD OF THE BREAKTHROUGHS - September 10, 2025