Swahili Service

KWA NINI PAULO HAKUOGOPA KIFO?

MFULULIZO: MATENDO YA ROHO MTAKATIFU

UJUMBE: KWA NINI PAULO HAKUOGOPA KIFO?

SOMO: MATENDO YA MITUME 21:1-15

MHUBIRI: REV. DR. WILLY MUTISO.

Mtume Paulo hakuogopa siku zijazo, mauti na milele. Paulo alikuwa katika safari ya kwenda Yerusalemu. Katika safari hii alikawia kwa siku saba mle Kaisaria katika nyumba ya Filipo mhubiri wa Injili. Paulo alipokaa katika nyumba na Filipo, mambo mengi yalifanyika.

  1. Kwanza-ishara za kumkataza Paulo kwenda Yerusalemu zilitolewa-Vs. 10-11.
  2. Pili-watu wa nyumba ya Filipo, na nabii Agabo kutoka Uyahudi na pia kundi lililokuwa katika safari pamoja na Paulo walimkataza Paulo kwenda Yerusalemu kwa maana mabaya mengi na dhiki zilimngoja Paulo mle Yerusalemu. Kwa sababu walimpenda Paulo, walitumia mbinu zote kumkataza Paulo asiende Yerusalemu-Vs. 12.
  3. Paulo aliwaeleza wote kwamba alikuwa tayari kufa na kwamba hakuogopa mauti na milele. Paulo aliamini kutii Roho Mtakatifu kuliko ndugu zake katika Injili. Kila mmoja wetu anatazamia milele, lakini je, wewe pamoja nami tunaweza kutazamia siku zinakuja mbele yetu na milele mbinguni?
  4. KWA SABABU DHAMBI ZAKE ZILISAMEHEWA
  • Kitu kinacho mfanya mtu kuogopa ni dhambi-Mwanzo 3:7-9.
  • Dhambi inaleta hukumu, hukumu nayo inaleta aibu na aibu inaleta kujificha kutoka kwa Mungu na watu.
  • Kuhukumiwa ni shida kubwa ya mwanadamu.
  • Bila suluhu hukumu inaleta tabia inayo mwaribu mwanadamu.
  • Damu ya Yesu Kristo iliyomwagika inaosha dhambi zote na dhamiri zetu.
  • Damu ya Yesu Kristo imeosha dhambi zetu, kiasi sisi tulikuwa mbali tumeletwa karibu na Mungu wetu-Waefeso 2:11-13.
  • Damu ya Yesu Kristo pekee inaosha dhamiri zetu kutoka kwa kazi zetu, tuweze kumtumikia Mungu aliye hai.
  • Mfalme Napoleon wa Ufaransa alishindwa vita mahali paitwapo Waterloo huko Belgium. Katika map yake aliweka alama nyekundu mahali pale. Alipokuwa karibu kufa kwake alisema “Kama si ile alama nyekundu, leo ningekuwa mfalme wa dunia yote.”
  • Shetani leo hii angali anatazama msalaba wa Yesu Kristo na kusema “Kama sio alama ya damu ya Yesu Kristo ningekuwa mfalme wa dunia yote.”
  • Kama sio pale Kalvari tungekuwa dhambini!!
  1. KWA SABABU YA USHUHUDA NA KUOKOKA KWAKE-Matendo 9
  • Muujiza wa wokovu.
  • Paulo alikuwa adui mkuu wa Yesu Kristo na ukristo.
  • Juhudi za Paulo kukomesha ukristo.
  • Paulo alikuwa na juhudi kuu kumaliza kanisa la Yesu Kristo.
  • Jinsi ya kuokoka kwake.
  • Aliona mwangaza mkuu.
  • Alisikia sauti ya Yesu Kristo.
  • Alibadilishwa kabisa-Matendo 9:12, 2 Wakorintho 5:17.
  • Alipata tumaini ya milele.
  • KWA SABABU PAULO ALIPATA MSINGI IMARA KWA MAISHA YAKE.
  • Maisha ya Paulo haikurudi kuwa kama zamani.
  • Msingi wake ulikuwa Yesu Kristo na tumaini ndani ya Mwokozi-Waebrania 12:18-24.
  • Maisha yako inapojengwa juu ya Yesu Kristo hakuna haja ya kuogopa dhoruba za maisha haya-1 Petro 2:6.
  • Ujasiri katika Yesu Kristo ni bima dhidi ya dhoruba na matisho ya dunia hii.
  • Paulo alikuwa na ujasiri juu ya uzima wa milele, hivyo kifo na mauti hazikuwa tisho kwake-Wafilipi 1:21.

Mwili bora, nyumba bora, marafiki bora.

  1. KWA SABABU PAULO ALIFAA AHADI DHABITI.
  • Paulo alikuwa na ahadi za Mungu, Mungu asiyeweza kudanganya-Yohana 5:24; 3:36; 3:16; 10:28.
  • Tumepewa ahadi dhabiti zaidi-Waebrania 10:23; 2 Petro 1:4.

MWISHO

  • Je, wewe unaweza sema kwamba “Niko tayari kufa?”
  • Mtume Paulo alikuwa tayari kuingia milele ya Mungu.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *