Swahili Service

LAZIMA KUSUBIRI WAKATI WA MAVUNO

MFULULIZO: JINSI YA KUJISTAHIMILI DHORUBA ZA MAISHA

SOMO: MATHAYON 13:24-30

Wakati huu wa Corona Virus (COVID-19), watu wengi duniani; wawe watoto wa shule, wazazi, waajiri na waajiriwa, wamejiuliza “Kwa nini Mungu anaruhusu maovu duniani (Why does God allow evil?).” Yesu Kristo Alijibu swali hili kwa njia ya mfano wa Kwekwe.

Pasta mmoja kwa jina, Rev. John Templeton, aliyekuwa rafiki na mweza na Billy Graham kwa miaka mingi alirudi nyuma ki-imani. Alimwacha Mungu kwa sababu gani?

Kanisa lake lilikuwa kubwa, washirika wa kanisa lake walimpenda sana, alihubiri duniani kote pamoja na Billy Graham. Sisi tuliyemjua Rev. John Templeton tulimpenda sana lakini alimwacha Mungu akawa Agnostic. Agnostic, ni mtu anayekuwa na mashaka kama Mungu yupo au kama Mungu hayupo. (Agnosticism is one giant doubt of the existence of God). Kwa nini Rev. John Templeton alipata mashaka haya ya kushuku kwamba Mungu hayupo? Ilianza na kutazama picha! Katika gazeti moja liitwalo “Life Magazine”. Ilikuwa ni picha ya mwanamke mwaafrika. Kulikuwa ni wakati wa kiangazi kubwa Afrika Mashariki, yaani wanyama walikufa njaa na kiu wakati huo. Ndiposa, mwanake huyu na mtoto wake walipigwa picha ya huzuzni nyingi.

Templeton alipoitazama picha akajiuiliza, Je, Kama Mungu Yupo, kwa nini anaacha njaa, kiu na umaskini duniani, zaidi Afrika?

Kama Mungu ni Muumba dunia na mbingu kwa nini haileti mvua kwa wakati wake bila kuchelewa? Hivyo Rev. John Templeton akwamwacha Mungu, akaacha kuihubiri injili ya Kristo na akakufa akiwa Agnostic!!

Ninapoihubiri injili ninakutana na watu wengi walio na swali kama la Rev. John Templeton “Ikiwa Mungu Yuko na ikiwa Mungu ni Pendo, basi kwa nini kuna uovu duniani.” Ni jambo la kweli unapotazama dunia hii, unaposikiliza Radion na kutazama kwenye runinga unaona kwamba kuna jambo mbaya hapa duniani:-

  • Katika dunia hii kwa kila dakika moja wanawake wanapigwa na kuumizwa na wanaume.
  • Wanawake 50 wananajisiwa na wanaume kila dakika.
  • Zaidi ya watu 300 wanakufa kila siku katika ajali ya barabarani kwa sababu ya ulevi wa pombe.
  • Kuna wizi wa kimabavu 5 kila nukta!
  • Watoto 500 wanaumizwa kila dakika duniani.
  • Yesu kristo alipoulizwa swali hii alijibu kwa mfano wa Mavuno. (Mathayo 13:24-30)
  • Watumishi wa Bwana tajiri walimuuliza maswali tatu. Maswali haya tatu ndiyo yanaoulizwa zaidi hivi leo.

Ebu tujifunze:-

I.  KUPANDA NGANO NZURI (Mathayo 13:24-27)

  • Swali la kwanza la watumishi lilikuwa, “Je, mbegu la ngano iliyopandwa ilikuwa nzuri?”
  • Waliuliza juu ya upandaji wa mbegu.
  • Pengine waliona mbegu ilichanganywa pamoja na magugu.
  • Hivyo ndivyo watu wa leo wanauliza wanapoona vita duniani, njaa, kukosa haki, chuki na ubaguzi wa rangi na magonjwa kama Corona Virus.
  • Wanapoelezwa Corona Virus ilibuniwa kuua hailiki ya watu.
  • Wanapoelezwa chanjo ya Corona linaletwa Afrika kuwaangamiza.
  • Wengi wanasema basi hii ni shauri la Mungu.
  • Mwanzo 1:31- “Mungu Akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya sita”
  • Mungu Aliumba viumbe wazuri sana na Mungu Akaazimia hivyo.
  • Mwenye shamba alipanda mbegu nzuri sana. Je, magugu yalitoka wapi?
  • Wewe na mimi tulizaliwa tukiwa watoto wazuri na kupendeza.
  • Wewe haukuzaliwa mlevi, msherati, mvuta sigara na bangi, mwizi muuaji, Malaya, mlawiti, mdanganyifu, jambazi, mfisadi n.k.
  • Kila tabia ni kujifunza (Behavior is all learnt).
  • Maovu haya yametokana na wewe!!
  • Mwanzo 1:26-27:- “Mungu akasema, na Tumfanye mtu kwa mfano Wetu na kwa sura Yetu, wakatawale na samaki baharini, ndege wa angani na wanyama wa inchi yote pia kila kiumbe kinachotambaa juu ya nchi”
  • 27-Mungu akaumba kwa mfano wake,kwa mfano wa Mungu alimuumba mwanamume na mwanamke (male and female).
  • Mfano wa Mungu maana yake ni kwamba mwanadamu amepewa hiari ya kuchagua kati ya mema na mabaya.
  • Umeumbwa na Mungu ukiwa na uhuru(freedom)ukiwa na uchaguzi wa binafsi(choice)ukiwa na kuwajibika(Accountability).
  • Hakuna uhuru bila uchaguzi ,Hakuna uchaguzi bila kuwajibika.
  • (Freedom comes with choice and choice comes with accountability).
  • Je,matokeo ya uchaguzi wa nafsi ya mwanadamu ni nini?(what are the results of human choice?) .
  • Mwanadamu alichagua kumwasi Mungu.
  • Mbegu aliyopanda Mungu ni nzuri lakini mwanadamu aliichanganya na dhambi zake.
  • Mungu aliumba uwepo wa uovu ,mwanadamu alichagua uovu,hivi kiini haswa cha uovu si Mungu, lakini uovu ulikuja sababu ya uhuru wake mwanadamu.
  • (God created the possibility of evil, people actualized the potentiality, and the source of Evil is not God’s power but man’s freedom).
  • Mungu aliumba vitu vyote vikiwa vyema lakini mwanadamu alichafua yote.
  • Mungu aliumba nyimbo lakini mwanadamu alichafua nyimbo.
  • Mungu aliumba tendo la ndoa (ngono) lakini mwanadamu alichafua ngono.
  • Mungu aliumba dunia mzuri lakini sasa mwanadamu ametengeneza viini vya korona virus.
  • Sasa ugonjwa unatengenezwa kwa bihashara za
  • Mwanadamu anatengeneza viini hili atengeneza dawa ,hili atengeneze fedha.
  • Wengine wanatengeneza vita duniani,wengine wanatengeneza chakula sumu,mayae sumu,maziwa sumu,nyama sumu,maji sumu hili kuua watu halaiki,hii ndio dhambi.
  • Uchaguzi wetu ndio umeleta kuanguka na ufisadi duniani.
  • Hivyo tumezaliwa katika dunia mbaya kwa sababu ya dhambi.
  • Uchaguzi na uhuru wa mwanamke  umefanya mimba mahali pa hatari kwa watoto.(the most dangerous place for the human baby is in the mother’s womb.)
  • Kwa sababu ya dhambi mwanamke amekuwa ndiye muuaji mkubwa duniani.
  • Kila mwanamke wa kawaida duniani ametoa  mimba sita katika maisha yake!!.
  • Lakini kila mimba inayotolewa,mwanamume amelipia gharama za upwaji  mimba!!uovu.

II.  KUNG’OA YALE MAGUGU (MATHAYO 13:28-29)

  • Swali la pili watumishi wa Bwana mkulima tajiri ni “wataka tuyakusanye haya magugu?”(Can we fix the problems).
  • Watu wengi wanauliza Je,ikiwa Mungu ni mwenye uwezo kwa nini  hajafanya chochote juu ya uovu duniani?.
  • Je,Mungu ni mwenyezi ,kwanini asimalize coronavirus-mara moja.
  • Hivyo wengi wanaona dhambi ni shauri ya Mungu.
  • Ni kweli,Mungu anao uwezo wa kumaliza uovu na dhambi na mahafa yote, lakini Mungu anasema “subiri mpaka wakati wa mavuno” (God is saying wait until the time of harvest)
  • Mungu anangojea mpaka wakati unaofaa kumaliza dhambi na uovu duniani.
  • Mtume Petro aliwajibu watu wa siku zake walipouliza swali hilo
  • (II Petro 3:9-10) “Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikie toba. Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi, katika siku ile mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa na inchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea”
  • Mimi ninapendezwa na subira na uvumilivu wa Mungu, maana kama si Mungu alinisubiri.
  • Kama Mungu aliyang’oa magugu miaka chache iliyopita – basi mimi ningalikuwa wapi?
  • Mimi nigekuwa katika magugu yale!
  • Kila mmoja wetu ni chombo cha neema yake Bwana Mungu.
  • Hata wewe bado kuokoka, neema za Mungu zinakusubiri, Mungu akiyang’oa magugu wewe ni moja wao.
  • Laiti leo kama ugalijua yaletao Amani kwa hio nafsi yako ungalimwita mwokozi sasa na kuokoka.
  • Yanayongojea ulimwengu huu ni mambo ya kutisha sana – hukumu yaja.

III.  KUNGOJEA MAVUNO (MATHAYO 13:30)

  • Swali ya tatu haikuulizwa na watumishi wa huyu mkulima tayari – lakini mimi ningeulizwa “basi tutafanyaje na magugu”
  • Mungu mwenyewe asema “yaacheni magugu mpaka wakati wa mavuno”
  • Kuna wakati unakuja Mungu ataishungulikia dhambi, shetani na wenye dhambi mara moja.
  • Ngano na magugu yatatenganishwa wakati wa mavuno.
  • Sasa hii katika makanisa yote, kuna ngano na wachungaji magugu.
  • Sasa makanisani kuna wachungaji – ngano na wachungaji magugu.
  • Sasa katika makwaya na viongozi wa ibada kuko na ngano na magugu
  • Tuwatenganishe sasa? Hasha, Bwana wa mavuno anasema subiri wakati wa mavuno.”
  • II Petro 3:11 “Basi kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa. Mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu.”
  • Siku moja tu, siku inaokuja Mungu atafanya kila ubaya kuwa uzuri na kumaliza dhambi na wenye dhambi mara moja.
  • Wakati wa mavuno hukaribu sana
  • Yesu amesema, “basi kesheni na kuomba maana hamjui siku ya mavuno (Marko 13:35-36)
  • Damu ya Yesu Kristo ni nyingi na inauwezo wa kuokoa kila mtu – lakini lazima kumpokea Kristo binafsi.
  • Ni miaka mingi tangu sabuni kubuniwa duniani lakini watu wangali wachavu.

MWISHO

  • Tusimlaumu Mungu kwa dhambi na uovu duniani-Anawaita wote waokoke.
  • Wakati wa mavuno ni karibu , Je wewe ni ngano safi au magugu?.
  • Kama bado kuokoka- leo mjie Mwokozi wako,tubu dhambi zako .Liitie jina Lake “Yeyote atakaye liita jina la Kristo ,ataokoka”.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *