Swahili Service

MAAJABU YA REHEMA ZA MUNGU

UJUMBE: MAAJABU YA REHEMA ZA MUNGU

SOMO: WARUMI 9:9-18

MHUBIRI: REV. DR. WILLY MUTISO.

Rehema ya Mungu inahitajika na kila mtu kufaulu katika maisha. Rehema za Mungu si za kununua wala kurithiwa. Rehema za Mungu zinapeanwa na Mungu mwenyewe kulingana na mapenzi yake. Kuna mambo ambayo yanatuweka katika njia ya kupokea rehema ya Mungu.

Kwa kawaida maisha yetu yanao mambo mengi yanayofanyika vigumu kutabiri maisha. Wakati mwingi kuna mambo yatakaotokea kiasi si wenye nguvu wanaoishi sana, si wenye hekima na ufahamu wanaofaulu, lakini wanapokea rehema za Mungu. Hivyo wanaotarajia Mungu kuwaneemsha wanapata Baraka zake.

Safari ya ukuu inaweza kuwa ngumu bali na rehema za Mungu. Bila rehema za Mungu hatima yako itaingiliwa na watu wabaya na kusumbuliwa zaidi. Hivyo kinacho leta maana katika maisha ni rehema na neema ya Mungu.

Watu wa kadri moja na mali sawa wanakuwa tofauti katika ustawi wao kulingana na rehema waliopewa na Mungu. Hivyo rehema zake ni za maana sana kwetu.

Rehema za Mungu zinaelekea jinsi apendavyo yeye mwenyewe kulingana na mapenzi na rehema zake.

Rehema za Mungu hazitegemei umri, jinsia, kabila, utajiri, elimu au kuitimu na ujuzi. Rehema za Mungu hazidhibitiwi na mipango (protocols), sheria, mapokeo na ufahamu.

Rehema za Mungu zikifanya kazi, unaweza kuwa umekuja mwisho na utumikiwe kwanza, unaweza kugunduliwa na kuheshimika, hata ingawa kuna kukataliwa na kuzuiwa na watu.

Rehema za Mungu hazitegemei mahali ulipo, lakini Mungu anakupanga. Unaweza kuwa mahali popote duniani lakini rehema za Mungu zinajua mahali ulipo kukupatia kufaulu na kupenya. Hebu tuone:-

MAELEZO YA REHEMA ZA MUNGU.

  • Katika maisha kitu kimoja ambacho hakibadiliki ni rehema za Mungu.
  • Rehema za Mungu zinapozungumza kwa ajili yako, maisha yako hayataeleweka na watu.
  • Kunao njia tatu ambazo zinaeleza jinsi rehema za Mungu zinafanya kazi katika maisha ya mtu.
  1. Neema ya Mungu.
  • Rehema ya Mungu inapofanya kazi katika maisha ya mtu, neema ya Mungu itafurika katika maisha yake.
  • Mungu anaachilia uwepo wake na nguvu zake kiasi huyu mtu anafanya maajabu, anatekeleza mambo ya juu zaidi, mtu anapewa kupenya na ushindi mkuu ajabu.
  • Daudi alipata uwezo wa kuuwa dubu na simba baadaye. Daudi alimuua Goliathi aliyekuwa shujaa tangu ujana wake-1 Samweli 17:34-37.
  1. Kibali cha Mungu.
  • Rehema ya Mungu inapofanya kazi katika maisha ya mtu, kibali cha Mungu kinaonekana.
  • Kibali cha Mungu kinafungua njia na mlango wa kukubalika na watu na kusaidiwa-Zaburi 5:12.
  • Watu watakupea radhi kuu.
  • Esta alichaguliwa kuwa malkia mle Shushani kutoka kwa wanawali wengi. Alipata radhi mbele ya mkuu wake na mbele ya mfalme.
  • Kutoka kwa mikoa yote 127, rehema za Mungu zilimwangukia Esta-Esta 2:8-10, 16-17.
  • Esta alipojitokeza mbele ya mfalme bila kualikwa, mfalme hakumuua kulingana na sheria ya ufalme- Esta 5:1-4.
  1. Huruma za Mungu.
  • Rehema za Mungu ni mafuriko ya huruma za Mungu.
  • Rehema za Mungu zinafunga kila shida, dhiki na ajali zote kutokea.
  • Rehema za Mungu zinaleta huruma na msamaha wake na upendo wake-Yohana 3:16.
  • Mwanamke aliyeshikwa katika hali ya uasherati alipata rehema na radhi ya Yesu Kristo-Yohana 8:4-11.
  1. Wema na fadhili za Mungu.
  • Panapo rehema za Mungu, wema na fadhili zitaonekana-Kutoka 33:19, 34:6.
  • Wema wa Mungu ni pamoja na Baraka zake-Yakobo 1:17.

KIPIMO CHA REHEMA ZA MUNGU.

  • Kunao vipimo kadhaa vya rehema ya Mungu.
  1. Kupendwa zaidi juu ya wote.
  • Rehema za Mungu zinafanya mtu kupendwa zaidi juu ya watu wote, hata wale wako na maarifa zaidi kukuliko wewe.
  • Daudi alipendwa zaidi kuliko ndugu zake waliokuwa na maarifa zaidi kumliko Daudi walikataliwa.
  • Ndugu zake walikatazwa kuketi mpaka Daudi afike-1 Sam. 16:6-13.
  • Rehema ya Mungu inaponena juu ya maisha yako haijalishi ni nani unayeshindana naye.
  1. Mungu atakuunganisha na watu wakukusaidia kufika hatima yako (divine connections).
  • Naaman aliunganishwa na nabii aliyekuwa Israeli (Elisha) kupitia kijakazi (mtumwa) kutoka Israeli -1 Wafalme 5:1-5.
  • Watu watakujia kwa neema za Mungu, wapate kusadia hatima yako.
  1. Kutambulika katika umati.
  • Rehema za Mungu zitakutafuta na kukupata hata katika umati wa watu.
  • Kipofu batimayo, mwanamke mwenye kutokwa na damu, kiwete aliyeketi karibu na mlango wa hekalu, Zakayo juu ya mti.
  1. Kuvunja mipaka, taratibu, mipango, sheria na mapokeo.
  • Kwa rehema za Mungu, mipango ya shetani, laana za vizazi na kuzaliwa kunavunjwa kabisa na Baraka za Mungu kukufikia mara.
  • Bikira Mariamu alishika mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu-Alikubali mbele za mbingu.
  1. Kufungua na kufunga milango.
  • Mungu kwa uweza na nguvu zake anafungua milango na kuachilia Baraka zake.
  • Milango iliyofungwa na shetani, pepo na watu wabaya inafunguliwa kwa utukufu wa Mungu.
  • Milango ya uovu, mikasa na mauti inafungwa na rehema za Mungu-Ufunuo 3:7-8.
  • Mungu ameahidi kukutengenezea njia nyikani na jangwani, kukupa maji na vijito jangwani ni mweza yote.
  1. Rehema za Mungu zinakupatia ushindi dhidi ya adui zako.
  • Rehema za Mungu zinakulinda kutoka kwa adui wote na kukulinda na adui wote-Isaya 54:17.
  1. Rehema zinabadilisha mipango mbaya juu ya maisha yako kuwa Baraka kwako.
  • Kunao mafikira mabaya ya adui yako, njama juu yako, kunao watu wanaojifanya rafiki zako wanaokupangia maovu.
  • Mungu anageuza mipango hiyo yote kuwa Baraka juu ya maisha yako-Mwanzo 45:4-8.

MWELEKEO WA REHEMA ZA MUNGU.

  • Rehema haitegemei uwezo na mbinu zetu, bali neema ya Mungu-Waebrania 4:16.
  • Kuna njia ambazo Mungu atatumia kutuweka katika station za rehema zake.
  1. Wokovu unakufanya kuwa katika kituo cha rehema za Mungu-Yohana 1:11-12.
  • Anayekataa kuokoka anajiweka mbali na rehema za Mungu-Yohana 3:18.
  1. Utii wa neno na kuzifuata amri za Mungu-Nehemiah 1:5
  2. Kuwasamehe watu na kuwaonyesha rehema-Mathayo 5:7.
  3. Kuishi maisha safi-Zaburi 5:12.
  4. Kuomba na kulilia rehema za Mungu-Maombolezo 3:22-23, Marko 10:46-52.
  5. Kuishi katika unyenyekevu-Yakobo 4:6.
  6. Kuishi katika shukrani-Zaburi 100.

MWISHO

  • Karibia ukapokee rehema za Mungu-Waebrania 4:16.
  • Pengine bado hujaokoka-Leo ndiyo siku yako.
  • Pengine unaishi dhambini-Leo tubu dhambi.
  • Pengine hukujihesabia rehema za Mungu kwako, leo jihesabu katika rehema zake.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

3 thoughts on “MAAJABU YA REHEMA ZA MUNGU”

  1. Somo kako kuhusu rehema za Mungu lomenibariki sana. Mungu aendelee kukuongoza ili utumike zaidi.

  2. Asante kwa mafundisho ya rehema za MUNGU.WAEBRANIA 4:16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri ,ili tupewe rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *