Swahili Service

MACHOZI YA MWOKOZI JUU YA WALIOPOTEA

SOMO: LUKA 19:41-44

 

Leo ni Jumapili ya Mitende, yaani, “Palm Sunday.” Siku kama hii miaka 2,000 iliopita Mwokozi wetu Yesu Kristo aliingia mji wa Yerusalemu huku akijua anaenda kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu. Yesu Kristo ni yeye yule jana, leo na milele. Yesu Ndiye Mwokozi yule aliyelia siku hiyo kwa ajili ya waliopotea dhambi. Hivi leo Yesu Kristo angalia analia kwa ajili yetu na Miji ya dunia hii. Leo tunatizama Mambo matatu:-

  • Injili ndio ipasayo amani yako.
  • Kuna siku ya Neema kwako.
  • Yesu Kristo yuko tayari kuokoa wenye dhambi wote.

INJILI NDIO IPASAYO AMANI KWA MWANADAMU.

  • Biblia inasema “hakuna amani kwa mwenye dhambi.”

Injili ndio ipasayo amani ya dhamiri

  • Dhambi ndiyo chanzo hasa ya kila shida.
  • Shida ya ulimwengu huu ni moja tu mwanadamu.
  • Popote panapo shida ya taifa, ya ulimwengu, ya jamii, kanisa, kiwanda, shule utakuta mwanadamu.
  • Wewe huko na shida kwa sababu ya dhambi.
  • Injili ya Yesu pekee ndio inaondoa dhambi.
  • Mzigo wa dhambi unapotolewa, amani inapatikana.
  • Kwa sisi tuliomjia Yesu Kristo tumepata amani. Hata katika shida tunao amani.
  • Tulipopata Yesu Kristo kwa njia ya Neema, dhambi haina nguvu juu yetu tena.
  • Wanao mtizama Yesu Kristo wanapata kuishi. Tunapomtazama mwana kondoo achukuaye dhambi za ulimwengu tunapata amani moyoni.
  • Hakuna amani ya kweli nje ya Yesu Kristo.

Wakati wa dhiki Injili ya Yesu Kristo inaleta amani.

  • Katika siku zilizopita wengine wamekuwa wagonjwa, wengine wamefiwa, lakini amani ya Injili imetosha.
  • Wenye dhambi hawana amani wakati wa dhiki, hawana nanga katika dhoruba ya maisha yao.
  • Yesu Kristo ni amani tosha katika maisha yetu.

Injili inaleta amani wakati wa mauti.

  • Je, nani atakupa amani wakati wa kufa kwako?
  • Je, ndugu na dada zako? Je, ni marafiki?
  • Je, pombe na warembo watakupa amani wakati wa kufa?
  • Yesu Kristo alitangaza amani kwa walio karibu na walio mbali.
  • Mwenye dhambi–Yesu Kristo ndiye amani yako. Injili yake ndio ipasayo amani kwako.

KUNA SIKU YA NEEMA-(V.42)

“Laiti leo ungalijua hata wewe katika siku hii yapasayo amani, lakini sasa yamefichwa machoni pako.”

  • Siku ya kawaida inao Asubuhi yake, Adhuhuri yake, na jioni yake, na usiku wa manane yake.
  • Pia siku ya Neema inayo asubuhi, adhuhuri na jioni yake!!
  • Mji wa Yerusalemu ulikuwa na asubuhi yake wakati wa manabii waliwatangazia kuja kwa Mwokozi aliye Masihi.
  • Mji wa Yerusalemu ulikuwa na adhuhuri yake wakati Yesu Kristo aliwahubiri, “njooni kwangu ninyi nyote, mtu awaye yote akiona kiu na aje anywe maji ya uzima.”
  • Mji wa Yerusalemu ulikuwa na jioni yake wakati Yesu Kristo aliulilia mji. “Laiti leo unalijua hata wewe, katika siku hii yapasayo amani, lakini sasa yamefichwa machoni pako.”
  • Siku ya Neema ni ile siku Yesu Kristo anatolewa kwako.
  • Wengine wanaamini siku ya Neema inaanza kuzaliwa na kumalizika kifoni.
  • Lakini shida ni kwamba moyo wa mwanadamu unakuwa ngumu pamoja na uzee.
  • Ni ngumu sana wazee kuokoka!! Mioyo na udogo wa mioyo yao imekauka kwa kila siku ya kuishi.
  1. Wakati wa ujana ndio wakati bora na rahisi kuokoka.
  2. Wakati wa huduma ya injili-Yerusalemu walikuwa na wakati wa Injili–nabii, mitume na Yesu Kristo.
  3. Wakati Roho Mtakatifu amemiminiwa juu yao.
  • Kuna wakati wakijiliwa na Mungu.
  • Ni lazima kutambua majira ya kujiliwa kwako-( Vs. 44).

YESU KRISTO YU TAYARI KUOKOA WENYE DHAMBI WOTE.

  • Yesu Kristo anadhihirisha nia yake kuokoa kwa njia mbili.
  1. Machozi yake. 
  2. Maneno yake.
  • Machozi ya Yesu Kristo ni machozi ya kweli – “ kama ungalijua.” Aliwaona wakiwa katika dhambi zao.
  • Yesu Kristo aliwaona mikono yao ikiwa na damu yake.
  • Yesu aliona hukumu juu ya Yerusalemu, 70AD. Laiti kama ungalijua siku ya kifo chako!!
  • Maneno yake Yesu Kristo, yalikuwa ya upendo kwao, “laiti ungalijua”.

MWISHO.

  • Ndugu na dada zangu, tutafuta sana kuingia njia ile nyembamba.
  • Usithubutu kukaa katika dhambi tena leo ndiyo siku ya Neema.
  • “Laiti leo kama ungalijua yapasayo amani kwako.”
  • Kama bado okoka, leo, sasa ni wakati wako.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *