SOMO: YOHANA 20:11-18
- Mwanamke amekuwa na sababu nyingi za kulia tangu Adamu na Hawa walipoanguka dhambini katika shamba la Edeni.
- Yesu Kristo alikufa msalabani katikati ya wanawake walio kuwa wakilia.
- Yesu alipofufuka kutoka kwa wafu aliwakuta wanawake waliokuwa wakilia.
- Maneno ya kwanza ya Yesu Kristo alipofufuka kutoka kwa wafu yalikuwa ni kwa wanawake waliokuwa wanalia.
- Yeye aliyezaliwa na mwanamke alikuja kuyapanguza machozi ya wanawake.
- Hebu ona njia Yesu Kristo alitumia kumfariji Mariamu Magdalene.
- Kwanza Kristo alitaka Mariamu aeleze sababu yake kulia. “Mama unalilia nini?
- Kwa kawaida maombolezo ya na kwisha tunapojua sababu yake.
- Tunahitaji kuelewa sababu yetu kulia.
- Swali la pili la Mwokozi, lilieleza hasa sababu ya Mariamu Magdalene kulia – “je, wanatafuta nani?
- Wewe nawe wamtafuta nani? Kwanini unalia?
- Jibu la kulia kwako ni sababu unamtafuta?
- Mwanadamu ni mtafutaji, unapowatazama wanadamu unaona watu wanaotafuta, kutoka asubuhi mpaka jioni, mpaka asubuhi nyingine, mwanadamu anatafuta.
- Tunatafuta Amani, upendo, furaha, fadhili, utoshelevu wa maisha.
- Lakini huyu mwanamke alilia na kumtafuta Kristo aliyekuwa amekufa.
- Yesu Kristo alimuuliza, kwanini unamtafuta aliyehai katika waliokufa?
- Yesu Kristo hapatikani katika walio kufa.
- Yesu Kristo hapatikani katika wafu, kama Budha, Mohammed, Abrahamu, Daudi, Mzee Kenyatta, Mandela, Nkuruma, Washington, mother Mariamu, na mitume wa zamani.
- Yesu Kristo yuhai, amefufuka kwa wafu, amepaa mbinguni, atarudi tena, na kila jicho litamwona (Wafilipi 2:9-11).
- Mungu hawezi kuacha mwanadamu kutosheka na yasiokweli na yaliokufa.
- Hivyo Yesu Kristo ni jibu la kilio chako hivi leo.
- Kwanini unalia? Je, umeachwa na baba, mama, ndungu na dada zako? Je umewachwa na mpenzi , mume au mke wako?- Yesu Kristo ni jibu kwako.
- Hebu tuone sababu huyu mwanamke alilia:-
I. JE, ALILIA KWASABABU YA MAOMBOLEZO YA ASILI?
- Je, umefiwa? Bwana aliyefufuka kutoka kwa wafu anakufariji kwa maana:-
- Anakuakikishia kuwafufua waliokufa.
- Yeye yuko pamoja nawe, msaidizi aliyehai ni wako.
- Kristo amekuonea huruma, yeye aliyemwonea huruma Lazaro, akamfufua kwa wafu atakufufua wewe.
- Kristo alisema “msifadhaike mioyoni mwenu” (Yohana 14:1-6).
- Kristo ametupatia ahadi, tusifadhaike, ametutengenezea na kutuandalia mahali mbinguni. Atatupokea yeye mwenyewe, kunajia moja pekee kuingia mbinguni “Mimi njia, na kweli na uzima” (yohana 14:6).
- Je, wapendwa wako ni wagonjwa?
- Yesu Kristo aliyekuwa amekufa, amefufuka hili kukuponya, anasikia maombi yako sasa.
- Kwa mapigo yake msalabani tulipona (Isaya 53:4-5).
- Kristo anawaongojea kubariki hata wanaokufa
- Je, wewe mwenyewe ni mgonjwa?
- Kristo anaelewa na uchungu wako
- Kristo anayajua masikitiko yako
- Yesu Kristo atakupa afya ya mwili na roho
- Je, wewe ni maskini?
- Yesu Kristo ni tajiri aliyehai
- Yesu Kristo hatakuacha hau kukupungukia (Waebrania 13:5)
- Je, umehuzunika?
- Kristo alichukua huzuni zako zote
- Joo kwake kwa njia ya Imani, yupo karibu nawe sasa
II. JE, ALILIA KWA SABABU YA MAOMBELEZO YA KIROHO?
- Je, unalia kwa sababu ya ubinafsi wako? – aibika!
- Je, unalia kwa sababu ya kuasi Mungu – basi tubu dhambi zako kwake.
- Je, unalia kwa sababu ya kukosa tumaini? – mwamini Mungu, anaweza
- Je, unalia kwa sababu ya neema yake? – mshukuru Bwana.
- Je unalia kilio cha anaye mtafuta Bwana.
- Basi usilie kwa dhambi zako mbali tubu kwake
- Je, unalia kwa sababu ya dhambi na uovu wako? – Yeye atakusamehe dhami zako zote.
III. YESU KRISTO NA HUDUMA YA WANAWAKE
- Wanawake ndio walikuwa wa kwanza msalabani.
- Wanawake ndio walikuwa wa kwanza kaburini.
- Wanawake ndio walikuwa wa kwanza katika kufufuka kwa Yesu Kristo.
- Wanawake ndio walikuwa waijilisti wa kwanza.
- Wanawake ndio wa kwanza mbinguni
- Mwanamke moja mhindi alisikika akimwambia mmisheni moja kule india. “Biblia lazima iliandikwa na mwanamke: Kwanini? “kwa sababu Biblia inanena mengi mazuri juu ya wanawake, kitabu cha kihindu hakineni mema juu ya wanawake.”
- Kila mahali injili ya Kristo inatangazwa na kupokelewa, wanawake walipata uhuru wao.
- Yesu Kristo amewaweka wanawake jukwaa moja na wanaume.
- Kwa Yesu Kristo ua mbinguni hakuna mwanaume hau mwanamke, wote ni sawa mbele yake.
MWISHO
- Leo, Kristo amefufuka kwa wafu. Yuhai leo na milele.
- Kwa sababu Kristo yuhai anaweza kukuokoa kwa dhambi zako.
- Kwa sababu Kristo yuhai anaponya mwili, nafsi na roho.
- Leo ni siku ya kuokoka na kuponywa.
Ameni.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO. - September 21, 2025
- GOD GUIDES OUR DESTINIES. - September 21, 2025
- GOD OF THE BREAKTHROUGHS - September 10, 2025