MFULULIZO: MAISHA NA NYAKATI ZA ELISHA
SOMO: 2 WAFALME 4:38-41
Hakuna anayenufaisha shetani kama pasta wa uongo. Kama jinsi Yesu Kristo amekawia kurudi nabii wa uongo wameongezeka duniani.
Leo tunatazama mmoja wa wana wa manabii aliyewapa wana wa manabii sumu-Vs. 38-41. Hebu tuone:-
MTU WA MUNGU ALIYEIPA KANISA SUMU.
- Siku hizi za mwisho kunao wahubiri, walimu, manabii wa uongo, wanaoipa kanisa la Kristo sumu kwa mafundisho yao.
- Katika historia ya kanisa kumekuwako manabii na walimu wa uongo.
- Unapotazama Tv (runinga) Kenya imejaa nabii wengi wa uongo.
- Paulo alituonya-2 Timotheo 4:3-4.
- Utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima.
- Watu watafuata nia zao wenyewe.
- Watu watajipatia walimu makundi makundi.
- Masikio ya utafiti, watageukia hadithi za uongo.
MBELE YA MUNGU MHUBIRI NA MWENYE KUHUBIRIWA WANAWAJIBIKA.
- Mhubiri wa uongo amehukumiwa tayari-Mathayo 18:6.
- Kila mkristo lazima kujaribu kila roho-1 Yohana 4:1-3.
- Siku hizi wakenya wengi wameingia katika hadithi za uongo.
- Mauti imejaa katika sufuria nyingi hapa nchini.
- Jinsi Paul Makenzi amewadanganya watu kujiua, pasta, nabii amewalisha washirika wake nyasi kama jinsi ng’ombe!!
- Juzi, mwingine amewalazimisha washirika kumpa vitambulisho vyao, mishahara yao yote, passport zao!!
- Biblia inaeleza-2 Timotheo 2:17-18, manabii wa uongo wataongezeka, wanawafundisho kama mjinsi Hamenayo na Feleto.
- Hamenayo na Felito walikosa ile kweli, walisema kiyama imekwisha kuwepo (rapture).
- Hamenayo na Felito walipindua imani ya wengi.
- Lakini neno la Bwana linasimama kwa maana Mungu awajua walio wake, walio wake ni wale wameacha uovu.
- Nyumba ya Mungu ni nyumba kubwa.
- Kuna wale (useless, used. Users. Useful)-2nd Timotheo 2:20-26.
- Masihi wengi watatokea duniani-Mathayo 24:23-27.
- Mwenye kujipendekeza kwa watu-Luka 6:26.
- Manabii hujipendekeza na kupendwa na watu si haba!!
TABIA ZA NABII NA WALIMU WA UONGO.
- Yesu Kristo, Paulo, Petro, Yakobo, Yuda na Yohana walitutayarisha juu ya walimu wa uongo.
- Wanaingia kanisa bila kuonekana-Yuda 1:4.
- Wanaendeleza kazi zao kwa siri-2 Petro 2:1-3; Marko 13:22
- Wanafuatwa na wengi-2 Petro 2:1-3.
- Wanaleta sana mgawanyiko katika kanisa na vikwazo vingi-Warumi 16:17.
- Hawana Mungu ndani ya mioyo yao-2 Yohana 1:7-11.
- Manabii wa uongo, wengi wao walianza kwa mafundisho ya kweli-1st Timotheo 4:1-5.
- Maneno yao yanaonekana kama hekima-1st 6:20-21, Wakolosai 2:8.
- Wanaonekana kama mitume wa Kristo-2nd Wakorintho 11:13-15; Mathayo 7:15.
- Wanafundisha sana juu ya ustawi (prosperity) na utajiri (1st 6:5).
- Wanafundisha kwa uongo juu ya neema (hyper-grace)-Yuda 4.
-
- Wanageuza neema ya Mungu kuwa ufisadi-wanabadili neema kuwa lesensi au ufisadi na uasherati.
- Wanajiinua juu ya Mungu-Mathayo 16:24-25. Wanakanusha neno la Mungu-Mwanzo 3:1, wanakataa jehanamu imo-Mwanzo 5:29.
-
- Hivyo manabii na walimu wa uongo wanaingia kisiri, wahubiri uongo, ni hatari-Mathayo 23:15.
HEBU TUONE YALIOJIRI MLE GILGALI.
- Gilgali ndio mahali wana Israeli walifanya kambi ya kwanza tangu kuvuka Yordani-Yoshua 4:19.
- Gilgali ndipo Yoshua aliwatahiri wana Israeli-Yoshua 5:2-9.
- Gilgali ndipo Wagibeoni walimdanganya Yoshua-Yoshua 9.
- Gilgali ni mwanzo wa kuingia nchi ya ahadi, ndio mahali Eliya alianza safari yake ya mwisho.
- Gilgali ndio mauti iliingia katika sufuria!! Ndiyo wana wa nabii (100) walipata mikate 20 kutoka kwa mtu wa Baali-shalisha.
- Kulikuwa na njaa kuu sana-Vs. 38. Kumbukumbu 28:15-29; Amosi 8:11-njaa ya neno.
- Elisha aliamurisha sufuria kubwa-Vs. 38.
- Mwana wa nabii hakujua maboga sumu na yalio salama-Vs. 39.
- Wakristo wengi hawajui sumu na chakula salama.
- Nabii aliweka sumu kwa kutofafanua sumu na chakula salama.
- Leo, neno la Mungu linawekwa elimu, psychologia, hadithi, ufisadi.
- Chakula kilipokuwa tayari, kilinukia vizuri, kilipendeza macho-lakini mauti ilikuwa katika sufuria!!-Vs. 39-40.
- Ukombozi ulikuwa katika ile unga-Vs. 41.
- Unga ni neno la Mungu-Zaburi 119:9; 2 Timotheo 3:16; Zaburi 19:7.
MWISHO
- Walikula chakula kilicho takaswa!
- Walipata nguvu ya kuhubiri.
- Usikimbie kanisa unapofundishwa neno safi.
- Usijiunge na watu wanaoongea mazuri, wananukia vyema, wanaosikiza vyema-lakini jiunge na watu wanaoishi vyema.
- Ee Bwana, funga macho yangu kuona sumu iliyo katika sufuria yangu.
- Ee Bwana nifundishe kufafanua mema na mabaya.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- WHO IS SPEAKING TO YOU? - September 3, 2025
- CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO. - August 31, 2025
- THE GOD WHO BREAKS YOKES. - August 31, 2025