MFULULIZO : KURUDI KWA YESU KRISTO
SOMO : UFUNUO 20:1-15
Ufunuo mlango wa 20 unataja kipindi cha miaka 1,000 mara sita (6) Ufunuo 20:2-7. Kipindi hiki cha wakati ndicho kinaitwa ‘millenium.’ ‘Millenium’ni neno la Latin maanake 1,000 ya miaka. Kwa miaka hii 1,000 Yesu kristo mwenyewe atatawala dunia hii-utawala wa Yesu Kristo utaleta wakati na enzi ya amani, ustawi na haki jinsi dunia haijaweza kuona tangu mwanadamu alivyofanya dhambi bustani Edeni.
Mpaka sasa tumeona na kujifundisha juu ya-
- Kunyakuliwa (rapture).
- Dhiki kuu.
- Kiti cha hukumu cha Kristo (BEMA).
- Harusi ya Mwana kondoo
- Kurudi kwa Yesu Kristo duniani.
Leo tunatazama miaka 1,000 ya utawala wa Kristo duniani, yaani millenium.
MWOKOZI YESU KRISTO WAKATI WA MILLENIUM-Ufunuo 20:4-6.
- Je, Yesu Kristo atakuwa anafanya nini wakati huu?
- Atakuwa anaongoza.
- Sasa Kristo ataongoza na kumiliki kiti cha enzi cha baba yake Daudi-Isaya 9:6-7.
- Kristo ataongoza dunia kwa nguvu, haki na utukufu.
- Utawala wake utaleta amani, ustawi na fanaka zaidi. Utawala wake utakuwa pamoja na kuleta haki, utakatifu na utukufu.
- Viongozi wa ulimwengu huu wameahidi mambo mengi lakini kwa sababu wao wametawaliwa na ubinafsi, ufisadi, ukabila na chuki.
- Lakini utawala wa Yesu Kristo utakuwa wa furaha, amani, upendo, utakatifu, haki na ukamilifu.
- Yesu Kristo atatawala.
- Kristo atatawala na fimbo ya chuma-Ufunuo 19:15.
- Atatawala jamii yote ya dunia hii.
- Wasiomtii Kristo watakabidhiwa kwa haraka sana.
- Uasi hautakubalika katika ufalme wa Kristo.
- Yesu Kristo atapokea utukufu.
- Watu wa kila kabila, jamii na taifa watasujudu na kumwabudu Kristo pekee-Isaya 40:5.
- Utakuwa wakati wa Yesu Kristo kupokea utukufu na sifa.
SHETANI WAKATI WA MILLENIUM-Ufunuo 20:1-3, 7-10.
- Shetani atakuwa jela-Vs. 1-3.
- Kwa miaka 1,000 shetani na pepo zake hawatazuia kazi ya Mungu!!
- Hakutakuwa na majaribu ya shetani.
- Leo hii shetani ndiye mfalme wa dunia hii-2 Wakorintho 4:4.
- Kazi ya shetani ni kupinga mpango wa Mungu duniani.
- Ona majina anayopewa Vs. 2, joka, yule nyoka wa zamani, ibilisi, shetani.
- Siku hio na wakati huo shetani hatakuwako duniani.
- Hebu fikiri dunia bila shetani, Kristo akitawala bila shetani-Utukufu-Haleluya!
- Shetani atahukumiwa-Vs. 7-10.
- Hapo Biblia inaeleza kwamba baada ya ile miaka 1,000, shetani atatolewa jela na kurudi tena duniani.
- Shetani atakusanya jeshi kubwa zaidi.
- Shetani na jeshi lake watauvamia mji wa Mungu (Yerusalemu) mahali Kristo anatawala. Hapa shetani anataka kuipindua serikali ya Kristo!!
- Hukumu itashuka kutoka mbinguni, moto, wote waliomfuata shetani na jeshi lake watauliwa wote.
- Shetani atatupwa katika ziwa la moto na kiberiti-milele na hata milele.
- Tunashangaa sana!! Hata Kristo akitawala kwa haki, upendo, utakatifu, mwanadamu atachagua kwenda na shetani.
- Haijalishi-moyo wa mwanadamu ni dhaifu na mdanganyifu. Haijalishi upendo wa Mungu juu ya mwanadamu-mwanadamu anahitaji wokovu-kwa neema.
- Mungu amejaribu kumpenda na kuokoa mwanadamu lakini mwanadamu ameasi!!
- Ona vizazi na nyakati (dispensations).
- Nyakati za bila lawama (age of innocence)-Mwanzo 3. Matokeo –uasi.
- Nyakati za dhamiri (age of conscience)-Mwanzo 5-6. Matokeo-ufisadi duniani kote.
- Nyakati za mwanadamu kujitawala (human government/self determination)-Mwanzo 11. Matokeo-ibada ya shetani-Babeli.
- Wakati wa ahadi (age of promise)-Mwanzo 12; Kutoka 1. Matokeo-utumwa wa Misri.
- Nyakati za sheria ( the age of law)-Kutoka 2; Mathayo 27. Matokeo-Mwanadamu alimuua muumba wake-msalabani.
- Nyakati za kanisa (the age of the church). Matendo 1. Matokeo-maasi duniani kote-kanisa litaasi Mungu duniani kote (worldwide apostasy).
- Nyakati za dhiki kuu (the great tribulation)-Ufunuo 19. Matokeo-vita vya armageddon.
- Nyakati za millenuim (miaka 1,000)-Ufunuo 20. Matokeo-mwanadamu na shetani watajaribu kupindua serekali ya Kristo.
- Moyo na nia ya mwanadamu ni kuasi. Hakuna chema katika mwanadamu-Warumi 3:10-11.
- Tumaini pekee ya mwanadamu ni kumjia Kristo na kuokoka.
- Yesu Kristo anabadilisha maisha na mwelekeo.
- Je, leo unasimama wapi-je, umeokoka?
WATAKATIFU WAKATI WA MILLENIUM-Vs. 4-6.
- Je, watakatifu watakuwa wakifanya nini wakati wa millenium?
- Watatawala pamoja na Kristo-Vs. 4.
- Tutatawala pamoja na Yesu Kristo-2 Tim. 2:12-13; 1 Peter 5:1.
- Watafufuliwa-Vs. 4.
- Katika mwanzo wa millenium watakatifu wote tangu Agano la Kale na wote waliokufa wakiwa katika Yesu Kristo katika dhiki kuu watafufuliwa miili yao.
- Hebu fikiri watakatifu wa Agano la Kale waliokufa katika imani, walitazamia siku hii-Yohana 8:56.
- Watapokelewa-Vs. 4.
- Wale watakataa chapa ya mpinga Kristo, Wayahudi na Wayunani katika ufalme wa Mungu-Mathayo 25:31-46.
- Imani ndani ya Yesu Kristo pekee ndio njia pekee ya kuingia mbinguni. (Imani pekee, kwa neema pekee, katika Yesu Kristo pekee, kwa utukufu wake pekee).
- Wokovu ni katika Yesu Kristo pekee.
WENYE DHAMBI WAKATI WA MILLENIUM.
- Je, kutakuwa na wenye dhambi wakati wa millenium? Ndiyo.
- Kutakuwa na wale watazaliwa wakati wa millenium (1,000 miaka).
- Unaona kwamba kuna Wayahudi na Wayunanai watakao ingia katika millenium kutoka kwa dhiki kuu, wakiwa katika miili yao (mwili na damu).
- Hawa watu wameokoka lakini watoto watakao wazaa watazaliwa katika mwili hivyo wanazaliwa wenye dhambi, wamepotea wanao asili ya dhambi-wanahitaji kuokoka!!
- Uhusiano wao na Mwokozi.
- Kwa sababu shetani yuko jela, mwenye dhambi atakuwa kama mwokovu!!
- Lakini bado anahitaji kuokoka.
- Watalazimishwa kuabudu sahihi.
- Kila mtu lazima atapiga magoti mbele ya Yesu Kristo.
- Kila mmoja atakiri Yesu Kristo ni Bwana-lakini bila kumpenda Kristo ni bure!!
- Kutoka nje hakutakuwa na tofauti lakini kutoka ndani ya mioyo kutakuwa tofauti sana.
- Watalazimishwa kutembea sahihi.
- Kutakuwa na kutii hata bila kumpenda Yesu Kristo kwa mioyo dhati.
- Wakati shetani atafunguliwa kwa muda mfupi-hawa watu watadanganywa na shetani-Warumi 2:4.
- Watapata fursa ya kumchagua Yesu Kristo kama Mwokozi wao au kumkataa-Yohana 14:6.
UMMA WAKATI WA MILLENIUM (Society)
- Wakati wa millenium (miaka 1,000) kutakuwa na mabadiliko mengi.
- Amani-hakuna vita popote duniani!!
- Maendeleo tele.
- Utakuwa wakati wa maendeleo na amani na binafsi-na dunia yote-Isaya 2:4; 9:4-7: 32:17-18; 33:5-6; 60:18.
- Furaha-furaha ya milele-Isaya 12:3-6; 14:7-8.
- Utakatifu-ufalme wa Mungu ni mtakatifu-Isaya 31:6-7; 35:8-9; Eze. 36:24-31.
- Utukufu-ufalme wa Mungu utakuwa dhahiri-Isaya 4:2; 35:2; 40:5; 60:1-9.
- Faraja-Kristo atashughulikia kila hitaji-Isa. 12:1-2.
- Haki-Haki kwa kila mtu itatendeka-Isa. 9:7; 32:16; 42:1-4; 65:21-23.
- Ufahamu kamili-hakutakuwa na tashwishwi-Isaya 11:1-2; 41:19-20; 54:13; Hababuki 2:14.
- Hakuna laana tena-laana zote zitatolewa-Isaya 11:6-9; 65:25.
- Hakuna magonjwa-hakuna kifo-Isaya 33:24; Yeremia 30:17; 33:6.
- Hakuna ulemavu wowote-Isaya 29:17-19.
- Ulinzi utakuwa wakutosha, hakuna utoto na ujinga.
- Utauwa na ufanisi utaleta wingi wa kila kitu chema-Isaya 35:1-2; 30:23-25; Yeremia 31:5; Yoeli 2:21-27; Amosi 9:13-14.
- Lakini bado tutangojea hali yetu ya mwisho (final state) mbinguni milele na milele.
MWISHO
- Leo, unapompokea Yesu Kristo, utawala wake ndani yako unaanza.
- Je, kuna wakati ulimpokea Kristo kabisa ndani ya maisha yako?
- Sasa ni wakati wako-Haleluya-Amina.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
