Swahili Service

MIAKA ELFU YA UTAWALA WA YESU KRISTO DUNIANI

MFULULIZO:  KURUDI KWA YESU KRISTO

SOMO:   UFUNUO 20:1-6

Wanadamu wameota ndoto na kutarajia wakati mwema zaidi hapa duniani. Plato katika jamhuri yake alitazamia wakati kila kitu kilichopindana kitafanywa laini. Bacon alitarajia sana Atlantis patakuwa mahali pa Amani na ustawi. Marais wengi wameahidi wanainchi wao wakati wa enzi ya Amani na ustawi. Huko America walikuwa na “the new deal,” new frontier,” the great society,” new world order.” wengine walisema “I have a dream”. Viongozi wa kwanza wa Africa na waajilishi wa mataifa ya Africa walikuwa na ndoto za kumaliza umaskini, ugonjwa, ujinga na utawala mbaya, baada ya miaka 60 Africa tungali na shida si haba.

Lakini wakati wa “dhahabu” yaani “golden age” haitaletwa na mwanadamu na mipango yake na ratiba zake. Amani na usitawi havitaletwa na mwanadamu kwa sheria na bunge hau seneti, haitaletwa na mikataba ya Amerika, Ulaya, Waarabu hau China. Amani ya kweli, uchumi na ustawi wa kweli utaletwa duniani ni Yesu Kristo na tawala wake hapa duniani. Yesu Kristo atakapo tawala hapa duniani ndio dunia itakuwa paradiso ya ukweli. Hivi leo tutajifunza jinsi dunia hii itakavyo kuwa chini ya utawala wa Yesu Kristo na wateule wake.

Hebu tuone:-

I.  AHADI YA MILLENIA (1000MIAKA)

  • Ahadi ya utawala wa Yesu Kristo duniani kwa miaka elfu (1000yrs) imejengwa juu ya Agano.
  • Kuna Agano mbalimbali katika Biblia.
  • Kuna Agano ambazo Mungu alifanya na mtu, watu, jamii, hau taifa.
  • Mungu alifanya Agano na Ibrahimu, jamii ya Yakobo, taifa ya Israeli, Kanisa (nka).
  • Kuna haina mbili za Agano.
  1. AGANO ZILIZO NA MARSHARTI – katika Agano za marsharti Mungu anatoa marsharti ambayo ni lazima kutimizwa hili ahadi itimie.
  • Katika II Mambo ya Nyakati 7:14 “ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu watajinyenyekesha na kuomba na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni, na    kuwasamehe dhambi zao na kuiponya nchi yao.’
  1. ANGANO MBILA MARSHARTI – kunazo Ahadi na Agano ambazo Mungu ameahadi lakini mbila marshati kwetu kama wanadamu.
  • Katika (II Samueli 7:12) “Nawe siku zako zitakapotimia ukalala na baba zao, nitainua mzao wako nyumba yako, atakayetoka viunoni mwako, nami nitaufanya imara ufamle wake.”
  • Agano hii itatimia Yesu Kristo atakapoketi juu ya kiti cha enzi ya Baba yake Daudi katika milleniamu.
  • Kwa maana Yesu Kristo ni wa uzao na kizazi cha ufalme wa Daudi (Mathayo 1:1, Luka 1:31-32)
  • Agano na ahaadi nyingine isiyo na marsharti inapatikana katika (Danieli 2:31-34)
  • Enzi za dunia hii katika wakati huu wa mataifa zimefuatana mpaka leo, wakati wa mataifa ya udongo na chuma yaani “umoja wa matiafa” (united nations).
  • Danieli na Nebukadreza waliona nyakati za mataifa mpaka wakati “nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hari.”
  • Jiwe hili ni ufamle wa Yesu Kristo na ndio umebaki.
  • Yesu Kristo ndiye jiwe hilo (Mwanzo 49:24, Zaburi 118:22, Isaya 28:16, I Wakorintho 10:4)
  • Yesu Kristo atavunja kabisa kazi zote za giza katika vita vya Armageddon.
  • Yesu Kristo atakomesha kila adui katika vita vya Armageddon, kila pepo na mamlaka ya giza hii, hii ndio ahadi ya milleniamu.

II.  WAKATI WA MILLENIUMU

  • Je, milleniamu ni miaka migapi? Neno mili ni elfu (mili-1000) “anum-maanake ni ‘mwaka.’
  • Hivyo ‘mili’ na ‘anum’ millinum. Yaani miaka 1000.
  • Basi kunamafundisho haina tatu juu ya wakati wa kunyakuliwa (rapture)
  1. POST MILLENNIAL VIEW – “baada ya miaka elfu”
  • Hawa wanaamini kwamba Yesu Kristo atarudi tena baada ya miaka 1000 ya Amani na ufanisi mkuu duniani.
  • Wanafunzi kwamba dunia hii inaendelea kuwa nzuri zaidi.
  • Lakini unapoangalia, dunia hii inaendelea kuwa mbaya kila kuchao, umaskini zaidi, magojwa zaidi, ujinga zaidi utawala mbaya zaidi, uchumi mbaya zaidi.
  • Is the world becoming better or worse?
  1. A-MILLENIAL VIEW – (HAKUNA MILENIUMU ITAKAYO KUWA)
  • “A” – maanake ni “hakuna”, hivyo A-milliniumu ni kusema hakuna miaka elfu.
  • Wasomi wengine wa biblia wanasema hili miaka elfu ni mseto tu.
  • A-miliniumu inaenda kinyume na (Luka 1:31-32)
  • Luka mtakatifu anasema Yesu Kristo atakuja . Atakuwa mwana wa aliyejuu, atakuwa mkuu. Ataketi katika enzi na ufalme wa Baba na Daudi.
  1. PRE-MILLENNIAL VIEW (YESU ATARUDI NA KUTAWALA MIAKA ELFU NA MILELE)
  • Biblia inatufundisha kwamba Kristo atalinyakua kanisa lake, kutakuwa na wakati wa dhiki kuu duniani kwa miaka saba (7).
  • Kutakuwa na kiti cha hukumu za Kristo mbinguni (miaka 7)
  • Baada ya dhiki kuu Yesu Kristo atarudi pamoja na watakatifu wake kutawala hapa duniani kwa miaka elfu.
  • Baada ya miaka elfu kutakuwa na kiti kikubwa cheupe cha hukumu, shetani na wale wasiomwamini Kristo watatupwa katika ziwa la moto milele.
  • Kristo atarudisha funguo kwa baba Mungu hili Mungu Baba awe yote ndani yayote milele na hata milele.

III. USITAWI WA MILINIAMU

  • Shetani atafungwa (Ufunuo 20:1-2) miaka elfu moja, atafunguliwa kwa muda mfupi, baadaye ataukumiwa katika ziwa la moto milele na milele.
  • Shetani anapokamatwa na kufungwa miaka elfu – duniani hakutakuwa na uasi, uongo.
  • Kwa sasa shetani yuko duniani na tena yuko na uhuru mwingi, dhambi za kila haina ziko duniani kwa sababu ya shetani.
  • Shetani atakapofungwa, hamna dhambi, bali Amani na usitawi (Isaya 2:3-4, Mika 4:4)
  • Shetani atakapofungwa dunia hii itarudishwa kwa rotuba yake, hakutakuwa na shida ya mazingira na hali ya hewa (Warumi 8:19-21)
  • Viumbe vyote vinamgojea Yesu Kristo arudi duniani.
  • Wanyama wote wanamgoja mwokozi Yesu Kristo kurudi (Isaya 11:6-9)

IV.  WATU WA MILLENIAMU

  • Kutakuwa na watu haina mbili katika miliniamu
  1. Wenye kutawala
  • Hawa ni pamoja na watakatifu wa Agano la kale, wakristo walionyakuliwa, wakristo waliokufa katika dhiki kuu na wote waliomkataa mpinga   Kristo.
  1. Waliosalia duniani huwa ni watu hawakufa kupitia dhiki kuu, huenda hawajaokoka lakini wamepona maradhi, machunu, dhiki na majaribu waliopitia.
  • Hawa watakuwa katika hali ya wokovu kwa maana shetani hayumo duniani.
  • Hawa watu tutawatawala na fimbo ya chuma chini ya Yesu Kristo .
  • Mara ya kwanza Kristo alipanda punda, sasa amepanda farasi mweupe!
  • Pale kale Kristo alisimama mbele ya Pilato, sasa Pilato atasimama mbele ya Kristo!
  • Pale mwanzo Yesu alikataliwa sasa kila ulimi unakiri Yesu Kristo ni Bwana.
  • Pale mwanzo Yesu Kristo alivaa taji ya miiba sasa amevaa taji ya utukufu.
  • Kristo atatawala kwa nguvu na enzi yake haina mchezo. Yeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme.

MWISHO

  • Je, utumishi wako sasa, kwa Kristo uko je?
  • Cheo chako katika utawala wa Kristo kinatengemea jinsi unavyotumika sasa.
  • Je, umeokoka? Kama bado leo jiadhari ukaokoke
  • Je wewe huko tayari kumlaki Kristo ajapo?
  • Fanya hima kuokoka, kujitakasa na kumfanyia Yesu Kristo kazi yake. Ameni.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *