MFULULIZO: UPENDO WA MUNGU NI WA MILELE
SOMO: MALAKI 1:6-14
Mungu apendezwi na vitu ovyo ovyo. Kama ni ibada na sifa afadhali hasipokee ibada kuliko ovyo. Mpe Mungu yaliyo mema kabisa (give God Your best). Siku moja jumapili kijana wa miaka 6 alisikiza mchungaji akiubiri ujumbe mrefu, kijana akachoka sana. Kijana akamuliza baba yake ‘Je, huyu mhubiri anafanya kazi gani katikati ya juma?’ baba akamwambia kijana, “huyu mhubiri huwa na kazi nyingi, anafanya kazi ya office, anawatembelea wangojwa, anatengeza ujumbe wa kuhubiri jumapili, anafanya ushauri wakristo, halafu anapumzika, kwa maana kuhubiri ni kazi zito sana.” kijana akafikiri sana baadaye akasema “kusikiliza mhubiri si rahisi pia!!” kusikiliza si rahisi, zaidi ukiwa haupendi kusikia. Malaki 1:6-14, iliandikiwa wachungaji wa kulipwa kama mimi.
Wana wa Israeli walikuwa wamerudi kutoka babeli kwa uamisho wa miaka 70. Hekalu tayari ilikuwa imejengwa upya na ibada kuazishwa upya. Lakini hata ingawa kutoka nje mambo yalionekana shwari, pale ndani uzembe wa kiroho ulikuwa umeanza kutawala watu kama jinsi saratani (cancer). Katika hali hiyo Malaki alitokea na changamoto kwao na sisi pia, kumpa Mungu yaliyo mema zaidi (giving God the best).
Mungu anataka sisi kujua kitu moja “Mungu anatupenda”. Mungu anatupenda na upendo mkuu, upendo usio na kifani. Lakini kama jinsi watu wa wakati wa Malaki miaka 2400 iliyopita, walichukia sana upendo wa Mungu kwao. Pengine wewe pia ni moja wao.
Kwasababu ya kuchukia Mungu, ibada yao ililegea, viongozi wao walikuwa wazembe, ndoa zao ziliaribika na kuvunjika. Sadaka na zaka zao, zilikuwa hoi hoi, walikataa kutumika. Kama tutaendelea mbele katika ratiba ya kiroho ya Mungu, Mungu anasubiri tumpe yaliyo bora zaidi. Kuna njia tatu za kumpa Mungu yaliyo bora zaidi:-
I. UWE NA IMANI TIMILIFU (1:6-7) (Embrace an authentic faith)
- Upendo wa Mungu ni pande mbili ,kwanza upendo wake ni kubembeleza ( tender) pande ya pili ,upendo wake ni mkali.Upendo wa Mungu ni uhusiano(relational)lakini pia Mungu lazima apewe heshima na utukufu wote. “Mwana umheshimu baba yake,na mtumishi umheshimu bwana wake.v6”
- Tunaitaji usalama wake kama mtoto ,lakini pia lazima tumpe Mungu heshima kwa ukuu wake.
- Mungu ni Baba wa Israeli (kutoka 4:22) na (kutoka 20:12)”Mheshimu Baba na Mama yako”.
- Makuhani hawakuwa na heshima kwa Mungu wao.
- Mungu anastahili heshima na utukufu maana yeye ni Mungu Mkuu (Yahweh).
- Huyu Mungu Mkuu habandiliki,Ni wa milele .
- Anastahili heshima zote (v.8- 14).
- Tusimzoee Mungu kiasi tukose heshima na utukufu.
- Kaini alitoa dhabihu ya mazoea kwa Mungu (Mwanzo 4).
- Kaini sadaka yake ilikataliwa kwa maana alitoa kwa dharau (attitude) (1 Yohana 3:12,Waebrania 11:4).
- Mungu anamtazama mwenye kutoa na pia matoleo yake,akitafuta(Imani timilifu).
- Mke akimdharau mume ,hau mume kumdharau mke wake, baraka za mume,hau mke hatapata (II sam 6:16-23).
II. MPE NAFASI YA KWANZA KWA MALI NA VITU VYAKO(1:8-9) (Give God priority over possessions)
- Wana wa Israeli pamoja na makuhani walikuwa na shida –walileta sadaka mbovu mbele za Bwana (v-8)
- Mungu tayari alikuwa amewajulisha kwamba hapendezwi na sadaka isiyostahili (Walawi 22:2,19-20).
- Mungu anataka nafasi ya kwanza kwa mali na juu ya vitu vyako vyote.Hawa watu walikuwa wakija kanisani kama kawaida lakini mioyo yao ilikuwa mbali na Mungu wao.
- Uhusiano wako na Mungu unapimwa na jinsi sadaka na zaka na utumishi wako ulivyo.
- Mungu aliwaambia wao wajaribu kutoa sadaka hizo kwa magavana wao.
- Wengi walikuwa na kazi zao, na kodi za kulipa – hivyo waliona kwamba Mungu atawaelewa.
- Kulikuwa na daraja tatu (3) standards za sadaka katika Biblia
- Toa kilichochema kabisa – (give the best) (Johana 12)
- Mpe hau mtolee Mungu kwanza (give to God first) (II Mambo ya Nyakati 31:5, Marko 12:41-44)
- Kumtolea Mungu lazima kuwe na gharama zake- (Giving should cost you something)Kitoa ni lazima kukugarimu kitu (II Sam 24. 24:
III. FAHAMU NA TAFAKARI UKUU WA MUNGU (1:10-14) (OF GOD) (Grasp the greatness of God)
- Mungu hapendelei mabaki (leftovers) afadhali kufunga kanisa, Mungu apendezwa na mambaki (V.11,14)
- Kutoa kunaenda sambamba n ukuu wa Mungu (Mika 6:3) (Isaya 1:12-13)
- Mungu hapendi kudanganywa (Mhubiri 5:5)
- Mungu anasema jina lake litakuwa kuu duniani, kama tupende na tusipende.
- Hivyo yafuatayo ni ishara za kochoka katika kanisa na ibada.
- Kutokuwa tayari – inadequate preparation for worship
- Kujitoa shingo upande – half hearted participation, mazoea katika ibada.
- Kutoelewa na maana ya ibada – improper motivation
MWISHO
- Tukijua ukuu wa Mungu na yale Yesu alitutendea, hatutacheza kanisa tena – tutampa Mungu kilichochema zaidi – Amina.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
