Swahili Service

MTU ALIYEUZA MAISHA YAKE

MFULULIZO: WASHINDWA WAKUU KATIKA BIBLIA

SOMO: WAEBRANIA 12:14-17

 

 

Biblia inatueleza kwamba palikuwa na mtu kwa jina lake Esau aliyeuza urithi wa uzaliwa wa kwanza. Esau alimwacha Mungu wa baba zake, alikosa imani timilifu. Esau badala ya kumtumikia Mungu wa baba zake aliamua kuwa mtu bila Mungu (secular-godless).

Waebrania anatueleza kwamba uamuzi wa Esau haukuwa busara. Kwa kumkataa Mungu Esau alileta shida nyingi katika maisha yake.

“Asiwepo kwenu mwasherati wala asiye mcha Mungu kama Esau aliyeuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja. Maana mwajua ya kuwa hata alipotaka baadaye kurithi baraka, alikataliwa maana hakuona nafasi ya kutubu, ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi”- Waebrania 12:16-17. Hebu tuone:-

  1. ESAU ALIKUWA BILA MUNGU
  • Kwa sababu Esau alichagua kuishi bila Mungu ndani ya maisha yake, yeye alijipatia shida kuu katika maisha yake na yale ya vizazi vyake baadaye.
  • Hata ingawa Esau alijuta sana, nafasi ya kutubu haikuweko tena.
  • Mpaka wa leo Wayahudi wanapo taja wakuu wa baba zao, wanataja Ibrahimu, Isaka na Yakobo.
  • Esau alikuwa ndugu mkubwa wa Yakobo kwa nyumba ya Isaka.
  • Biblia inatueleza kuwa ndugu hawa wawili walipoendelea kukua, Esau alikuwa mwindaji mkuu, mtu wa nchi ya nyika lakini Yakobo alikuwa mtu wa nyumbani karibu na mamaye Rabeka- Mwanzo 25:27.
  • Esau alikuwa- mwanaume, kifua chake kilijaa nywele, mwanaume wa hakika.
  • Yakobo naye alikuwa mtu wa nyumbani, “mtoto wa mama” mwanaume- mke.
  • Yakobo alikuwa jeuri kiasi kuliko ndugu yake.
  • Kile chakula alichompa Esau kilikuwa ni chakula cha ziada tu (snack)- Mwanzo 25:29-34.
  • Kwa sababu ya kupuuza u-milele wake, Esau aliuza urithi kwa kupewa chakula chepesi tu.
  • Esau ni watu wanaopuuza urithi, uzima wa milele, Mungu, Mbinguni, kwa furaha na manufaa ya muda mfupi. “Maana ya urithi wa mzaliwa wa kwanza ni nini?” Esau aliuliza.
  • Esau alipuuza ule urithi. Leo hii tungekuwa tunasema, “Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Esau.” Esau alimwacha Mungu siku hio.
  • Mzaliwa wa kwanza alirithi baba yake, alikuwa mwakilishi wa nyumba ya babaye, alipata mara dufu ya mali ya babaye, alibeba jina na sifa za nyumba na ukoo wa babaye- Esau alikana zote!! Kwa kupata chakula cha siku moja.
  • Waebrania inasema Esau aliuza urithi wake kwa bei ya uji kwa sababu Esau alikuwa mtu bila Mungu (godless).
  • Kwa kumkataa Mungu katika maisha na shughuli zake, Esau alifanya uamuzi mbaya.
  • Esau alikuwa bila Mungu, bila uungu. Hii si kusema Esau alikuwa muuaji, mwizi, jeuri.
  • Esau alipendwa na baba yake sana, Esau alimjali baba yake. Yakobo alipotoroka nyumba kwa miaka 20, Esau alitumikia wazazi wake.
  • Esau hakuwa mlafi, alipopewa mali na ndugu yake Yakobo, Esau alisema tayari amebarikiwa kutosha- Mwanzo 33:9.
  • Esau alimsamehe ndugu yake Yakobo.
  • Esau na Yakobo walimzika Isaka pamoja kwa heshima zote, hivyo Esau hakuwa mtu mbaya, lakini shida ya Esau ni kuishi bila Mungu (godless).
  • Ibrahimu alijenga madhabahu kwa Mungu wake, Isaka alijenga madhabahu kwa Mungu wake, Yakobo alijenga madhabahu kwa Mungu lakini Esau hakuwa mtu wa ibada, alimwasi Mungu wake.
  • Esau aliishi bila ibada, bila dhabihu, bila kanisa, bila maombi, bila kukesha, bila kutafuta uso wa Mungu, bila kutafuta mapenzi ya Mungu kwa maisha yake!!

JE, SHIDA YA KUISHI BILA MUNGU NI NINI?

  • Manufaa ya kuishi bila Mungu ni;-
  1. Siku moja zaidi.
  2. Pesa zaidi.

Ya kufanya shughuli zako kwa maana hakuna kutoa sadaka na fungu.

Hakuna kuishi maisha safi na hakuna watu wa kusema wewe ni mwenye dhambi.

  • Uhuru wa kuishi upendavyo, kama hakuna Mungu, basi mtu ataishi apendavyo.

Mtu bila Mungu hajali juu ya hukumu ya milele.

  • Lakini shida za kuishi bila Mungu ni nyingi zaidi.
  • Uamuzi bovu- alipofika wakati wa kuoa Esau alifanya uamuzi ulioleta shida kwa wazazi wake- Isaka na Rabeka- Mwanzo 26:34-35.
  • Esau hakujali atakayeoa. Ndoa mbaya, maisha mabaya!!
  • Esau alifunganishwa nira moja na watu wasio na Mungu- 2 Wakorintho 6:14-15.
  • Kuchagua mke au mme ni jambo kubwa si kama jinsi kununua gari!! Vijana wananunua gari kwa sura yake, hawajali engine, mafuta, spares na udhabiti.
  • Kwa sababu ya chakula kimoja tu, Esau alipoteza urithi wa milele kwa kuwa Esau hakuwa na Mungu.
  • Esau aliishi bila mchungaji wa maisha- Zaburi 23.
  • Esau aliishi bila tumaini ya milele, uzima wa milele, Agano la milele- Waefeso 2:12.

MAISHA BILA MUNGU NI BURE- Mhubiri 12:1-14.

Maisha bila Yesu ni ubatili mtupu.

  • Esau aliuliwa na Dani mwanaye Yakobo kwa kupinga mazishi ya Yakobo huko Machpelah (Talmud).
  • Esau- Edomu (mwekundu) hakumpendeza Mungu- Malaki 1:2-3; Warumi 9:10-13.
  • Esau alikuwa na wake watatu. Wa mwisho alikuwa kaka yake Basmat Binti ya Ishmaeli.
  • Warumi ni wazaliwa wa Esau, ndio ufalme wa Rumi unaitwa ufalme wa Edomu (Talmud).
  • Somo kutoka kwa maisha ya Esau.
  • Lazima kutunza sana nyakati tamaa za mwili.
  • Nyakati za udhaifu ni wakati wa majaribu wakati huo tunaangalia mambo na utoshelevu wa saa hio hio bila kutazama mambo ya milele.
  • Lazima kujua majukumu yetu, tusiuze hatima yetu kwa sababu ya furaha ya kitambo kidogo tu.

MWISHO

  • Esau ni mmoja wa washindwa katika Biblia.
  • Esau aliishi maisha yake bila Mungu, bila ibada, bila madhabahu.
  • Kuna wakati mtu hawezi kutubu dhambi zake- Esau alilia sana, machozi yake mengi hayakubadilisha chochote.
  • Mungu alichukia Esau kwa sababu alidharau wokovu, neema na mambo ya milele na ahadi za Mungu kwake.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *