Swahili Service

MTU AMETUMWA KUTOKA KWA MUNGU

MFULULIZO: SAFIRI NA YOHANA

SOMO: YOHANA 1:6-8

 

Je, ni nani aliye mtu mkuu aliyeishi duniani? Si Yesu Kristo, kwa maana Yesu Kristo alikuwa Mungu. Yohana Mbatizaji ndiye aliye mtu mkuu zaidi duniani kwa maana Yesu Kristo alisema hivyo.

Mathayo 11:11- “Amini nawaambieni, hajatokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji. Lakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye.”

Nataka kuongea juu ya huyu mtu aliye mkuu zaidi, lakini pia nikueleze jinsi wewe unaweza kuwa mkuu zaidi kuliko Yohana Mbatizaji.

Mtume Yohana aliandika Injili ya Yohana- Yohana anaitwa mtume wa nuru, mtume wa uzima na mtume wa upendo.

Hakuna mtu katika Biblia tunaye elezwa juu yake kama Yohana Mbatizaji. Huduma ya Yohana ilidumu miezi sita peke!!

Yohana Mbatizaji halingani na mtu mwengine katika Biblia. Jina lake latisha watu. Hakuna mchungaji angependa Yohana kama mshirika.

Yohana alikuwa hodari sana lakini pia alikuwa mtu mnyenyekevu.

Chakula chake kilikuwa nzige na asali, nguo na mavazi yalikuwa ya kutisha zaidi.

Yohana hakuwa na hitaji ya chai, mikate na vyakula vya kawaida!!

Yohana alizaliwa na wazazi Watakatifu- Luka 1:5 -6. Yohana alijazwa Roho Mtakatikfu angali tumboni mwa mamaye. Luka 1:15- Roho wa Eliya ulimjaa Yohana ili awe mwenye kuenda mbele ya Mwokozi wetu Yesu Kristo- Luka 1:17. 

Hebu tumwone huyu mtu aliyetumwa kutoka mbinguni- kuna mambo matatu yaliyo sababu ya Yohana Mbatizaji kuwa mtu mkuu zaidi aliye zaliwa na wanawake.

Haya mambo pia yanahitaji kuwa juu yako ikiwa kwa kweli unamtafuta Mungu wako.

MWITO WA MUNGU JUU YA MAISHA YAKO- Yohana 1:6.

“Kulikuwa na mtu aliyetumwa na Mungu.”

  • Yohana mwenyewe alielewa na mwito wa Mungu juu ya maisha yake- Yohana 1:23.
  • Yohana alielewa vizuri sana hakuwa hapa duniani kufanya kazi ya kawaida.
  • Alikuwa hapa duniani kwa kazi mwafaka.
  • Mungu anapotaka kumtumia mtu, anamfanya tayari sana kwa kila kitu.
  • Kila mwana wa Mungu ni mwanawe na anaye mwito maalum juu ya maisha yake.
  • “Kuna mtu aliyetumwa kutoka kwa Mungu.”
  • Yohana alikuwa “mtu” si malaika.
  • Mpango wa Mungu ni watu- Waefeso 4:1.
  • Mtoto wa Mungu, je, mwito wako ni nini? Tembea mwito wako.
  • Pengine unasema, mimi ni mwalimu, mkulima, mtu wa mikono, biashara, fundi, lakini ni mwito.
  • Mungu alikuita na mwito na kazi ya kufanya.
  • Mungu ametupatia kila mtu karama, talanta na uwezo ili tutimize mwito wake.
  • Kila kazi unayofanya ni mwito, lazima ukafanye kwa utukufu wa Mungu.

MWITO WA MUNGU NI WA DHAMANI SANA, TUNAHITAJI UTII

  • Mungu anafanya kazi na wanaotii.
  • Ikiwa tunapenda Mungu ni lazima kumtii.
  • Utii ni gharama nyingi sana.
  • Mwito wa Mungu ni utii.

MWITO WA MUNGU NI PAMOJA NA UNYENYEKEVU WA KWELI

  • Yohana hakufanya MIUJIZA, Yohana hakuwa na kanisa kubwa na wafuasi wengi.
  • Yohana hakuvaa masuti ya pesa wala kula chakula na wakuu wa nchi.
  • Yohana hakuwaponya wagonjwa na kuwafufua wafu, Yohana hakutembea juu ya maji na kuwafukuza mapepo.
  • Hivyo kwa nini Yesu Kristo anasema Yohana Mbatizaji ndiye mkuu zaidi kwa wanadamu wote?
  • Unyenyekevu.

“Imenipasa kupungua na yeye aongezeke.”

  • Yohana aliishi na lengo moja pekee- “Utukufu wa Mungu.”
  • Hakuna nguvu na uweza kuliko ule unaopatikana kwa unyenyekevu na kumtumikia Mungu ili apate utukufu wote.
  • Bila unyenyekevu hatuwezi kupokea kitu chochote kutoka kwa Mungu.
  • Bila unyenyekevu tunajidharau mbele za Mungu.
  • Bila unyenyekevu hatuwezi kumwona Mungu- Zaburi 25:9.
  • Unyenyekevu unaweka moyo na roho yako katika hali ya kupokea kutoka kwa Mungu na kusema “Mapenzi yako yafanyike ndani yangu.”
  • Unyenyekevu unatoa ubinafsi- tunakufa kwa nafsi zetu kumwishia Mungu pekee- Yakobo 4:6.
  • Unyenyekevu unafanya mtu wa cheo cha juu zaidi kuwatumikia walio chini zaidi.
  • Yesu Kristo alinyenyekea zaidi akashuka chini mahali tulipo- Wafilipi 2:5-11.
  • Unaponyenyekea:
  1. Utainuliwa juu.
  2. Utaingia katika uwepo wake.
  3. Utakombolewa.
  4. Utakuwa mkuu katika ufalme wa Mungu.
  5. Utapokea neema nyingi zaidi kutoka kwa Mungu- Yakobo 4:6.

UJUMBE WA UTUKUFU NA TUMAINI- Mathayo 11:11

  • Hakuna nguvu zaidi duniani kama unyenyekevu na kutafuta utukufu wa Mungu- Matendo 1:8.
  • Baada ya miaka mingi huko Afrika Kusini (South Africa) missionary Robert Moffat alirudi kwao Scottland kujaribu kuwaita wengi kuwa missionaries Afrika.
  • Alipofika alishangaa sana ni wanawake wachache walimlaki!!
  • Ujumbe wake ulikuwa kutoka Mithali 8:4- “Kwenu wanaume ninawaita”.
  • Lakini hakukuwa na wanaume kanisa isipokuwa kijana mmoja wa miaka 14.
  • Kwa kuvunjika moyo, Moffat alikata ujumbe wake haraka. Hakuna aliyopokea mwito.
  • Baada ya miaka miaka, yule kijana alijitoa kuwa missionary Afrika, jina lake ni Dr. David Livingstone!!
  • Mungu anapotaka kazi yake itendeke anawaita watu, wanaume kwa wanawake wanyenyekevu.
  • Mungu leo anawaita watu wanyenyekevu kama Yohana Mbatizaji.

 

MWISHO

  • Mungu anatafuta kizazi cha Yohana Mbatizaji.
  • Anatafuta watu- watakao sema- “Bwana nipo nitume.”
  • “Kuna mtu aliyetumwa kutoka kwa Mungu.”
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *