MFULULIZO: NIFANYE NIWE BARAKA
SOMO: 1 TIMOTHEO 6:1-19 (11)
“Bali wewe mtu wa Mungu uyakimbie mambo hayo, ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi upendo. Piga vita vile vizuri vya imani. Shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi”-Vs. 11-12.
Huu ndio ujumbe wa pili katika mfululizo wa “Nifanye kuwa baraka.”
Wakati mtume Paulo anamuandikia Timotheo pamoja nasi, anataja mtu anayeitwa “Mtu wa Mungu.”
Paulo anasema ili uweze kufikia kiwango cha kuitwa “Mtu wa Mungu” au “mwanamke wa Mungu” ni lazima kukimbia mambo, kufuata mambo na kupigana vita vizuri-1 Timotheo 6:11-12.
Katika mazishi ya watu wengi, karibu kila mtu tunasomewa hadithi ya marehemu (eulogy).
- Kuzaliwa kwake.
- Masomo.
- Ndoa na mapenzi.
- Kazi-mahali, cheo.
- Jinsi huyu aliwaguza watu mbali mbali.
- Watoto wake, wajukuu.
- Yote aliyekamilisha katika maisha.
Lakini haitajwi tumekuja kumzika “mtu wa Mungu” au “mwanamke wa Mungu.”
Cha muhimu zaidi ambacho kinahitajika sana ni paweze kuandikwa juu ya kaburi yako “Hapa amelala “Mtu wa Mungu” au “mwanamke wa Mungu.”
Kwa sababu kuwa mtu wa Mungu si jambo la kawaida.
Hili tupate heshima na cheo cha kuitwa “mtu wa Mungu” au “mwanamke wa Mungu” kuna mambo ya kufanya na mambo yakutofanya.
Lazima kukimbia, kufuata na kupigana vita. Leo twaona mambo ya kufuata. Paulo ametupa mambo sita ya kufuata. Hebu tuyaone:-
FUATA HAKI-Righteousness.
- Mungu anapenda kila mtoto wake kufuata haki.
- Haki ni utakatifu na utakatifu ni haki.
- Utakatifu ni kujitenga na dhambi, wenye dhambi na kila hali ya dhambi. Kujitoa kwa Mungu kama dhabihu takatifu.
- Haki ni kufanya yaliyo sahihi na safi mbele za watu.
- Utakatifu na haki zinaenda pamoja, kwa maana huwezi kuwa mtakatifu na kukosa kuwa mwenye haki mbele za watu.
- Kuwa mwenye haki kila siku ni kuwa muadilifu (integrity).
- Tunaishi katika ulimwengu watu wanasema haki haina maana siku hizi, lakini haki ni ya mbele za Mungu.
- Kuwa mwenye haki Maanake ni:-
- Ikiwa umekopa fedha au mali ya mwenzako, lipa kwa wakati wa makubaliano.
- Lipa deni zako.
- Huwezi kuwa “mtu wa Mungu” ikiwa haulipi deni zako.
- Ikiwa umeajiliwa kazi, maliza hio kazi. Huwezi kuwa “mtu wa Mungu” ikiwa hautekelezi majukumu ya kazi yako.
- Ikiwa umesema utakuwa mahali fulani wakati fulani kukutana na fulani, kuwa pale wakati ule. Kukosa ni kuwa mwizi wa masaa ya mwenzako.
- Huwezi kuitwa mtu wa Mungu ikiwa huwezi kuweka saa.
- Kuwa mwenye haki ni lazima kutimiza haki, ukweli, upole, fadhili, unyenyekevu na kuaminika-Waebrania 4:15.
- Kuwa wenye haki lazima kuwa na sahihi na kila mtu.
- Kuwa mtu wa Mungu ni lazima kutenda haki katika kila jambo maishani.
- Haki kila mara ni mbele ya watu (human relationships).
- Kujiweka mbali na watu ni kuwa mbali na Mungu.
- “Mtu wa Mungu ni mtu wa Mungu, usiku na mchana, nyumbani na nje, safarini na ofisini.
- Fuata haki na kila mtu na utakatifu mbele yake Mungu-mtu wa Mungu.
FUATA UTAUWA (GODLINESS)-1 Tim. 6:11.
- Utauwa ni kuwa kama Mungu.
- Utauwa ni uhusiano wako na Mungu yaani kuwa haki na sahihi na Mungu wako.
- Utauwa ni kuwa kama Mungu-kuwa kama Mungu ni kupenda anayopenda Mungu na kuchukia anayoyachukia Mungu.
- Huwezi kuwa kama Mungu na kushiriki mambo ya shetani-kufundisha ulawiti, transgenderlism, umalaya, ukabila, ubaguzi.
- Kuwa mtu wa Mungu lazima kufuata utauwa.
- Je, wewe ni mtu wa Mungu?
FUATA IMANI (FAITH)-1st Tim. 6:11.
- Kuwa na imani ni kumtegemea Mungu-Waebrania 11:1. Ni pamoja na kuwa mtu wa Mungu kutegemewa (reliable), kuwa mwaminifu (fidelity, reliability or dependability).
- Kwa kawaida wachungaji wengi wanatumika kwa kanisa moja miaka (4.4) lakini katika biashara, shirika, serikali ni miaka 30.
- Kuwa na imani ni kuvumilia na kudumu.
- Mtu wa Mungu lazima kuwa mtu wa imani.
- Wachungaji wengi wanakaa katika makanisa ya miaka chache kwa sababu na kuwachunga watu wasio na imani.
- Mimi nimekaa hapa kwa sababu ya uaminifu wa wengi wenu.
- Mwaka wa 2021, makanisa 4,500 yalifunga milango, makanisa 3,000 yalianza USA. Hii ni kwa sababu ya washirika wasio na imani.
- Mtu wa Mungu ni mtu mwenye imani.
FUATA UPENDO (LOVE)-1 Tim. 6:11.
- Ikiwa mtu hafuati upendo hawezi kuwa mtu wa Mungu-Yohana 13:34-35.
- Amri ya Mungu kwetu ni upendo.
- Upendo wa Mungu ni bila masharti-Agape.
- Huwezi kuwa mtu wa Mungu bila upendo.
FUATA SUBIRA (PATIENCE)-1 Tim. 6:11.
- Subira ni uvumilivu na tunda la roho-Wagalatia 5:22-23.
- Hili tuwe kama Mungu tazama uvumilivu wa Mungu kwetu.
- Mungu ni Mungu wa subira ndio hatuangamizwi.
- Huwezi kuwa mtu wa Mungu bila subira.
FUATA UPOLE (MEEKNESS)-1 Tim. 6:11.
- Upole si unyonge bali ni kudhibiti nguvu zako.
- Upole ni mtu ambaye amezirudisha nguvu zake kwa Mungu.
- Mtu wa Mungu lazima kufuata upole.
- Yohana Batozaji alikuwa mtu mpole. Upole wa Yohana ndio ulikuwa nguvu zake (Joasephus).
- Yesu Kristo alisema “Kwa wote waliozaliwa na mwanamke hakuna mtu mkuu kuliko Yohana.” Kwa nini? Upole.
- Yohana alisema “imenipasa kupungua bali Kristo aongezeke.”
- Mfalme Daudi alikuwa mpole. Katika Zaburi zote za Daudi hakuna mahali amejipongeza kwa kumuua Goliathi!!
- Paulo alijiita mdogo wa mitume wote-upole.
- Huwezi kuwa mtu wa Mungu bila upole.
MWISHO
- Kuwa mtu wa Mungu au mwanamke wa Mungu lazima kuwa mtu anayefuata haki, utauwa, imani, upendo, subira na upole.
- Je, wewe ni mtu wa Mungu?
- Je, katika kaburi lako tunaweza kuandika “Hapa amelala mtu wa Mungu?”
- Mungu atupe neema ya kuwa mtu na mwanamke wa Mungu. Amen.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO. - September 21, 2025
- GOD GUIDES OUR DESTINIES. - September 21, 2025
- GOD OF THE BREAKTHROUGHS - September 10, 2025