Swahili Service

MUNGU ANAHESHIMU WANAOMHESHIMU

MFULULIZO: SIONI HAYA

SOMO: 2 TIMOTHEO 2:14-26

 

Biblia inafundisha wazi mambo yanayompendeza Mungu na yasiyompendeza. Mungu anapenda sana kuwaheshimu watu wake, lakini lazima na wao kumheshimu Mungu. Wana wa Eli hawakumheshimu Mungu. Eli alikuwa na dhambi ya kuwaheshimu wanawe kuliko Mungu. Eli alipata hukumu ya Mungu kwa Matendo yake- 1st Sam.2:29. Kuna watu aina nne wametajwa:-

  • Watu ovyo (useless).
  • Watu wanao tumiwa na wenzao.
  • Watu wanao tumia watu.
  • Watu walio bora.

Je, tunamheshimu Mungu kwa jinsi gani?

MPE BWANA WAKATI WAKO.

  • Daudi alimtafuta Bwana mapema.
  • Samweli alianza kumtumikia Mungu akiwa mtoto.
  • Zaburi 27:4- “Neno moja nimelitaka kwa Bwana nalo ndilo nitakalo tafuta, nikae nyumbani mwa Bwana siku zote za maisha yangu. Niutazame uzuri wa BWANA na kutafakari hekaluni Mwake.”
  • Wazo lake Daudi ni apatikane katika uwepo wa Bwana kila siku.
  • Sehemu ya wakati wako lililo maana zaidi ni wakati wako na utulivu mbele za BWANA- (Quiet time) – Q.T.
  • Danieli alichukia wakati wa kumwita Mungu BWANA WAKE mara tatu kila siku.
  • Enoko alitembea na Mungu mpaka akatoweka- Mwanzo 5:24.
  • Kutembea na Bwana ni maana kwamba uhusiano wako na Mungu ni bora- Amosi 3:3.

MTUMIKIE BWANA NA KARAMA ZAKO ZOTE

  • Kila mkristo anayo talanta moja na pia karama za Roho Mtakatifu.
  • Mfalme Daudi alikuwa mwimbaji wa nyimbo, alicheza kinubi, tarumbeta na vyombo vingi.
  • Nuhu alikuwa seremala, alijenga safina.
  • Luka alikuwa daktari wa dawa. Alitoa utumishi wake kwa ufalme wa Mungu.

MTUMIKIE BWANA NA MALI YAKO.

Mathayo 6:21- “Kwa kuwa hazina yako ilipo ndipo utakapo kuwepo na moyo wako.”

  • Mambo ya muhimu ya mtu yanaonekana kwa vile mtu anavyotumia wakati, fedha na nguvu zake.

MHESHIMU MUNGU KATIKA HEKALU LAKO.

1st Wakorintho 6:19-20- “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni Hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu mliyepewa na Mungu? Wala nyinyi si mali yenu wenyewe. Maana mlinunuliwa kwa dhamani, sasa basi mtukuzeni Mungu katika miili yenu.”

  • Hivyo ule vizuri, pumzika, fanya mazoezi.
  • Usijifanye najisi kwa pombe, uasherati wa uzinzi, madawa ya kulevya, tattoos na kujidunga dunga mwili wako.
  • Kimbia tamaa za ujanani, ukafuate haki na imani na upendo na amani pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi- 2nd Timotheo 2:21.
  • Yosefu alikimbia dhambi, Lutu alikimbia Sodomu, Musa aliacha anasa za Misri.

WATU WANAO HITAJIKA KANISANI NA WASIO HITAJIKA.

  • Watu wasio hitajika kanisani;-
  • Wanao lala kama Yona- watu wanapotea dhambini.
  • Wasio na nguvu kama Samsoni- vita vinapoendelea.
  • Watu wanaoficha dhambi kama Akani- Yoshua 7.
  • Watu wanaopenda anasa kama Daudi- 2nd Samweli 11:1-20.
  • Watu wenye kuwapendeza watu kama jinsi Herode- Matendo 12:1.
  • Watu wanao hitajika kanisani;-
  • Watu wenye kujitoa kama jinsi Danieli- 1:8.
  • Watu wanao kimbia dhambi kama Yusufu- Mwanzo 39:12.
  • Watu wanaofukuza pepo kama Paulo- Matendo 19:24-27.

 

MWISHO

  • Basi nasi sote tuwe kama 1st Wakorintho 15:58.
  • Kuimarika
  • Msitikisike
  • Mkazidi sana kutenda kazi ya BWANA siku ZOTE, kwa kuwa mwajua kwamba taabu yenu sio bure katika BWANA.

 

 

 

 

 

 

 

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *