MFULULIZO: JINSI YA KUSTAHIMILI DHOROBA ZA MAISHA
SOMO: II WAKORINTHO 12:7-10, II WAKORINTHO 11:1-30
Maisha si rahisi, maisha haya si kitanda cha maua ya waridi, bali maisha yana miiba yake. Mtu moja alisema. “Mungu hakuna wakati nilikushukuru kwa sababu ya miiba yangu, lakini nimekushuru zaidi mara elfu kwa maua uliyo nipa.” twahitaji kujifunza kumtukuza Bwana kwa miiba yetu.
Katika mwaka wa 1527, Martin Luther alikuwa na mwaka mgumu zaidi maishani. Tarehe 22, 1527, alikuwa akihubiri mle Wittenberg alipopata kizungu zungu na kuanguka chini, kutoka pale alipata kuwa mgojwa sana. Alipoendelea kupona, janga la virus likapitia mji wa Wittenberg, nyumba yake ikawa hospitali kwa wengi, watoto wake wakawa wagonjwa na marafiki wengi walikufa. Katikati ya janga hilo Martin Luther ndipo aliandika wimbo tunaofahamu “Mungu kwetu ni ngome imara.” (A mighty fortress is our God)
Katika maisha haya tutapambana na miiba ya kila haina. Tungependa kukwepa lakini miiba imo kila mahali waridi huja pamoja na miiba yake.
Hebu tusome tena (II wakorintho 12:7-10) Zawadi kuu ambayo kanisa lingali ipa dunia wakati huu ni NEEMA (GRACE).
Kuna neema ya kuokoka na kuna Neema ya kuishi maisha ya kikristo. Zawadi kuu na asili mali yetu si ratiba na mipango yetu nzuri, wala si mahubiri, lakini neema ya Mungu huku tukiishi maisha ya neema mbele ya ulimwengu kila siku.
Kwa miaka mingi tumehubiri kwamba, siku zinakuja kuwe na mpango mpya ya dunia hii, yaani “NEW WORLD ORDER.”
Saa hii “NEW WORLD ORDER” imefika mabandiliko makuu duniani yatafanyika hapa duniani mwaka huu wa 2020. mageuzi makuu yaani “revolution” imeanza. Dini (Kanisa) moja, serikali moja, fedha moja, benki moja, elimu moja, ujumbe moja, shetani ameketi juu ya kiti chake cha enzi yake. Haya yote yanafanyika kwa ruhusa ya Mungu Baba!! Mpiga Kristo tayari yupo duniani, nabii wa uongo naye yupo, mnyama aliyetajwa yupo na kahaba mkuu, wote wamejitokeza, kanisa limefungwa, tukirudi ujumbe utakuwa moja kutoka Roma na kwa dakika zilizo pangwa kwa ratiba ya kanisa la ulimwengu (world church)
Lakini neema ya Mungu aliyejuu, itatosha hata katika vita kali ilio mbele yetu neema yake itatosha, hata katika mauti na kifo.
Katika somo hili, mtume Paulo alipewa mwiba. Mwiba huleta maumivu. Huu mwiba ulikuwa ni shida Fulani hatujaambiwa mwiba huu ulikuwa kitu gani. Pengine mwiba huu ulikuwa ni ugojwa, jaribu, udhaifu, dhihaka, mateso, (II Wakorintho 11:29) jela na gereza (II Wakorintho 11:23-27)
Wengine wanafikiri mwiba wa mtume Paulo ulikuwa ni ungojwa wa macho, malaria (wagalatia 4:15 na Wagalatia 6:11).
Wengine wanasema Paulo alikuwa na ugojwa wa ASTHENES hau udhaifu wa mwili (II Wakorintho 10:10)
Wanahistoria wa kanisa la karne ya kwanza wanasema, Paulo mtume alikuwa mtu mdogo sana kwa umbo. Kichwa upara, miguu ilikuwa na rickets, macho makubwa na pua refu.
Lakini tutaishije katika miiba yetu? Biblia, katika kufungu hiki inatueleza mambo kadhaa.
Hebu tujifunze:-
I. KUBALI MIIBA YAKO (ACCEPT) (NALIPEWA MWIBA) 12:7-8
- Rev. Dr. John Orberg, mwandishi, mwalimu na mhubiri mkuu duniani alikuwa ni mtu wa kuanguka-anguka wakati wa kuhubiri. Watu walikuja kwa kanisa lake wajionee kama Orberg ataanguka!!
- Ilimpasa Dr. John Orberg kumtengemea Mungu kwa kila neno alilonena – Mungu alimtumia kuwaleta watu wengi kwa Kristo.
- Paulo alimwoba Mungu amwondolee mwiba huu mara tatu.
- Yesu Kristo alimwoba Mungu Baba kumwondolea kikombe cha uchungu mara tatu.
- Mara tatu maanake ni maombi yalikuwa ya huzuni nyingi zaidi.
- Paulo aliomba mara tatu, akamwanga roho ya huzuni zaidi.
- Paulo aliomba mara tatu, akamwanga roho yake kwa Bwana.
- Lakini mara tatu mbingu ilinyamaza kimya kabisa!!
- Baadaye Mungu aliongea, jibu la Mungu lilikuwa pengine tofauti na matarajio ya Paulo “Neema yangu yakutosha, maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu”
- Mungu hakuondoa ule mwiba, lakini alimpa Paulo neema ya kuishi katika mwiba.
- Pengine wewe pamoja nami tumeomba sana janga la coronavirus (covid-19) kuondolewa.
- Pengine umeomba biashara yako kufunguliwa, iwe ni hoteli, shule, usafiri.
- Pengine wewe mchungaji umeomba makanisa kufunguliwa, pamoja na injili ya mitaani.
- Lakini Bwana amesema, “neema yangu yakutosha”
- Je, neema ni nini? Neema ni kitendo cha Mungu kukupatia yale usiyestahili.
- Neema ni wokovu wa Mungu kwako.
- Neema ni ahadi ya Mungu kukupa kibali chake bila kukuhesabia.
- Neema ni nguvu, uwepo and na uwezo wa Mungu.
- Kabla mtume Paulo hajakutana na Mungu Paulo mwenyewe hakuwa mtu wa neema (Matendo 8:3)
- Paulo alipokutana na Mungu alibandilishwa ndiposa, Paulo ameongea sana neema na Amani ya Mungu.
- Paulo alipojua neema ya Mungu amepewa hakuweza kuomba tena mwiba utolewe!!
- Hivyo, Paulo mtu mfupi, kibara, miguu mifupi, macho kubwa na pua refu lakini Mwingi wa neema ya Mungu.
- “Neema ya Mungu haiwezi kukupeleka mahali haiwezi kukuhudumisha.”
- Maanake, hatuwezi kujaribiwa zaidi ya jinsi tuwezavyo.”
- Tusiombe mzigo nyepesi, bali omba nguvu zaidi.
- Tusiombe safari fupi, bali omba miguu ya nguvu.
- Tusiombe shida chache, omba suluhisho nyingi.
- Je, tutaishije maisha yaliojaa neema?
II. POKEA MIIBA YAKO (OWN YOUR THORNS) II WAKORINTHO 12:9) (BASI NITAJISIFIA UDHAIFU WANGU KWA FURAHA NYINGI)
- Kanisa ni mahali pa watu walio na shida.
- Kila mtu yuko na shida yake, lakini wengi waishi katika hali ya kukataa ukweli huu.
- Kanisa ni nyumba ya wagojwa, lazima tuwe na ujasiri na moyo wa kukubali na kupokea miiba yetu (accept and own your thorns).
- Kanisa ni mahali pa watu wa miiba!!
- Lakini wengi wanakuja na maski na kujifanya wao si watu wa shida na miiba.
- Wengi wanakuja na shida ya kuumia moyoni, lakini wanaokuja wanakutakana na watu wamevaa maski, wanafikiri ni wao tu wanaoshida, wanaona wakifungua mioyo yao watu watawakataa.
- Kujificha kwa maski kutakufanya maskini zaidi (Yohana 1:17)
- Fungua moyo wako kwa Bwana, wacha aone miiba yako maana neema na ukweli zinaenda pamoja.
III. TUMIA MIIBA YAKO (USE YOUR THORNS) MAANA NIWAPO DHAIFU NDIPO NILIPO NA NGUVU” (II WAKORINTHO 12:10)
- Yesu Kristo, katika (Mathayo 5:3) alisema “heri walio maskini wa roho maana ufalme wa mbinguni ni wao”
- Maanake “heri wale wanafahamu na kungundua udhaifu wao na wanao weka tumaini yao yote kwa Bwana.”
- Dunia na elimu ya ulimwengu na tamaduni zake zinafundisha kukataa udhaifu na kuuficha, lakini Biblia inafundisha, kukubali, kupokea na kutumia udhaifu wetu, kwa maana tunapo kubali, kupokea na kutumia udhaifu wetu tunapomwomba Bwana, kumtengemea kwa nguvu zake katika maisha yetu.
- Tunapokubali udhaifu wetu tunakuwa watu wa neema na kuneemesha wengine.
- “kijana moja alipanga harusi kumwoa mchumba wake wa miaka saba. Karamu ya harusi yake aliipanga na kuiadaa katika hoteli kubwa zaidi mjini Nairboi, gharama ya arusi hii ilikuwa kshs.1500000 (1.5m) baada ya kupanga kila kitu na kutangaza bi-arusi akavunja uchumba. Kijana alipojaribu kupata pesa zake kutoka kwa hoteli haikuwezekana kwa sababu hoteli tayari walikuwa wamenunua vyakula na mapambo yote. Hivyo kijana aliamua kuendelea na karamu, akaenda mahali alipolelewa katika mtaa ya mabanda nduni ya mathare valley slums akawaalika wengi. Hawa maskini kwa mara ya kwanza maishani wakala chakula katika hoteli-5 star. Huko wakitumbuishwa na wanamsiki mashuuri. Hawa watu wa mitaani wakafurahi zaidi.
- Huyu kijana alitumia udhaifu wake, na kuvunjika kwake kuwabariki watu wasiostahili.
- Huyu kijana aliwatendea miujiza watu wa mtaa
- Yesu Kristo alivaa taji ya miiba, akawa dhaifu hili sisi nasi tupate kuwa watoto wa Mungu.
MWISHO
- Bwana unifundishe utukufu wa msalaba ninaobeba
- Bwana nifundishe dhamana ya miiba yangu.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- CHRISTMAS: THE BIRTH THAT BROKE EVERY BONDAGE - December 25, 2025
- CHRISTMAS: WHY DID CHRIST COME? - December 24, 2025
- KRISMASI MAANAKE NI FURAHA KWA DUNIA YA DHIKI NA SHIDA - December 21, 2025
