Swahili Service

MUNGU NI M’WEZA

MFULULIZO: SIONI HAYA

SOMO: 2 TIMOTHEO 1:12-14

 

Mungu ni mwenye uwezo wote kufanya yote aliye ahidi kutenda. Hakuna jambo lililo ngumu kwake-Yeremia 32:17; Luka 1:37.

Hakuna anayeweza kupinga mipango ya Mungu-Ayubu 42:2. Mungu aliviumba vyote viweze kumtumikia-Zaburi 119:91.

Mungu anafanya yanayompendeza-Zaburi 115:3. Upana wa uweza wa Mungu ni mkuu zaidi.

  1. Mungu anaokoa kabisa-Waebrania 7:25.
  2. Mungu anao uwezo kuwasaidia wanao jaribiwa-Waebrania 2:18.
  3. Mungu anao uwezo kudhibiti yote-Wafilipt 3:21.
  4. Mungu anao uwezo kukomboa kutoka kwa moto-Danieli 3:17.
  5. Mungu anao uwezo kufanya zaidi ya matumaini yetu-Waefeso 3:20
  6. Mungu anao uwezo wa kulinda-Yuda 24; 2 Tim. 1:12.

Leo tunajifunza juu ya uwezo wa Mungu kulinda wokovu wako.

Katika kifungu hiki, Mtume Paulo anasisitiza juu ya uhakika wa kudumu katika wokovu.

Je, tunaweza kuwa na hakika juu ya wokovu?

Madhehebu mengi yanaamini wokovu unaweza kupoteza, kwamba aliyeokoka anaweza kupoteza tena. Miongoni mwa hawa kunao, Methodist, Lutherans, Anglican, Pentecostal, charismatic na protestant churches. Mtizamo huu unaitwa (ARMINIAN VIEW.)

  • Hawa wanaamini kwamba mtu anao uamuzi wa kukata wokovu kwa hiari yake mwenyewe.
  • Sisi Wabatisti tunaamini kwamba, Mungu anapotuokoa, hawezi kutunyang’anya wokovu.
  • Tunaamini kwamba mtu anapookolewa kwa neema ya Mungu, basi huyu atadumu kabisa katika wokovu daima.
  • Tunaamini kwamba tunaokoka kwa uamuzi wa binafsi, lakini wakati wa kuokoka mtu anabadilishwa mara moja na kufanywa kuwa mwana katika jamii ya Mungu.
  • Tunaamini mtu anapookoka uhusiano bora unafanyika kati yetu na Mungu lakini ushirika wetu na Mungu unaweza kuvunjika na kurejeshwa kupitia kuungama dhambi.
  • Je, ni nani aliye sahihi. Je, Yesu Kristo anaweza kukulinda katika wokovu usipotee? Mungu anaweza.
  • Mtume Paulo anajibu maswali haya katika kifungu cha 12. Hebu tuone na kujifunza:-

UONGOFU WA PAULO (Conversion)

Kuokoka kwa Paulo kulihusisha mtu.

  • Paulo anasema “Ninamjua yeye niliyemwamini na kusadiki.”
  • Paulo anasema alikutana na Kristo kwa njia ya kwenda Damaseki-Matendo 9:4-6.
  • Paulo anasema mtu wa dini, kulingana na dini hiyo Paulo alikuwa mtakatifu zaidi ya wote-Wafilipi 3:6.
  • Paulo anasema wokovu wake ni uhusiano na mtu aitwaye Yesu Kristo.
  • Hii ndio njia pekee ya kuokoka. Wokovu ni uhusiano na Yesu Kristo-Waefeso 2:8-9; Matendo 4:12; 1 Yohana 5:12.
  • Wokovu ni kukutana na Yesu Kristo moja kwa moja, uso kwa uso kwa njia ya imani.

Kuokoka kwake Paulo kulikuwa mpango.

  • Paulo anasema kuokoka kwake kulikuwa ni njia ya “kuamini.”
  • Kuokoka ni imani ndani ya “mtu”-Yesu Kristo- Yohana 3:16; Warumi 10:9; Yohana 3:36. Wokovu ni wako kwa imani pekee ndani ya Yesu Kristo pekee.

Wokovu wa Mtume Paulo ulikuwa wakovu wa kudumu-“Ninamjua niliye mwamini.”

  • Tunapomjia Yesu Kristo kwa imani, anatuokoa daima milele-Tumebadilishwa.
  • Wakovu aliyetununulia Kristo huwezi kurudiwa tena-Waebrania 6:4-6 (eternal security).

UJASIRI WA MTUME PAULO.

Ujasiri wa Paulo umejengwa juu ya Mungu.

  • Paulo anao hakika ndani yake aliyemwokoa.
  • Watu wanao hakika ya wokovu wao pia wana imani timilifu.
  • Watu hawa wanamwamini Mungu wao kwamba ni mwenye uwezo wa kuwalinda.

Ujasiri wa Paulo umejengwa juu ya nguvu za Mungu kulinda wokovu wake.

  • Mtume Petro pia aliamini nguvu za Mungu kulinda wokovu-1st Petro 1:5.
  • Wokovu wetu unategemea nguvu za Mungu kulinda-Isaya 26:4; Luka 1:37.

Ujasiri wa Paulo ulijengwa juu ya ahadi za Mungu.

  • Paulo anasema “amesadiki” nguvu za Mungu kulinda roho yake.
  • Paulo amesadiki wokovu ni kwa neema, wokovu ni wa milele, wokovu ni kipawa cha Mungu, hakuna kinachoweza kunitenga na ufalme wa Mungu-Warumi 8:38-39.
  • KUJITOA KWA PAULO.

Mtume Paulo alijitoa nafsi yake.

  • Paulo alimtegemea Mungu akampa nafsi, mwili na roho milele.

Paulo alitoa huduma na utumishi wake kwa Mungu.

  • Huduma yake kwa Mungu alimpa.

Paulo alitoa wokovu wake kwa Mungu.

  • Mpaka siku ya Bwana na siku ya mwisho duniani ni mbele ya kiti cha hukumu.
  • Paulo alijua siku yake ya mwisho duniani atakuwa ndani ya Kristo-Wafilipi 3:9.
  • Wokovu hautegemei nafsi yangu, lakini Yesu Kristo na nguvu zake za kulinda nilichoweka amana kwake Yesu Kristo.

MWISHO

  • Kila mmoja wetu aamini kwamba kunaye Mungu mkuu mbinguni aliye uwezo wa kuokoa, kulinda na kuhifadhi nafsi zetu mpaka mwisho wa dahari.
  • Huyu Mungu aliyetuokoa atatufikisha mbinguni salama-1 Wathesalonike 5:23.
  • Je, uliwahi kuokoka siku moja? Je, unao hakika ya wokovu wako?
  • Kama hauna hakika, leo hii toa nafsi yako kwake.
  • Kama unao hakika, basi ishi katika hakika Mungu anakulinda mpaka siku ya mwisho na milele.
  • Yesu Kristo anaokoa kabisa-Waebrania 7:25; Wafilipi 1:6.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *