MFULULIZO:UPENDO WA MUNGU
SOMO: MALAKI 1:1-5
Upendo wa Mungu ndio ujumbe wa katikati katika Biblia. Malaika alianza unabii wake na neno la upendo wa Mungu. “Nimewapenda ninyi, asema Bwana” lakini watu walikuwa wamerudi nyuma wakamwambia Mungu “umetupendaje?” walikuwa wamepoteza upendo wao kwa Mungu wao. Hivyo Mungu alianza kuwaeleza jinsi alivyowapenda tangu wakati wa Yakobo na Esau. Watu wa mbali walijua kwamba Mungu alipenda Israeli kwa sababu ya jinsi aliwachangua kutoka kwa wengi katika mataifa, jinsi aliwashindania juu ya adui zao.
Hebu tujifunze juu ya upendo wa Mungu:-
I. UPENDO WA MUNGU NI KWA WASIOSTAHILI (V.2-3) (UNMERITED).
- Bwana alisema “nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia”
- Mungu alimkataa Esau, kwa sababu Esau hakuwa mtu wa Imani (Waebrania 11:6)
- Yakobo alichanguliwa pamoja na jamii yake, naye Masihi Kristo akazaliwa kwa jamii ya Yakobo.
- Yakobo alichanguliwa kwa neema yake Bwana.
- Uchanguzi wa Yakobo ulifanyika kabla ya wao kuzaliwa.
- Esau na Yakobo hawakustahikli upendo wa Mungu , lakini neema inachangua kulingana na nguvu na ufahamu wa Mungu.
- Mungu anatuchangua kwa neema yake, hivyo tunaokolewa kwa neema, tunamtumikia Mungu kwa neema, tunaishi na kulindwa na neema, hivyo upendo wa Mungu ni kwa wasiostahili.
II. UPENDO WA MUNGU HAUBANDILIKI (UNCHANGING)
- Mungu anaposema “Nimewapenda ninyi” maana yake ni “nimewapenda na ningali ninawapenda.” “I have loved you and I love you still.”
- Wana wa Israeli walikuwa wamemwasi Mungu, hawakumpa BWANA heshima (V.6) walimtolea Mungu chakula najisi (V.7), walimwasi Mungu katika sharia ya ndoa zao (Malaki 2:16) walikuwa wamemkosa Mungu katika sadaka zao na zaka zao (Malaki 3:7-13)
- Hata ingawa Israeli waliyafanya hayo yote, upendo wa Mungu ulizidi kwao.
- Upendo wa Mungu ni wa milele, haubandiliki kamwe.
III. UPENDO WA MUNGU NI KWA WOTE (UNIVERSAL)
- Uchanguzi wa Mungu kwa Yakobo na Esau, haikuhusu wokovu, hau milele, lakini kwa ufalme wa Mungu na kuzaliwa kwa Kristo.
- Waisraeli, walichanguliwa na Mungu kuwa missionary kwa ulimwengu wote, hili wote waokoke.
- Upendo wa Mungu umeonyeshwa kwa kila mtoto wa Mungu kwa njia nyingi:
- kuchanguliwa na Kristo Yesu tangu jadi.
- Kristo ametuweka katika agano lake.
- Wokovu wa Yesu kwetu na uzima wa milele.
- Msamaha wa dhambi, kuhesabiwa haki, kufanywa wana wa Mungu na utakaso.
- Mungu amekulinda kila siku na ahadi yake ya uzima wa milele.
MWISHO
- Ujumbe wa Malaki ni ya kwamba, Mungu aliye mkuu, wa milele, mwenye nguvu zote anakupenda na upendo usiyestahili, usiobandilika na upendo mkuu kwa wote (Yohana 3:16).
- Je, utampenda Mungu kama jinsi anavyokupenda?
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
