Swahili Service

MUNGU, TALAKA NA BIBLIA

MFULULIZO: MUNGU IN UPENDO

SOMO:   MALAKI 2:10-16, YEREMIAH 3:6-8, MATHAYO 19:9           

Talaka ni jambo linalo husu watu wote. Wengine hapa wamepitia kwa njia moja hau nyingine talaka. Pengine wazazi, watoto, jirani hau washirika wamekuhusisha katika ndoa zao na shida za ndoa zao. Biblia imenena mengi juu ya ndoa, talaka na ndoa za pili.

Hebu tujifunze:-

I.   MUNGU HAPENDEZWI NA TALAKA (MALAKI 2:10-16)

  • Mungu alipoanza ndoa, alipenda ndoa kudumu mpaka mwisho wa maisha, kwa hivyo mawazo yetu juu ya ndoa yanahitaji kuwa hivyo.
  • Mungu hakupanga ndoa za kuvunjika na talaka.
  • Lakini pia maana Mungu anayafahamu yote, Mungu anaruhusu talaka katika Biblia.(2:10-16)
  • Malaki anatueleza kwamba Mungu alikuwa na sababu tatu za ndoa.
  1. Ndoa inaonyesha jinsi Mungu alivyo (to mirror God’s image)
  2. Ndoa ni kwa sababu ya umoja katika mume na mke wake. (marriage is for communion)
  3. Ndoa ni Mungu kutafuta uzao wenye kumcha Mungu (Godly heritage)
  • Malaki alikuwa akizingatia jambo la wanaume waliokuwa wakiwaacha wake zao na kuwatalaki, baadaye hawa wanaume waliwaoa wanawake wakigeni.
  • Wanawake wengi hawakuwa na makosa yeyote kutalakiwa na mume zao.
  • Hawa wanaume walipenda wake wa kigeni kwa hivyo uhusiano wao na Mungu ulikuwa ovyo pia.
  • Walikosa imani na Mungu na wake zao, hawakuzingatia uhusiano wao na Mungu.
  • Hawa wanaume waliendelea kuabudu miungu ya kigeni, miungu ya wanawake wa kigeni (V.14)
  • Malaki anawaeleza kwamba talaka inaweza kuwa jamba la binafsi lakini talaka unausisha kila mtu, watoto, wakwe, kanisa, rafiki na uma. (V.16)
  • Talaka ni udhalimu kwa uhusiano na umoja wa jamii na umma.
  • Mungu anaelewa na talaka kibinafsi, kwa maana Mungu mwenyewe alitalaki Israeli kwa sababu ya ukahaba (Yeremia 3:6-8 )
  • Mungu anaelewa na uchungu wa talaka maana amepitia katika talaka.
  • Lakini Mungu aliwasamehe wana wa Israeli na kuwarudisha kwake. Panapo dhambi pana msamaha.

II.  TALAKA KATIKA BIBLIA

  • Hebu turudi katika Biblia na Agano la kale tuone jinsi Biblia inasema na tuelewe ni kwanini Yesu Kristo alisema aliyosema katika (Mathayo 19:9)
  • Wakristo wengi wamekuja kuelewa kwamba Yesu alisema sababu moja pekee ya talaka ni uasherati.
  • Katika agano la kale wayahudi na dini yao ya kiyahudi yaani (Judaism) makuhani walitengewa maandiko mawili juu ya talaka. (Kumbu Kumbu ya Torati 24:1)
  • Hati ya kuachana (Certificate of Divorce) ilikuwa ni bima hau, ulinzi kwa mwanamke aliyeachwa na mme wake.
  • Hati ya kuachana ilikuwa na maana mbili.
  1. Mume aliyemwacha mke wake hangeweza kumrudia tena.
  2. Hati ya kuachana pia ilimruhusu mwanamke aliyeachwa kupata kuolewa tena ili asisumbuke hau apate kuingia kwa ukahaba.
  • Mke huyo alipopokea ile hati ya kuachwa mme huyo alipoteza haki zake zote na huyo mke alikuwa tayari na huru kuolewa na bwana mwingine.
  • Biblia katika (Kumbu Kumbu 24:1) “Neno ovu” maanake ni uesharati (sexual immorality).
  • Kutoka 21:10-11)
  • Katika mistari hii ya Biblia twaona sababu zingine mbili za kuachana. Yaani mke kumwacha Bwana wake. (Chakula chake, nguo zake na ngono yake) hizi zote tatu zisipunguzwe kamwe. (in polygamous situations). Ngono ni pamoja na upendo.
  • Hivyo kiapo cha ndoa kilikuwa sehemu tatu. Uaminifu, chakula na nguo, upendo na ngono. (fidelity, provision and sexual relationship and     affection)
  • Talaka na kuachana kulienda sababa na haki ya kuolewa na kuoa tena (divorce and remarriage)
  • Mateso katika ndoa yanakuja kwa sababu ya kukosa upendo.

 

III. YESU KRISTO ALIYOSEMA KATIKA MATHAYO 19:1-9

  • Kristo katika Mathayo 19:9 na Luka 16:18 alikuwa akichangia swali aliyoulizwa na    mafarisayo juu ya sharia ya Musa na mpango wa Mungu juu ya ndoa.
  • Wataki wa Musa, talaka ilikuwako nyingi sana.
  • Seneca, mwana historia mkuu katika historia ya wayahudi ameandika juu ya mwanamke aliyekuwa ametalaki mara 23.
  • Yesu aliwaambia mafarisayo, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao Musa aliruhusu lakini hapo mwanzo haikuwa hivyo.
  • Utafusiri wa kiebrania kwa Greek ulipata mashaka – kulikuwa na wale walitalaki wake zao mbila sababu yoyote hivyo talaka zao zilikuwa si halali ni sharia hivyo Yesu na msimamo wake katika (Mathayo 19:9 na Luka 16:18)

IV.  RABI HILLEL NA SHAMMAI

  • Miaka katha kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo kuliishi rabi wawili Hillel na Shammai.
  • Hawa wawili walikuwa na shule zao jau ya talaka, wote walikuwa na wafuasi si haba. Juu ya Kumbu Kumbu 24:1
  • Hillel alifundisha mtu anaweza kumtalaki mke wake kwa sababu yeyote (anycause) Mathayo 1:19.
  • Shammai alifundisha kwamba talaka ni kwa sabau moja tu-uesharati.
  • Yesu Kristo alisimama na shammai, msimamo ambayo mtume Paulo pia amekaza sana juu ya (Kumbu Kumbu 24:1)
  • Talaka ni jambo la kuhuzunisha sana lakini talaka inaruhusiwa panapo uesherati, kutokutosheleshwa na kukosa ngono na upendo (infidelity, provision and love)

MWISHO

  • Talaka si nzuri hata mme na mke wakikumbaliana kuachana.
  • Talaka inaudhi watoto, jamii, kanisa na umma
  • Mungu anachukia talaka.
  • Tuwe na huruma na upendo kwa wale wamepitia hali ya talaka.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

1 thought on “MUNGU, TALAKA NA BIBLIA”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *