MFULULIZO: MJUE MUNGU WAKO.
SOMO: MWANZO 7:16.
Mungu anapomfungia mtu, anafungia nje mauti, hatari zote, tauni na uaribifu wote. Katika mwaka huu wa 2026, sisi hatuhesabu ulinzi kutoka kwa mwanadamu au kutegemea nguvu za mwanadamu-Tunamlilia Mungu Bwana wetu pekee atupe ulinzi wake. Tunategemea nguvu zake za kutufungia-Mwanzo 7:16.
“Na walioingia,waliingia mume na mke na kila kitu chenye mwili, kama vile alivyomwamuru Mungu, Bwana akimfungia.”
Kila mtu anapenda kuwa salama-Usalama kutokana na maovu, hatari, uaribifu na dhoruba za maisha.
Usalama ni hitaji la msingi kwa kila mmoja wetu, lakini katika dunia inayojaa dhoruba na ubaya na dhambi, ulinzi wa mwili huwezi kutosha. Hata ingawa tunafunga nyumba zetu, tunaweka CCTV, na kujilinda kwa magonjwa, lakini mabaya na maovu yanatupata.
Ukweli ni kwamba mipango ya mwanadamu kujilinda haitoshi. Lakini ulinzi wa Mungu ni kamilifu.
Katika Mwanzo 6, Nuhu alimtii Mungu kujenga ile safina. Nuhu aliyafuata maagizo ya Mungu, alitumia vifaa vyote kama jinsi yaliyokuwa maagizo ya Mungu, lakini baada ya yote kutendeka, Mungu alifanya jambo la ajabu kuu-Mwanzo 7:16, “Bwana akamfungia.”
Kifungu hiki cha maandiko kina maana fiche, kwamba usalama na ulinzi wa kweli hautoki tu katika kumjua Mungu na kumtii, lakini ulinzi wa kweli unatoka kwa Mungu.
Safina ilikuwa salama si tu sababu ilijengwa vizuri lakini kwa sababu Mungu mwenyewe alimfungia Nuhu ndani ya lile safina.
“Bwana alimfungia” haikuwa kufungiwa ki-asili lakini Maanake ni kwamba BWANA alimfungia Nuhi kiroho,,mbali na hukumu, hatari na uaribifu.
Mungu aliye “Mfungia” Nuhu ni yeye yule anaye wafungia watu wake leo.
Mungu anapokufungia, basi, amefungia nje yako mauti, hatari na uaribifu. Katika mwaka huu wa 2026, hatutegemei mbinu, mipango na nguvu za mwanadamu, tunamlilia Mungu wa ulinzi atufungie ndani. Hebu tutazame:-
KUFUNGULIWA NA MUNGU, NI MUNGU KUJITOA KUKULINDA WEWE.
Mungu hatumi watu kukulinda-Zaburi 121:3-4.
- Aliye mlinzi wa Israeli hasinzii wala halali usingizi.
- Mungu mwenyewe ndiye mlinzi wako binafsi.
Mhuri wake una nguvu zaidi kuliko nguvu za mwanadamu-Mhubiri 9:11.
- Ulinzi wa kweli si kwa wenye nguvu au wale wamejihami sana.
- Ulinzi na usalama ni kwa wale wanalindwa na Mungu mwenyewe.
Ulinzi wa Mungu ni kamilifu na tosha-Ayubu 1:10.
- Hata shetani alishuhudia kwamba Mungu alimzingira Ayubu kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake na vitu alivyokuwa navyo.
Mungu anapokufungia-hakuna kitu chochote kinaweza kuingia pasipo kibali cha Mungu-Ufunuo 3:7.
- Mungu anapofunga hakuna wa kufungua, Mungu anapofungua hakuna wa kufunga.
- Nuhu na jamii yake walifungiwa ndani na Mungu-Dunia yote iliangamia katika gharika-Mwanzo 7:16.
ULINZI WA MUNGU UNAFUNGIA NJE GHARIKA NA MAFURIKO YA ADUI.
Leo hii kuna mkondo na mafuriko ya uovu duniani-Isaya 59:19.
- Adui anakuja kama mkondo wa maji-Mungu anainua standard ya juu zaidi,
Mungu anajua jinsi ya kuwalinda watu wake katikati ya hukumu-2 Petro 2:9.
- Mungu anajua kuwaokoa watauwa na majaribu.
Ulinzi wa Mungu si kwa mwili pekee, bali ni pamoja na nafsi, roho na hisia-Zaburi 91:5-6.
- Hatuogopi hofu ya usiku wala mshale urukao mchana, wala tauni ipitayo gizani wala uele uharibuo adhuri.
- Hatari zipo kila mahali, lakini ulinzi wa Mungu ni dhabiti popote wakati wote.
“Kufungiwa ndani” na Mungu Maanake ni kuzingirwa na uwepo wa Mungu-Zakaria 2:5.
- Mungu kwetu ni ukuta wa moto unaotuzunguka pande zote na Mungu pia ni utukufu ndani yetu.
- Wana wa Israeli waliona ulinzi wa Mungu mle Geshoni, kiasi tauni zilipopita Misri hazikufika Geshoni-Kutoka 8:22.
MUNGU ANAPOKUFUNGIA NDANI ANAFUNGIA NJE KULA NGUVU ZA GIZA.
Mungu anajua kilio cha kufungia ndani na kile cha kufungia nje-Zaburi 34:7.
- Malaika wa Bwana hufanya kituo, akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.
Kufungiwa ndani Maanake ni kufunikwa hata husipofahamu-Zaburi 121:7-8.
- Mungu anakulinda unapotoka na unaporudi.
Mungu anapokulinda hakuna mpango wako utakao kosa kustawi-Isaya 46:10.
- Atakulinda njia zako zote, mwanzo mpaka mwisho.
- Dunia huenda ikafurika, lakini Mungu atakupandisha juu zaidi ya mafuriko yale-Mwanzo 7:17-18.
- Pahali watu wengine wanazama, wewe utainuka juu zaidi.
- Danieli katika tundu la simba, hangeweza kuuliwa na simba, sababu ya ulinzi wa Mungu-Danieli 6:22.
KUFUNGIWA NDANI NA MUNGU, KUNAHITAJI UTII NA IMANI.
Nuhu alitii maagizo, akajenga lile safina kulingana na maagizo-Mwanzo 6:22.
- Utii ndio msingi ya mhuri wa Mungu kuwa juu yako.
- Hauwezi kufungiwa ndani ya ulinzi wa Mungu usipokuwa katika mapenzi ya Mungu-Isaya 1:19.
- Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi.
Kulindwa na Mungu ni dhawabu ya kutembea na Mungu-Mwanzo 6:9.
- Nuhu alikuwa mwenye haki, akatembea na Mungu katika siku zake.
Ni lazima kudumu katika uwepo wa Mungu hili tupokee ulinzi wake-Ruthu 2:12.
- Mungu atazawadi wale wanaochukua hifadhi chini ya mabawa yake.
- Rahab alipata hifadhi na usalama, sababu alikubali mpango wa Mungu-Yoshua 2:18-21.
ULINZI WA MUNGU NI KWA VIZAZI KWA VIZAZI NA ULINZI WA MUNGU UNAWEZA KUPEANWA.
Mungu anapokufungia ndani, anakufungia pamoja na nyumba yako-Mwanzo 7:1.
- Mungu alimwambia Nuhu, njoo wewe pamoja na nyumba yako, pamoja na wanao na mke zao.
Ulinzi wa Mungu unawafunika watoto wako hata wakati umekufa-Zaburi 103:17.
- Ulinzi na baraka za Mungu zinaenda vizazi baada ya vizazi.
- Unapoomba, ombea watoto wako, weka hua juu ya maisha yao na vizazi vyao baada yako kuwa duniani-Maombolezo 3:25.
- Mungu ni mwema kwa wale wamgojeao.
Ulinzi wa maagano unawafikia wote, uzao wako wa kiroho na uzao wa mwili-Matendo 2:39.
-
- Ahadi za Mungu ni kwako na watoto wako.
- Lutu alikombolewa kwa sababu ya maagano ya Mungu na Ibrahimu-Mwanzo 19:29.
MWISHO
- Ndugu zangu, siku tunazoishi zimejaa hatari za kiroho na za kimwili.
- Lakini tunamtumikia Mungu wa ulinzi na usalama.
- Mungu wetu anajua hatari zinazokaa mbele zetu, Mungu peke yake ndiye anaweza kutulinda kutoka hatari hizi zote.
- Katika mwaka huu, kila siku omba, “Bwana nifungie ndani ya safina la salama, kwa rehema zako nifungie ndani, fungia nje adui zangu na kila mafuriko na gharika ya mapepo.”
- Omba “Bwana nifungie mbali na ajali na mikosi, na mauti.”
- Bwana nifungie ndani yako, weka ukuta kunizingira mimi, watoto wangu na nyumba yangu.
- Mungu atawalinda walioingia katika safina yake. Je, wewe umo ndani ya safina ya Mungu?
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- MUNGU WA ULINZI - February 1, 2026
- YOUR STAR MUST SHINE - January 28, 2026
- MUNGU WA ISHARA NA MAAJABU - January 25, 2026
