MFULULIZO: MAISHA NA NYAKATI ZA DAUDI
SOMO: 1 SAMWELI 18:14-30
Mikali anawakilisha wanawake wanaoumia wasioeleweka, waliokataliwa. Wamevunjwa mioyo, wametusiwa na kutumiwa vibaya, wamekanyangwa chini. Hebu tuone maisha ya Daudi na Mikali, “Mwanamke anapompenda mwanamme.”
AINA ZA WANAWAKE DUNIANI.
- Wanawake ni wa aina nyingi.
- Wapenda sherehe (party girls). Hawa wanapenda sana kuwa na maisha mema na ya raha.
- Wanaweza kupenda pombe, vilabu na ngono. Kuna wale watapenda raha sana kiasi wawe walevi na usanii.
- Maisha yao ni maisha ya kujifurahisha nafsi zao. Urembo na mavazi, kutembea na usafiri/utalii.
- Wanawake wa gharama ya juu zaidi-(High maintenance woman).
- Hawa ni wanawake wa matumizi ya juu sana.
- Lazima mme kutumika pesa nyingi kuwafurahisha, kuwavalisha, kuwarembesha na kulisha.
- Hawa ni wanawake grade ya juu.
- Wanawake wazimu (psycho woman, crazy).
- Hawa ni wazimu kiasi, watafanya mambo ajabu bila aibu na bila kutumia akili zake. Hawajali matokeo ya vitendo vyao.
- Hawa wanaweza kuwa na fujo, vita
- Wanarusha na kutupa vitu, vyombo na chochote kipo karibu na wao.
- Wanaweza piga nduru na kutamka matusi hata mbele za watu na jamii.
- Wanaweza vunja nyumba au gari, kuchoma nyumba, nguo-wazimu.
- Kazini wanaweza leta aibu, kutisha watu-hawa ni wanawake wazimu na kisirani zaidi kichaa.
- Mke nyumbani (house wife).
- Huyu ni mwanamke hodari nyumbani, anayajali maisha, mipango na taratibu.
- Huyu anapanga mambo ya nyumba na jamii yake kama kazi yake-Mithali 31.
- Mfuata mtu (stalker woman)
- Mwanamke huyu kila wakati anafuata mumewe. Anataka kujua mme yuko wapi kila saa.
- Anataka kujua mumewe anafanya nini, wapi na nani. Anataka kujua mumewe anafikiri nini kila wakati.
- Mwanamke maonyesho (show girl/drama queen).
- Huyu ni mwanamke wa vituko na kupanga vituko na kuongea vituko vyake (drama queen).
- Mwanamke wa dini (religious woman).
- Huyu naye anapenda sana dini, kila kitu kwake ni dini.
- Mwanamke bosi (mke dume, mke bomba).
- Huyu naye anapenda kuongoza kila mtu, watoto, mme, jirani, wazazi.
- Anapenda kukalia kila uhusiano.
- Mke vipawa (jackpot woman).
- Huyu naye yuko na kila kitu, sura nzuri, pesa, akili, kazi, masomo, marafiki wa cheo, jamii yake mashuhuri, mali, heshima na lugha.
AINA ZA WANAUME DUNIANI.
- Kupe (parasite).
- Huyu mwanamme anatafuta mke wa kumsaidia, anategemea mke au wanawake wamlee.
- Huyu hana mpango wa kujitegemea kufanya kazi, kuchoka, kulima. Huyu ni kiwete cha maisha lakini zaidi tu kupe ya kunyonya damu ya mke, jamii na nchi.
- Mwame rahisi (cheap man).
- Huyu naye hapendi kutumia pesa na mali yake juu ya yeyote hata kwa nafsi yake.
- Anajali sana uchumi, hapendi kutumika.
- Mpenda raha-mwenye kujipenda (hedonist-self-lover).
- Huyu naye anapenda raha zote za dunia hii, iwe ni mavazi, nyumba, gari, pombe, usafiri, utalii, chakula na vitu vya dhamani.
- Mdanganyifu (cheater).
- Huyu naye atadanganya kila mtu mpaka yeye mwenyewe.
- Huyu lazima kudanganya kwa kila kitu.
- Hawezi kuishi na kumpenda mke mmoja, lazima ataenda nje ya ndoa na kulala na yeyote yule hata watu wa damu yake na ukoo.
- Huyu ni mwanamme Malaya, mzinzi na msherati.
- Kaburu- Beberu, gaidi (dictator/bully).
- Huyu naye ni beberu ya mtu, katika uhusiano ni lazima atawale.
- Huyu anapenda njia yake mwenyewe wala si njia ya mwengineo.
- Mtoto wa mama (mama’s boy).
- Huyu naye hata awe ameoa ni lazima awe na mama yake katika maisha yake.
- Katika kila maamuzi lazima mama yake kuhusika.
- Huyu hapendi kuhama na kuacha mama yake. Anapenda mamake karibu naye.
- Mfuata mtu (stalker).
- Huyu naye anamfuata mke wake au rafiki wake wa kike. Anataka ajue mke yuko wapi, na nani, unafanya nini na je, ni kitu gani anafikiria sasa hivi?
- Anataka kujua siri zote, simu na mawasiliano yake na kila mtu.
- Huyu atakufuata bila wewe kujua.
- Huyu anaweza kuwa mtu wa vita sana na ghadhabu nyingi.
- Mlevi (addict).
- Huyu naye anapenda sana sumu yake- iwe ni pombe, madawa ya kulevya, wanawake, michezo, marafiki, densi.
- Mwenda wazimu (mentally ill/crazy).
- Huyu naye ni mwendawazimu lakini hajui ni wazimu gani yuko nao.
- Mtu kamilifu (perfect man).
- Huyu naye yuko mkamilifu katika eneo zote za maisha.
- Kiroho- ameokoka, kifedha yuko na uwezo wa kulipa gharama zake zote, kiakili anaweza kuamua mambo katika jamii.
- Heshima- anajiheshimu na kuwaheshimu watu wote.
- Huyu ni mtu anayependa jamii (mature-emotionally, financially, socially, spiritually, economically, psychologically and mentally).
DAUDI, MIKALI NA SAULI
- Daudi ametoka kuwa si mtu mpaka kuwa mtu mashuhuri sana katika Israeli na nchi jirani.
- Daudi ametoka maisha ya fiche sasa amejulikana na kila mtu.
- Daudi sasa anajulikana na mfalme, taifa, watu wote, jeshi lote, wanawake wote, jamii ya mfalme Sauli pia imemfahamu Daudi sana.
- Kila mtu anapenda kufika kiwango hiki ambacho Daudi alifika.
- “Kufaulu kuna baba wengi lakini kutofaulu ni yatima.”
- Kitu kimoja katika kufaulu kwake Daudi ni kwamba wanawake walimpenda sana!!
- Kufaulu kwake Daudi kulimletea vipawa na zawadi nyingi. Zawadi moja ni kuwa mme wa Binti yake mfalme Sauli.
- Daudi alikuwa na wake wengi pamoja na Abigaeli, Ahinoam, Bethsheba, Mikali na Mazuna. Leo twaangazia uhusiano wa Daudi na Mikali.
- Mikaili anawakilisha wanawake wengi duniani na kanisani.
- Wanawake wengi wanateseka, kudharauliwa, kutumiwa vibaya na kukataliwa.
- Je, ni kwa nini wanawake wengi hawapendi kuolewa, kwa nini wengi wana hasira na uchungu sana?
- Wengi hawana raha, matarajio na sura ya tumaini. Kumwelewa Mikali kunasaidia.
- Mikali alikuwa bintiye mfalme Sauli.
- Mikali alikuwa na matarajio ambayo hayakutimia.
- Pengine Mikali alijua kuwa ataolewa ndoa ya mpango, kisiasa, lakini Mikali hakufikiri kwamba babaye mfalme atamrusha mewanamme kwa mwanaume mwingine.
- Huyu mwanamke (Mikali) aliumia na kuteseka katika mikono ya mtu ambaye angemlinda (Sauli).
- Hivyo maisha ya Mikali yakajaa uchungu juu ya wanaume wote na zaidi juu ya mabwana. Hivyo iwe ni baba, ndugu au mwanaume yeyote- Mikali alichukia!!
- Ni dhambi kubwa kuwatumia wanawake kama jinsi vitu.
- Mikali alimpenda Daudi lakini Daudi hakumpenda Mikali. Mikali hakuwa chaguzi yake ya kwanza- 1 Sam. 18:17.
- Merabu- ndiye angekuwa mke wa Daudi lakini mfalme Sauli alimpatia Adrieli kwa sababu ya fedha- 1 Sam.18:20.
- Mikali alimpenda Daudi lakini Daudi hakumpenda Mikali. Huyu ndiye mwanamke pekee aliyempenda mwanamme katika Biblia- 1 Sam.18:26-28.
- Daudi alimchukua Mikali, hakumpa Mikali chochote katika maisha.
- Mfalme Sauli babaye Mikali alimtumia bintiye kama chombo- 1 Sam. 18:20-21.
- Mfalme Sauli hakuchukua Mahari yoyote- 1 Sam. 18:25.
- Mikali aliona chuki ya babake juu ya mume wake Mikali- 1 Sam. 19:11-17.
- Daudi alimwacha Mikali kwa miaka (10-15). Wakati huo huo Daudi alichukua wanawake wengine.
- Mfalme Sauli alimpatiana Mikali kwa mwanamme mwingine- 1 Sam.25:44.
- Baada ya mfalme Sauli kufa, Daudi alidai Mikali bila kumpenda.
- Hasira ya Mikali ilipanda juu zaidi kwa sababu ya uchungu- 2 Sam. 6:20-23.
- Daudi alimchukia Mikali kabisa mpaka kifo- 2 Sam. 6:23.
- Lakini Mikali hakuwa tasa kabisa kwa maana alizaa watoto na Adrieli- 2 Sam.21:19.
MWISHO
- Kunao Mikali wengi duniani na kanisani. Hivyo waelewe na kuwasaidia, usihukumu!!
- Wanawake wengi wako na hasira na uchungu kwa jinsi wametumiwa vibaya na waume wao, baba na ndugu zao.
- Wake wengi, watoto wanakaa katika ndoa na jamii za shida, waombee. Lakini Yesu Kristo anabadilisha yote 2 Wakorintho 5:17.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO. - September 21, 2025
- GOD GUIDES OUR DESTINIES. - September 21, 2025
- GOD OF THE BREAKTHROUGHS - September 10, 2025