MFULULIZO: WASHINDWA WAKUU KATIKA BIBLIA
SOMO: WALAWI 10:1-10; WAEBRANIA 12:18-29
Leo tunatazama watu wawili waliokuwa ndugu, majina yao ni Nadabu na Abihu. Hawa ndugu wawili walipotea kwa maana hawakumchukua Mungu maanani. Hawakujali kanuni za ibada, unii na utakatifu. Hawakumwabudu Mungu katika kweli na katika Roho Mtakatifu.
Tunakutana na Nadabu na Abihu katika Kutoka 6:23- “Haruni alimwoa Elisheba binti ya Abinadabu umbu yake Nashoni naye akamzalia Nadabu na Abihu na Eliazari na Ithamari.”
Hapa twaona Nadabu na Abihu ni wanawe Haruni. Haruni naye ni ndugu yake Musa. Nadabu na Abihu pia wako na ndugu zao Eliazari na Ithamari. Jina Nadabu maanake ni “mngwana” anayeheshimika (noble). Abihu maanake ni “baba yangu ndiye.” Nadabu na Abihu walizaliwa katika utumwa wa Misri. Nadabu na Abihu walielewa sana hali ya utumwa. Hawa ndugu wawili walizaliwa mtawalia- Hesabu 3:2.
Katika kutoka 24:1-“Kisha Bwana akamwambia Musa, kweeni wewe na Haruni na Nadabu na Abihu na watu sabini na wazee wa Israeli, mkamfikilie BWANA, mkasujudie kwa mbali.”
- Wana wa Israeli walikuwa wamefika mle mlima wa Sinai. BWANA alimwamuru Musa kukwea mlima Sinai na Nadabu na Abihu walipata heshima na nafasi kubwa kusonga karibu zaidi na Mungu. Katika watu zaidi ya millioni sita, Nadabu na Abihu wamehesabika katika wa sabini na nne (74).
- Musa peke yake atamkaribia Mungu lakini wale wengine watamuona Mungu kutoka mbali- Kutoka 24:9-11.
- Hawa wote walimwona Mungu, Nadabu na Abihu walipata ile heshima ya kumwona Mungu.
- Baadaye Nadabu na Abihu walipata nafasi kubwa zaidi ya kuwa karibu zaidi kama makuhani wa Mungu- Kutoka 28:1-15.
- Nadabu na Abihu na baba yao watakuwa na mavazi ya ukuhani kwa utukufu na uzuri (dignity and honor).
- Hivyo Nadabu na Abihu wamepata kuona maajabu ya Mungu kule Misri, Bahari ya Shamu, wamepanda Mlima Sinai.
- Wamepata furaha ya kumwona Mungu.
- Lakini pamoja na nafasi kuu waliokuwa nayo katika Walawi 10:1-11, maisha yao yalipata mwelekeo mwingine.
- Hapa ni mmoja wao watu waliopata ghadgabu ya kifo kwa sababu ya kutotii Mungu.
- Baadaye kulikuwa na Kora, Dathani na Abiramu waliomwasi Musa na Mungu huko jangwani wakafa- Hesabu 16:17.
- Anania na Safira bado- Matendo 5:1-10.
- Ni jambo mbaya sana kucheza na ibada na vitu vya Bwana vilivyowekwa wakfu-iwe ni vyombo, sadaka, nyumba au mti.
Hebu tuone:-
MOTO KATIKA BIBLIA
- Moto ni ishara ya uwepo wa Mungu.
- Musa, kwanza alikutana na Mungu katika kichaka kilichowaka moto.
- Wana wa Israeli waliongozwa na guzo ya moto jangwani.
- Mle Sinai Mungu alijidhihirisha kwa wana wa Israeli katika moto.
- Madhabahu ya kwanza katika hema ya Bwana, Mungu alijidhihirisha kwa moto- Walawi 9:23.
- Mfalme Suleimani alipojenga hekalu la Mungu, Mungu alijidhihirisha kwa moto- 2 Mambo ya Nyakati 7:1.
- Wanafunzi wa Yesu Kristo siku ya Pentekoste Roho Mtakatifu alishuka kama moto juu ya kila mmoja wao- Matendo 2:2-4.
- Sodoma na Gomorrah ilichomwa na moto- Mwanzo 19.
- Siku ya mwisho dunia, mbingu zitawaka moto- 2 Petro 3:12.
- Naye Nadab na Abihu walichomwa moto kutoka kwa uwepo wa Mungu- Walawi 10:2.
MOTO WA KIGENI.
- Moto wa ‘kigeni’ si jambo mpya.
- Leo kanisani upo ‘moto wa kigeni’ kwa (doctrines), mafundisho, mazoea na mafikra.
- Nadabu na Abihu walifanya nini?
- Wakati wa ibada yao haukufaa- Walawi 16:2.
- Moto wa chetezo ulihitaji kutoka kwa madhabahu ya Bwana.
- Musa na Haruni hawakuweko- Walawi 9:8-18.
- Nadabu na Abihu walikuwa watu wa kumsaidia Musa na Haruni- Walawi 9:8, 12, 18.
- Kwa kiburi Nadabu na Abihu walienda kutoa moto wa kigeni.
- Nadabu na Abihu walitaka pia kuonyesha mavazi mapya.
Nadabu na Abihu walitumia wamlaka isiyo yao. Hawakumweleza Musa na Haruni juu ya ibada yao. Pia hawakumweleza Mungu ambaye ndiye mwenye ibada.
- Sababu ya ule moto haikujulikana- Walawi 10:33.
- Nadabu na Abihu hawakutafuta sana kumtukuza Mungu pekee katika ibada yao.
- Moto wa kigeni ni wakati ambao nia zetu si kumtukuza Mungu katika ibada zetu- 1 Wakorintho 10:3- “Basi mlapo na mnywapo au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.
- Masomo ya kujifunza.
- Tusicheze na utakatifu wa Mungu- Walawi-10:3.
- “Moto wa kigeni” haumtukuzi Mungu wa mbinguni.
- Wokovu bila msalaba ni ‘Moto wa kigeni’.
- Kuhudhuria kanisa bila ibada ni ‘Moto wa kigeni.’
- Ibada bila Roho Mtakatifu ni ‘Moto wa kigeni.’
- Ushuhuda bila ujuzi wa kibinafsi ni ‘Moto wa kigeni.’
- Kufundisha neno la Mungu bila kujiandaa ni ‘Moto wa kigeni.’
- Maombi bila roho na kweli ni ‘Moto wa kigeni.’
- Ubatizo bila maji mengi ni ‘Moto wa kigeni.’
- Meza ya Bwana bila kuzingatia na kujihoji ni ‘Moto wa kigeni.’
- Kuhubiri bila Biblia ni ‘Moto wa kigeni.’
- Moto wa kigeni unaharibiwa na moto wa Roho- Walawi 9:24; 10:2, 10:6.
MWISHO
- HAWAKUMTUKUZA MUNGU.
- Kama jinsi Musa- Kumbukumbu 32:48-51.
- Kama jinsi Nadabu na Abihu- Walawi 10:1-3.
- Kama jinsi Hophri na Phinehasi- 1 Sam. 2:12-17.
- Kama jinsi Wakorintho- 1 Wakorintho 11:29-30
- Moto wa kigeni ndani ya kanisa, ibada, nyimbo na mazoea ya maonyesho ya binafsi.
- Nadabu na Abihu walikufa, walimchezea Mungu wa Israeli.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
