MFULULIZO: JINSI YA KUFANYA VITA VYA KIROHO
SOMO: MWANZO 2:18-25
Vita vya kiroho vinapoingia katika ndoa, hiyo ndoa inaweza kugonjeka kiasi ya ndoa kufa. Leo tunataka kutizama sababu ya ndoa kugonjeka, ishara za ndoa gonjwa na jinsi ya kushinda vita juu ya ndoa yako, pia jinsi ya kuwashauri walio katika ndoa zilizo na shida- Mwanzo 2:18-25.
Ndoa ilibuniwa na Mungu mwenyewe. Ndoa ni ya zamani kuliko serikali, shule na kanisa. Ndoa ilianza na Mungu, ilikuwa ni wazo lake. Mungu ndiye aliyesherehekea ndoa ya kwanza hivyo ndoa ndio idara ya kwanza iliyoidhimishwa na Mungu mwenyewe.
Kunazo kanuni tano (5) ambazo lazima kufuata kufaulu katika ndoa la sivyo ndoa itagonjeka na kufa.
Leo hii, ndoa nyingi ziko katika shida kiasi kuvunjika. Kuna nyumba nyingi za Wakristo, mume na mke wanapigana kila siku. Washauri wa ndoa wanashangaa kwamba shida za ndoa zimeongezeka zaidi mpaka ndoa za wachungaji wa kanisa, maaskofu na wazee wa kanisa. Ndoa inaweza kuvunjika wakati wowote hata ndoa ambazo zimedumu miaka mingi.
Vijana wengi leo wanasema ikiwa ndoa ni kama ya wazazi wao, kuteta na kupigana, basi wao hawatapenda kuingia katika ndoa.
Watoto wengi wanaozaliwa leo, wanazaliwa nje ya ndoa. Wiki hii serikali ya Kenya kupitia utafiti wa (K.N.B.S) wameonyesha kwamba 37% ya jamii hapa Kenya zinaongozwa na wanawake. Jinsi wanawake wanavyopata nguvu zaidi kiuchumi na kihaki, ndivyo ndoa zinaendelea kuvunjika. Bila kuwezesha wanaume na mtoto wa kiume, jamii itapata taabu nyingi. Nguvu na mamlaka katika ndoa na jamii inategemea umri, masomo, jamii aliyezaliwa na fedha na mapato ya mme au mke.
ÌIkiwa waumini hawatasimama wima, shetani atavunja kila ndoa na jamii. Kanisa nalo haliwezi kuwa na nguvu ikiwa ndoa na jamii za waumini zimevunjika au ni gonjwa. Katika historia ya dunia na kanisa, shetani analenga sana ndoa na jamii. Hivyo, shetani, wachawi na warogi wanachukia ndoa na jamii. Hebu tuone:-
KANUNI TANO (5) ZA KUFUATA NDOA STAWI- Mwanzo 2:24
- Kanuni ya kwanza: Lazima mwanaume atamwacha mama na baba yake.
- Kama kanuni hii ya kwanza haitafuatwa, ndoa lazima kugonjeka na kufa.
- Mungu ameamrisha baada ya ndoa na Arusi, siku hio hio lazima maarusi wahame na kwenda zao kwa nyumba yao.
- Mungu hajaruhusu kukaa katika nyumba moja na wazazi tunapofunga ndoa.
- Haijalishi upendo na nguvu za jamii, mume lazima kuacha baba na mama yake baada ya arusi na ndoa.
- Kanuni ya pili: Kuambatana na mkewe- Mwanzo 2:24.
- Mume na mke wanahitaji kuishi pamoja katika nyumba moja.
- Mambo ya kuishi mbali mbali ni kuvunja msingi wa ndoa.
- Kuishi mbali na mke kunaleta ugonjwa wa ndoa.
- Chochote kinachotenganisha mme na mke wake, iwe ni kazi au masomo, kinahitaji kukataliwa.
- Kanuni ya tatu: Mwili mmoja- Mwanzo 2:24.
- Mwili mmoja ni mme mmoja na mke mmoja.
- Hakuna mme au mke anayeweza kumpenda mwingine. Tumepewa upendo wa mke mmoja au mme mmoja.
- Hakuna anayeweza kuambatana na zaidi ya mmoja.
- Wake zaidi ya mmoja haukuwa mpango wa Mungu. (Polygamy) series or retaination.
- Musa aliruhusu mke zaidi ya mmoja kwa sababu ya ugumu wa mioyo- Mathayo 19:5-8.
- Kanuni ya nne: Umoja na urafiki wa karibu- Mwanzo 2:25.
- Lazima ndoa iwe na umoja na urafiki wa karibu sana.
- Kusiwe na siri kati ya mme na mke.
- Ndoa ni kushiriki karibu kila kitu, hata hewa.
- Kanuni ya tano: Utawala na mamlaka katika ndoa- Waefeso 5:23.
- Utawala katika ndoa, mme ndiye kichwa cha nyumba kama vile Yesu Kristo ndiye kichwa cha kanisa.
- Mke ni msaidizi anayefaa, mke a anasaidia tu, kazi ya mme ni kila kazi (Division of labour).
ISHARA ZA NDOA GONJWA
- Kukosa umoja na furaha.
- Kuhukumiana na kuteta, kuingiliwa na watu wa jamii.
- Kukosa uwezo wa kutatua shida za nyumbani pasipo watu wa nje kuingilia ndoa yao.
- Wakati mme na mke hawawezi kuzungumza wao kwa wao, kuishi mbali mbali.
- Wakati mme na mke wanakataana tendo la ndoa, au tendo la ndoa inapofanywa kinyume cha asili.
NJIA YA KUSAIDIKA
- Mme na mke kujisalimisha kwa Yesu Kristo.
- Kurudia madhabahu ya maombi kama jamii moja.
- Kutatua shida ya jamii siku ile ile shida imetokea.
- Kubali makosa, omba msamaha, vumilia ndoa.
MAOMBI
- Kila maovu yanayopigana na ndoa yangu, shindwa katika jina la Yesu Kristo.
- Ee Bwana, ingilia kati ya ndoa na jamii yangu katika jina la Yesu Kristo.
- Ninaomba ukombozi wa ndoa yangu katika jina la Yesu Kristo.
- Kila roho wa kuvunja jamii yangu ninakukemea katika jina la Yesu Kristo.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
