MFULULIZO: PASAKA
SOMO: YOHANA 12:9-19
Yesu Kristo alianza safari ya kwenda msalabani kwa kuingia Yerusalemu. Njia hii ya kwenda msalabani ilikuwa ni njia ya huzunu na mateso mengi lakini Yesu Kristo alichagua kuipitia njia hiyo. Watu wengi walimlaki Kristo, huku wakitoa mavazi yao na kutandaza matawi ya mitende. Waliimba wimbo wa Hosana, hosanna “tuokoe sasa.” Unabii wa Zakaria 9:9, ulitimia siku hii ya Jumapili ya mitende, miaka 2000 iliyopita. Hebu tujifunze:-
NJIA YA KWENDA MSALABANI ILIKUWA NJIA YA HATIMA-Yohana 12:12-13.
Yesu Kristo alikuja duniani kuokoa sasa wakati huo ulifika.
- 13, Neno “Hosana” Maanake ni “okoa sasa.”
- Watu wote walikuwa tayari kwa ukombozi.
- Yesu Kristo alikuja kuokoa watu na dhambi zao-lakini watu walitarajia ukombozi wa kisiasa, ukombozi kutoka kwa utawala wa Roma.
Watu waliamini sana Yesu Kristo alitoka kwa Mungu.
- Yesu Kristo alikuwa chaguo la wote kuwa “masihi” alitimiza yote ya unabii-Zakaria 9:9
NJIA YA KWENDA MSALABANI ILIKUWA NJIA YA KUJITOA-Yohana 12:14-15.
Kule kuingia Yerusalemu kulitangaza kujitoa kwake kwa kazi iliyokuwa mbele zake Mwokozi.
- Lakini safari ya kwenda msalabani haikuanza mle Bethania, safari hii ilianza milele.
- Safari hii ya kwenda msalabani ilianza Edeni, wazazi wetu walipofanya dhambi ya kwanza.
- Katika milele hata kabla kuumbwa kwa mbingu na nchi.
- Safari ya Yesu Kristo kutuokoa ilianza milele.
Kuja kwake Yesu Kristo duniani kulikuwa ni kujitoa kwake kwa Baba yake.
- Watu walihitaji mfalme sana, kiasi walitaka sana kumlazimisha Yesu Kristo kuwa mfalme wao.
- Watu hawa hawakutaka ukombozi kutoka dhambi lakini ukombozi kutoka kwa utumwa wa Roma.
- Watu hawa hawakutaka kufanya mapenzi ya Mungu lakini ushindi juu ya Roma.
- Watu walishangaa badala ya Yesu kuingia Yerusalemu juu ya farasi ya vita, aliingia Yerusalemu juu ya punda, ishara ya amani-Marko 10:45.
NJIA YA KWENDA MSALABANI ILIKUWA NJIA YA UVUMBUZI-Yohana 12:16
Watu hawa walitambua kwamba mawazo yao juu ya masihi yalikuwa makosa.
- Walimsalimia Kristo kama mfalme wao, lakini hawakutambua ufalme wake ulikuwa ufalme gani.
- Hawakuelewa ufalme wa Kristo juu ya maisha yao.
Wanafunzi wa Yesu Kristo na wao walitambua mpango wa Mungu kwa ulimwengu.
- Wanafunzi wa Yesu Kristo hawakutambua jinsi ya kazi na shabaha ya Yesu Kristo mpaka kufufuka kwake.
NJIA YA KWENDA MSALABANI ILIKUWA NJIA YA UKOMBOZI-Yohana 12:17-19.
- Njia aliyochukua Yesu Kristo ilikuwa njia ya wokovu kwa watu wote.
- Yesu Kristo alijua kwamba ni lazima kufa ili wote wapate uzima wa milele.
- Hii ilikuwa njia ya ukombozi ambayo shetani hangeweza kuzuia.
- Watu wote walijitokeza kumpokea Yesu Kristo Yerusalemu kwa ushindi mwingi zaidi.
MWISHO
- Jumapili ya mitende ilikuwa ushindi mkuu kwa maana Yesu Kristo alikuwa anaenda msalabani kwa ajili yetu.
- Hakuna mtu, au shetani aliyeweza kumzuia Kristo kwenda msalabani.
- Yesu Kristo alikuja duniani kutufia, tupate kuokoka.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
