Swahili Service

NYAKATI ZA UFALME WA MATAIFA

MFULULIZO: DANIELI-MUNGU NDIYE HAKIMU.

SOMO: DANIELI 2:31-49

 

Leo tunatazama unabii aliouona mfalme Nebukadreza katika ndoto ya yule sanamu. Nebukadreza aliota ndoto iliyomsumbua maisha yake.

Kitabu cha Danieli ni msingi ya unabii wa Biblia. Ufunuo ni tafsiri ya ule unabii. Leo tunatazama historia na Biblia kuonyesha jinsi Biblia ni kitabu cha ajabu-Danieli 2:31. Mfalme Nebukadreza alistaajabu sana kijana Danieli alipoeleza ile ndoto yake. Danieli 2:36-38, ndiyo maana yake ile ndoto ya mfalme Nebukadreza. Nebukadreza alipendezwa kwamba katika ile tafsiri yeye ndiye “dhahabu” Danieli 2:39-45, baada ya falme hizo, Mungu wa mbinguni ataweka ufalme usioweza kuaribika, ufalme usioweza kumilikiwa na watu, ufalme wa milele.

FALME ZA WATU WA MATAIFA.

  • Sanamu ile inaonyesha historia ya ulimwengu huu, lakini Danieli alipoandika unabii huu miaka 2,600 iliyopita huu ulikuwa unabii. Hivyo unabii ni historia katika kurudi nyuma (reverse).
  • Katika historia ya ullimwengu huu, Yesu Kristo alitufundisha kwamba kutakuwa na kipindi kirefu za falme za mataifa ambazo pia zitatawala taifa la Israeli-Luka 21:24.
  • Nyakati za mataifa zilianza na ufalme wa Babeli chini yake mfalme Nebukadreza mpaka ufalme wa Roma, mpaka mwaka 1967, wakati Wayahudi walioteka mji wa Yerusalemu na kufanya Yerusalemu mji mkuu wa Israeli.
  • Hebu tuone falme zilizo akilishwa na ile sanamu katika ndoto yake mfalme Nebukadreza.
  1. Huu ulikuwa ufalme wa Babeli chini ya Nebukadreza na milki yake.
  • Nebukadreza alipendezwa sana kujua kwamba enzi yake ndiyo dhahabu.
  • Baadaye Nebukadreza alijenga sanamu kubwa ya dhahabu.
  • Pamoja na kuelewa na ule unabii Nebukadreza alifikiri ufalme wake ni wa kudumu milele.
  • Danieli alimjulisha kwamba ufalme wa dunia hii ni kwa muda tu.
  1. Fedha-Medo-Uajemi (539-331 BC).
  • Katika mwaka wa 539BC kabla kuzaliwa kwa Yesu Kristo, Cyrus mkuu alichukua ule ufalme wa Babeli.
  • Ufalme wa Medo-Uajeni ulitawala dunia kwa miaka 200.
  • Kitabu cha Esta kiliandikwa wakati huu wa Uajeni.
  • Nabii Nehemia alitumika wakati huu, nabii Danieli alikuwa bado hai.
  1. Shaba-Wagiriki (331-146BC).
  • Baada ya nyakati za Uajeni, Wagiriki walipewa ufalme wa dunia yote.
  • Mfalme wa kwanza wa enzi ya Ugiriki alikuwa Alexander the Great.
  • Alexander the Great alishinda vita dunia yote akiwa miaka 30.
  • Alexander alilia kwa kukosa mahali pa kuendelea na vita duniani.
  • Majeshi ya Ugiriki walivaa chepeo ya shaba na pia ngao za shaba.
  • Mpaka hivi leo dunia ingali inatumia elimu na tamaduni za Wagiriki.
  • Hippocrates baba wa dawa na matibabu aliishi wakati huu wa enzi za Wagiriki.
  • Wanaphilosophia wakuu duniani walikuwa Wagiriki-Aristotle, Socrates na Plato waliishi siku za enzi za Wagiriki duniani.
  1. Chuma-Roma (146BC-400 AD).
  • Katika ile sanamu ndoto ya mfalme Nebukadreza miguu zilikuwa za chuma.
  • Roma iliposhinda vita vyake juu ya Carthage mwaka 146BC, ndiyo Roma ilichukua mamlaka kutoka Wagiriki.
  • Kwa miaka 500 Warumi walitawala dunia yote.
  • Kama jinsi chuma inao nguvu zaidi kuliko dhahabu, fedha na shaba, ufalme wa Roma ulikuwa na nguvu nyingi zaidi ya wote mbele yake.
  • Warumi walichangia katika mambo mengi duniani mpaka leo.
  • Barabara, jeshi, amani ya dunia, majengo, siasi, serikali na usimamizi wa nchi, Demokrasia, hesabu na philosophia.
  • Kilimo na mbinu za ukulima tunazotumia mpaka leo zilitoka Roma.
  • Roma ilijenga 52,000 maili ya barabara lami (85,000), Amerika=(46,000 maili) 56,000 km, baada ye miaka 2,500.
  • Barabara zilizojengwa na Warumi miaka 2,500 bado zinatumika leo.
  • Miguu miwili inaonyesha falme mbili Magaribi-Roma na Constantinople (Istabul) Mashariki.
  1. Chuma na udongo-U.N-Umoja wa mataifa.
  • Nchi za kwanza (tajiri) na nchi za tatu (maskini).
  • Enzi ya sasa ni enzi ya chuma na udongo.
  • Baadaye hivi karibuni Europa itajiunga mataifa 10 kulingana na Ufunuo.
  • Katika Mathayo 24, Yesu Kristo aliweka nguvu unabii wa Danieli.
  • Enzi hizi zote ni za utawala wa watu wa mataifa.
  • Hivi karibuni jiwe lilikatwa mlimani bila mkono wa mwanadamu itafanyika na jiwe hilo litakuwa ufalme wa Mungu wetu. Ufalme wa Yesu Kristo utakuwa wa milele na milele.

UFALME WA MUNGU

  1. Ufalme wa Yesu Kristo leo ni ufalme wa kiroho.
  • Yohana Mbatizaji alihubiri “Tubuni kwa maana ufalme wa Mungu umekuja.”
  • Yesu Kristo alipokuja duniani alianza ufalme wa Mungu.
  • Ufalme wa Mungu uko ndani yenu au pamoja nasi-Luka 17.
  • Ufalme wa Mungu, ufalme wa mbinguni ni “Mtu”-Mathayo 6:33; Warumi 14:17.
  1. Ufalme wa Yesu Kristo unaokuja utakuwa ufalme halisi.
  • Kristo atakaporudi duniani ataleta ufalme wa miaka 1,000. Baada ya miaka 1,000 ya ufalme hapa duniani kutakuwa na dunia mpya, mbingu mpya, Yerusalemu mpya, Mungu atatawala milele na milele.
  • Hapatakuwa dhambi tena, shetani na mwenye dhambi tena-Marko 14:25.
  • Yesu ndiye lile jiwe lililokatwa mlimani bila mkono. Ufalme wa Yesu Kristo hautakuwa na mwisho-Ufunuo 20.
  • Falme zote za mwanadamu zitakwisha na ufalme wa Mungu pekee utadumu milele na milele.

YESU KRISTO NDIYE

  1. Yesu Kristo ndiye mwamba wa wokovu.
  • Danieli anaposema jiwe lilikatwa mlimani bila mikono ya mwanadamu, Maanake ni kwamba Yesu Kristo ndiye Mungu mwenyewe.
  • Yesu ni mwamba wenye imara na salama.
  • Yesu Kristo ndiye “Jiwe la pembeni”-Matendo 4:11-12.
  1. Yesu Kristo ndiye mwamba wa nguvu.
  • Jiwe hilo lililokatwa mlimani bila mkono, lilitupwa kwa miguu na nyayo za lile sanamu.
  • Kwa nguvu zake ile sanamu ilianguka na kusaga ile sanamu mpaka vumbi.
  • Yesu Kristo atakapokuja tena duniani atayapiga mataifa, utawala wa falme zote. Chochote kilichojengwa na mikono ya mwanadamu kitang’olewa na kutupwa-Ufunuo 17:12-14.
  1. Yesu Kristo ndiye jiwe kuu la mamlaka-Danieli 2:44.
  • Yesu Kristo ni jiwe linalopiga kwa haraka sana mambo yote ya mwanadamu.
  • Mungu wa mbinguni atavunja-vunja chochote mwanadamu amejenga katika historia.
  • Maendeleo yote ya dunia hii itakuwa mavumbi na kuchukuliwa na upepo-Isaya 2:2-4.
  • Charles Wesley alitunga wimbo kuonyesha jinsi ufalme wa Yesu Kristo duniani utakavyokua, “Jua kila ling’arapo.”

MWISHO

  • Je, katika falme hizi mbili ni ufalme gani wewe utatumia pesa na wakati wako?
  • Baada ya maisha haya duniani, tutaishia katika shimo ya 6x6x4.
  • Tulio na Mwokozi Yesu Kristo tutaishi milele na milele katika ufalme wake.
  • Je, umejengwa maisha yako juu ya mwamba imara-Yesu Kristo?
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *