MFULULIZO: TUMAINI HAI.
SOMO: 1 PETRO 3:8-12, (10).
Kila mtu anapenda kuishi maisha bora zaidi. Sijakutana na mtu yeyote asiyependa kuishi vyema na bora. Kila mtu anapenda kuwa na furaha, amani, baraka na ufanisi-maisha mema.
Lakini shida ni watu katika dunia hii hawajui maisha mazuri na bora na maisha ya namna gani. Wengine maisha mazuri ni kuwa na pesa, wengine ni kuwa na uwezo wa kusafiri nchi za mbali na kuona ulimwengu wote. Kadhalika kwa wengine ni kujulikana na kila mtu (popularity), maisha ya sifa pia, wengine maisha mema ni kuishi kwa utulivu na amani.
Ukweli wa mambo ni kwamba maisha yanaleta siku njema na siku zisizo njema. Leo nataka kukupa kifunguo cha maisha mema na bora katika dunia hii ya shida na maangaikoi yanayokuzingira pande zote-1 Petro 3:8-12.
Petro anawaandikia Wakristo waliotawanyika pote, kwa sababu ya dhiki na mateso yasioletwa na amani yao katika Yesu Kristo. Kaisari Nero aliamura kuwatesa Wakristo. Wakristo hawa walikuwa katika dhiki nyingi sana. Pamoja na shida na dhiki, Petro anawaandikia jinsi ya kuishi, Kuishi maisha mema kwa kupenda maisha yao. Kama utapenda maisha mema basi utahitaji kufanya yafuatayo:-
UWE NA MTAZAMO MZURI (Attitude).
- Maisha mema ni swala la mtazamo, wala si mali na pesa nyingi, lakini mtazamo katika hali tatu ya uhusiano-Mahali pa kazi, serikali na nyumbani na zaidi katika ndoa.
Nia moja-V. 8.
- Uhusiano mwema ndio kifunguo cha maisha mema.
- Kitu ngumu zaidi katika maisha ni kudumisha uhusiano.
- Mahali palipo na zaidi ya watu wawili panao uhusiano.
- Palipo na watu zaidi ya mmoja ni lazima pawe na mafikira tofauti na mafikra tofauti yanaleta farakano.
- Uhusiano mwema ni kuwa na nia moja, kuhurumiana na kupendana kama ndugu na kunyenyekeana.
- Je, tupate wapi mfano wa nia moja? Yesu Kristo alikuja duniani kuwapatanisha wanadamu na Mungu wao.
- Yesu Kristo ndiye kielelezo chema cha upendo, huruma, fadhili na unyenyekevu.
- Unapokuwa na msimamo dhabiti katika Yesu Kristo ndiposa utakuwa na uhusiano mwema na watu.
- Hivyo uhusiano mwema na watu wote unategemea jinsi uhusiano wako na Yesu Kristo ulivyo.
- Maisha mema ndio lengo la kizazi chetu. Kila mtu anatazamia maisha mema.
- Michael Jackson alikuwa muimbaji hodari sana hata katika kifo nyimbo za Jackson zimenoga duniani. Watu wengi wangependa kuwa Jackson, lakini Jackson alikufa kwa kula madawa ya kulevya zaidi.
- Kwa dunia hii maisha mema ni kuishi maisha ya dhambi.
- Mbele ya macho ya dunia hii mfalme Sulemani aliishi maisha mema.
- Mfalme Sulemani alikuwa na pesa, dhahabu, uwezo, anasa na wanawake-lakini yeye alisema “Nimechukia maisha-Mhubiri 2:17.
- Kulingana na mfalme Sulemani, maisha mema sio elimu-Mhubiri 1:13.
- Maisha mema sio hekima, ufahamu na uhodari-Mhubiri 1:16-17.
- Maisha mema sio kufanya mambo makuu-Mhubiri 1:14.
- Maisha mema sio raha na anasa-Mhubiri 2:2-6.
- Maisha mema sio mali na vitu na miradi mikubwa-Mhubiri 2:4-6.
- Mfalme Sulemani alituandikia shairi la huzuni-Mhubiri 4:2-3.
- Hivyo tuwe na nia nzuri na uhusiano mwema na serikali-1 Petro 2:13-15, waajiri 2:18-21 na katika ndoa 1 Petro 3:1-7.
UWE NA MWITIKIO MWEMA (RESPONSE)-USILIPIZE KISASI-1 Petro 3:9.
- Usilipe mabaya kwa mabaya.
- Ikiwa mtaishi maisha mema, basi sitalipiza mabaya kwa mabaya na lawama kwa lawama.
- Ukitendewa mabaya usilipe mabaya-Mungu ndiye mwenye kulipa.
- Uwe kama Yesu Kristo-1 Petro 2:21, 23.
- Maisha mema ni jinsi unavyowaitikia wengine, yaani jibu lako.
UWE NA KIWANGO (STANDARD) KIPIMO CHEMA-1 Petro 3:10-11.
- Pima sana ulimi wako, dhibiti ulimi na maneno yako-Zaburi 141:3.
- Mtu atakaye ishi maisha mema ni yule anatawala ulimi wake.
- Screw inayolegea haraka katika kichwa cha watu ni ile ya ulimi.
- Kijana mmoja alienda shule ya mwana philosophia Socretes ili ajifunze kunena (aratory). Socrates alimlipisha karo mara dufu. Alipouliza kwa nini, Socrates alimjibu, “Kijana inapasa nikufundishe science mbili, moja kunena, pili kunyamaza.”
- Ikiwa unapenda maisha mema, jifundishe jinsi ya kudhibiti ulimi wako.
- Acha mabaya.
- Tenda mema.
- Tafuta amani.
- Fuata sana amani.
- Badala ya kulipiza kisasi bariki, hurumia, tafuta amani-Mathayo 5:9.
- Wapimie watu Yesu Kristo katika kila ubaya wametenda-Warumi 14:17; 2 Timotheo 2:22; Warumi 12:18; Warumi 14:19; 2 Wakorintho 13:11.
- Watu watakao ishi maisha mema ni wale wana mtazamo mwema, mwitikio mwema na kipimo chema.
UWE NA MOTISHA MWEMA (RIGHT INCENTIVE)-1 Petro 3:12.
- Petro anatukumbusha jinsi ya kuwa na motisha nzuri kwa sababu macho ya Mungu yanatazama.
- Mungu anatazama kujibu maombi yetu.
- Mungu yuko tayari kukutana na mahitaji yako yote ikiwa utakuwa na mtazamo mwema, mwitikio mwema, kipimo chema na motisha njema.
MWISHO
- Tunaishi katika dunia mbaya sana.
- Watu kwa kawaida hawakutakii mema.
- Lakini Mungu anayaona yote na yuko tayari kuyajibu maombi yako.
- Basi, wewe nawe uwe na mtazamo mwema, mwitikio mwema, kiwango chema na motisha njema (Good attitude, response, standard and incentive).
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
- UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI. - October 19, 2025
- THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR. - October 19, 2025
