MFULILIZO: MUNGU NI PENDO
SOMO: MALAKI 4
Tangu dunia hii kuumbwa kumekuwa na siku ya hukumu ya Mungu juu ya watu wake na mataifa ya ulimwengu. Lakini kuna siku ya hukumu ya mwisho. Siku hio inaitwa “siku ya Bwana” siku hio inakuwa mwanzo wa hukumu, kilio na kuomboleza kwa wote wasio okoka. Katika vita vya dunia vya pili (WW II) majeshi ya pamoja na muungano (Allied forces) walifahamia sehemu mbalimbali za juropa, lakini tarehe 6 Juni 1944 iliitwa siku ya vita kali yaani (D-Day).
- Siku hio historia itafika kikomo chake
- Serikali zote za dunia na system za ulimwengu zitamalizika kabisa!
- Yesu Kristo ataazisha ufamle wake duniani kama mfalme wa wafalme na Bwana wa Mabwana.
- Waliookoka watahukumiwa mbele ya kiti kikubwa cheupe cha hukumu (the great white throne judgement)
- Siku ya hukumu itakuwa mwanzo wa kilio, kuomboleza na shida kwa wote wasiookoka.
- Biblia inafundisha juu ya enzi tatu ambazo zinaitwa siku ya Bwana
- Siku ya dhambi na shitaka moyoni – siku zote mbele ya Yesu Kristo kuzaliwa duniani (the day of guilt)
- Siku ya Neema – siku tangu kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo (the day of Grace)
- Siku ya Bwana – siku yaja ya kutamatisha siku hii ya Neema (the day of the Lord) Malaki4:1-2)
Neno la Malaki linapinga mafundisho ya:-
- Universalism – “sisi zote twaenda mbinguni (we are all going to heaven)
- Liberalism – “hakuna jihanamu wala mbinguni” no hell no heaven.
- Humanism – “mwanadamu anaweza kujimudu mwenyewe na kujikamilisha mwenyewe” human kind can perfect themselves,” utu na Ubuntu
- Atheism – hakuna Mungu, “hakuna maisha baada ya kifo” no God or after life”
- Lakini si kila mtu anaenda mbinguni, Jihanamu ipo
- Hakuna mtu yeyote anaweza kwenda mbinguni kwa nguvu zake mwenyewe.
- Biblia inafundisha kwamba kuna hali ya milele kwa kila mwanadamu (the final state of humanity)
- Malaki na Ufunuo wanatueleza kwamba kuna hukumu kwa wenye dhambi wote na kuna Baraka kwa wenye haki, wanao mtumkia Mungu na wasio mtumkia (Malaki 3:18)
- Katika Malaki 4:2 tunajifunza kweli tatu juu ya siku ya Bwana, siku ya kutisha sana:-
I. NI SIKU YA USONI, (It is Future Day)
- Katika karne zilizopita, kumekuwa ni siku na nyakati mbaya duniani hii ya dhambi.
- Nyakati za Nuhu, Mungu alituma gharika wanadamu wote wakafa isipokuwa watu 8
- Ilikuwa siku ya hukumu huko Sodomo na Gomora
- Babeli, ufalme mkuu zaidi ulianguka Mungu alipowaandikia “Mene Mene Tekeli na Persi”
- Israeli waliangamizwa wakati Kaisari wa Roma alituma majeshi ya Roma juu ya Israeli mwaka wa 70AD
- Ilikuwa ni siku mbaya wakati Europa (Europe) walikufa kwa ugonjwa bubonic plague, watu millioni 30 wakafa”
- Ilikuwa siku mbaya katika vita vya ulimwengu vya kwanza na vya pili (WWI na WWII)
- Ilikuwa siku za hukumu korea, vietman, Iraq, Afghanistan na katika vita vya sasa War on Terrorism
- Dunia hii imeona siku za taabu na giza kuu, lakini siku yaja, juu ya wote wasiokoka.
- Malaki alipoona siku hio anasema mara mbili katika 4:1 “tazama siku inakuja” Malaki anasema hio siku inakuja upesi.
- Siku ya Bwana yakaribia – kila kuchao hio siku yakaribia
- Je, utakuwa wapi siku hio? Hakutakuwa na mahali pa kujificha, hakuna rushwa.
- Mahali pakujificha na salama na ulinzi itakuwa dani ya mtu – Yesu Kristo (Warumi 8:1)
II. ITAKUWA SIKU YA KUONGOFYA SANA
- Malaki anaeleza kwa njia mbili juu ya uaribifu wa siku hio (Malaki 3:2)
- Siku hio itakuwa kama jiko la moto (oven)
- Siku hio itakuwa kama moto unao choma kichaka
- Lakini katika moto wa Mungu hata mizizi ya miti itachomeka, hivyo hakuna kumea tena
(Isaya 10:16, 30:27, Yeremia 21:11-14, Yoeli 2:1-3, Sefania 1:14-18)
- Yesu Kristo naye alisema juu ya moto usioweza kuzimika (Marko 9:43-48)
- Kristo alitufundisha juu ya tajiri moja aliyeenda Jehanamu (Luka 16:24)
- Mtume Paulo alisema juu ya moto (II Wathesa 1:7-8)
- Yohana aliona siku hio (Ufunuo 8:7-8) ufunuo 13:13, 20:9, 21:8
- Jehanamu ni mahali
- Mahali pa kuchomeka milele na kutengana na Mungu milele, mahali pa upweke
- Je, utakuwa wapi siku hio?
III. ITAKUWA SIKU YA MWISHO
- Siku hio inachoma mizizi na matawi.
- Mizizi ndio chanzo, kuzaliwa, matawi inaonyesha siku za mbele (root – origin, branches – future)
- Mungu anapoharibu mizizi ya mtu, maanake ni kumaliza historia, urithi na kizazi cha mtu
- Katika ziwa la moto, hakuna kumbu kumbu, urithi, ukumbusho.
- Jehanamu hakuna cha kukumbuka (no past, nothing to draw satisfaction)
- Matawi niyakuzaa matunda, watu wanapomkataa Kristo na injili yake, wanakatwa na kutupwa
- Jihanamu hamna future na tumaini.
- Dante – Abandon all hope, ye who enter here”
- Ni nani ataingia katika hukumu hii?
- Malaki anaeleza “ni wenye kiburi na kila anayetenda maovu”
- Wenye kiburi ni wale wanaochemka na sifa zao “to boil over”
- Watendao maovu ni wale “wanafanya kazi ya kujinufaisha kupitia kwa uovu na kwa njia zizizo za haki.
MWISHO
- Kama huna Yesu Kristo, wewe ni moja wao, waendao motoni
- Leo geuka maisha yako, muelekee Yesu Kristo kwa kutubu dhambi zako.
- Kuna uzima tele katika jina la Yesu Kristo – liite jina lake leo.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
