SOMO: ZABURI 29:11
UTANGULIZI
Amani timilifu, Amani ya ndani inapatikana katika ushirika na Mungu. Uhuru wa kweli wakati wote kutoka na kila shida ya kiroho na mwili hutoka kwa Mungu pekee. Zaburi 29:11- “Bwana Atawapa Watu Wake Nguvu; Bwana Atawabariki Watu Wake Kwa Amani”.
Ndoa nyingi, nyumba nyingi na mahali pa kazi pamekuwa uwanja wa vita kwa watu wengi sana. Hali ya fedha imezorota kwa wengi na watu wengi wanaishi katika deni. Mataifa mengi yanatafuta Amani na vita 53 zaendelea duniani hivi leo.
Lakini Bwana asema hivi— “Bwana atawapa watu wake nguvu, Bwana atawabariki watu wake kwa Amani”
Hebu Tujiifunze:-
I. AMANI YA KWELI HUTOKA KWA MUNGU (Isaya 26:3)
- Wakristo wengi hawajui jinsi ya kudai ahadi hii ya Amani (Zaburi 29:11)
- Amani inatengemea uhusiano wetu na Mungu.
- Immanuel Kant (Mwana philosophia) alisema “Amani si ukosefu wa vita, wala matisho ya vita, lakini Amani ni hukosefu wa matisho ya vita”
- Kuwa salama si kusema Amani hipo, lakini ikiwa adui yetu angalipo basi Amani bado.
- Hivyo hamna Amani wakati shetani angalipo na wakati wowote anaweza kutushambulia.
- Hivyo kila siku na kila saa lazima tukukesha na kuomba.
- Hivyo Amani inapatikana katika kuwa tayari kwa vita.
- Kufanya mkataba na waovu, na wagaga na shetani hakuleti Amani.
- Shetani hana huruma kamwe.
- “Amani ina patikana katika kujitayarisha vita (J.F. Kennedy )
- Kuwa tayari kwa vita ni pamoja na kujifundisha vita. Katika vita vya kiroho ni lazima kujifundisha vita.
II. VITA VYA KIROHO VINAENDELEA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.
- Dunia hii ni uwanda wa vita kuu na kaburi ni uwanda wa mabaki ya vita hivi.
- Lakini hata ingawa, tuna pata Amani katika kujifanya tayari kwa vita, ni lazima kuchangua vita vyetu vizuri.
- Daudi alikataa vita na ndungu yake Elihu kwa sababu Adui alikuwa Goliathi (I Samweli 17)
- Hivyo Mungu apate kutufungua macho kuchangua vita vyetu vyema.
- Wasio haki wanakosesha wateule Amani (Isaka alidharauliwa na Ishimaeli)
- Wasio haki huwatesa wateule kama vile wana wa Israeli mle Misri. (Zaburi 125:3, Isaya 43:2)
III. MATESO YA WATEULE YAKO NA KIKOMO CHAKE (Zab.125:3)
- Wateule wanaishi milele lakini shida zao zina kikomo.
- Wasio haki hawawezi kudhulumu hatima ya wenye haki milele.
- Mungu alipanga kwamba Muisraeli aliye na hatia asipigwe zaidi ya mara 40. (Kumbukumbu 25:3)
- Hivyo ni wakati wako kutoka kwa shida yako hivi leo (Mathayo 24:22)
- Adui zetu wamepangiwa wakati wao (Waamuzi 3:1)
- Adui mkuu wa Amani yetu ni dhambi.
- Silaha kuu yetu ni Maombi, hivyo ushindi wetu hukaribu.
MWISHO
- Wewe nyumba ya vita inayo pigana na Amani yangu , Shindwa sasa katika Jina la Yesu Kristo
- Kila nguvu ya adui juu ya Amani na Furaha yangu shindwa katika Jina La Yesu Kristo
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- CHRISTMAS: THE BIRTH THAT BROKE EVERY BONDAGE - December 25, 2025
- CHRISTMAS: WHY DID CHRIST COME? - December 24, 2025
- KRISMASI MAANAKE NI FURAHA KWA DUNIA YA DHIKI NA SHIDA - December 21, 2025
