Swahili Service

TAFUTA KUTEMBELEWA NA MUNGU

SOMO: LUKA 1:26-38

 

Mungu anaweza kuwatembelea watu wake kibinafsi au kiwingi. Mungu anaweza kuwatembelea watu wake moja kwa moja au kwa njia nyingine ile.

Kutembelewa na Mungu ni baraka. Watu wa Mungu wanahitaji kujiweka katika hali na mahali wanaweza kutembelewa na Mungu.

Mungu anapokutembelea, kila jambo ndani ya maisha yako yanabadilika kabisa kwa wema wako. Mungu anapotembelea mtu, ahadi zake za kale na unabii unatimia.

Kila tembeleo la Mungu linaleta maonyesho ajabu ajabu. Mungu anapotutembelea, mambo makuu, ishara, maajabu na miujiza yake inafanyika mara moja.

Jambo la busara zaidi ambalo lingetendeka kwa yeyote, ni kutembelewa na Mungu.

Kutembelewa na Mungu kama jamii, binafsi, taifa au kanisa linahitaji kuwa jambo la kawaida kwetu.

Hebu tutazame:-

NJIA ZA MUNGU KUTEMBELEA WATU

  • Omba sana Mungu akutembelee kila mara katika eneo zote za maisha, kiroho, uchumi, ndoa, jamii, masomo na kila eneo unaohitaji kutembelewa leo na kila mara.
  1. Kuondolewa utasa na ahadi zake kutimizwa ndani ya maisha yako- Mwanzo 21:1.
  • Kutembelewa na Mungu kulimaliza kabisa utasa katika maisha ya Sara.
  • Kwa kutembelewa na Mungu Sara alivunjwa utasa.
  • Ahadi za Mungu zilitimia na Isaka akazaliwa.
  1. Mungu alipotembelea wana wa Israeli katika utumwa wao Misri, Mungu aliona mateso na kilio chao- Kutoka 4:32.
  • Kwa kutembelewa na Mungu utumwa wa Misri ulivunjika.
  • Walitambua Mungu hajawaacha, walipomlilia Mungu, Mungu alishuka kwao na kuwakomboa.
  • Haijalishi mateso na dhiki tuliopitia chini ya adui zetu, tunapokea ukombozi, Mungu anapotembea kwa nguvu zake.
  1. Kuondolewa njaa na ukosefu- Ruthu 1:6.
  • Kutembelewa na Mungu kulisimamisha njaa, tauni na janga za wakati mrefu zaidi.
  • Wema wa Mungu ulishuhudiwa mbali kwamba Mungu amewatembelea watu wake na kuwapa chakula.
  • Mungu anaouwezo wa kutembelea binafsi, jamii, taifa na kuwaondolea kila hali ya njaa, janga za ukosefu na kuwapa watu wake mavuno- 2 Wafalme 7:1-2.
  1. Urejesho kupitia nguvu za Mungu matokeo yake uponyaji na miujiza- Matendo 3:1-11.
  • Kiwete aliyekaa mlango wa Hekalu Yerusalemu kwa miaka mingi, alitembelewa na Mungu.
  • Miujiza, ishara na maajabu yanawezekana. Uponyaji wa kila hali ya magonjwa, ukombozi kutokana na dhiki zote, urejesho wa Mungu kuonekana.
  1. Kutembelewa kuliko juu zaidi ni kuokolewa- Luka 1:68, 78.
  • Zakaria alielewa kwamba Mungu alipowatembelea watu wake ni pamoja na kuokoa nafsi zao.
  • Panapo wokovu, panao kutembelewa na Mungu- Matendo 9:1-10.
  • Tunahitaji kumtumaini Mungu kutembelea Athi- River kama vile alivyofanya mle Samaria- Mtendo 8:1-10. Watu binafsi kuokoka kama vile Towashi wa Ethiopia au kutembelewa kama jamii kama jinsi Kornelio- Matendo 11:1-12.
  1. Roho Mtakatifu aliposhuka Yerusalemu siku ya Pentekoste, ilikuwa ni Mungu kutembelea watu wake- Matendo 3:19.
  • Mungu anapo tutembelea tunapata kujazwa Roho Mtakatifu na miujiza kufuata kila tuendako- Marko 16:16-17.

JINSI YA KUJIWEKA TAYARI KUTEMBELEWA NA MUNGU

  • Mungu anapotembelea mtu au watu si kwa sababu tunastahili, lakini ni kwa neema na kwa jukwaa ya damu ya Yesu Kristo.
  • Hatustahili kutembelewa lakini tunaweza kujiweka katika hali ya kutembelewa kwa njia zifuatazo:-
  1. Kumsifu na kumwabudu kwa moyo wote- Matendo 16:25-26.
  2. Maombi kali kali na kufunga saumu- Yakobo 4:14-17; Matendo 12:5-12.
  3. Kutembea katika haki na utii- Zaburi 1:1-3; Waebrania 12:4; Mathayo 5:8.
  • Mungu anapatikana panapo moyo safi- Zaburi 24:3-4.
  1. Tunapo simama katika imani dhabiti- 1 Wafalme 18:41.
  • Macho ya imani yanaona mbali zaidi- Kutoka 14:13-14.
  1. Kujitoa sana kwa kazi ya ufalme wa Mungu- Matendo 8:1-10.

MATOKEO YA KUTEMBELEWA NA MUNGU

  1. Maonyesho ya nguvu za Mungu- Isaya 64:1.
  • Miujiza, ishara, maajabu yanaonekana.
  1. Urejesho wa Mungu. Mungu anaturudishia tuliyopoteza- 2 Wafalme 6:1-7; Yohana 10:10.
  2. Kusawishiwa na kuokoka- Matendo 2:37-40.
  3. Utukufu wa Mungu- Mathayo 17:1-8.
  4. Hukumu kwa wenye dhambi.
  • Kora, Dathani, Abiramu- Hesabu 16:27-30.
  • Sodomu na Gomora- Mwanzo 18:20-21.
  • Herode- Matendo 12:21-23.
  • Kaini- Mwanzo 4:9-16.
  1. Mwongozo na kuelekezwa na Mungu- Mwanzo 12:1; Isaya 48:17.
  2. Kutembelewa na Mungu kunatutia nguvu na kudhibitisha uhusiano wetu na Mungu- Mwanzo 12:6-7, 13:14-18, 18:1-2.

MWISHO

  • Mungu Yu tayari kuwatembelea watu wake hivyo, ni lazima kutarajia kutembelewa.
  • Tujiweke tayari katika station ya imani na utakatifu, kumgojea Bwana atutembelee.
  • Tuombe Mungu atutembelee sasa.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *