I TIMOTHEO 1:12-17
UTANGULIZI
Baada ya kuhubiri miaka mitatu pale Efeso, paul aliacha kanisa la Efeso mikononi mwa mhubiri kijana Timotheo. (Matendo 19) Timotheo alikuwa kijana, alipata shida si haba katika uchungaji. Kwanza waalimu wa uongo walikuwa katika kanisa la Efeso (1:18-20) mafundisho ya uongo (1:3-7) ghasia katika ibada (2:1-15) viongozi kanisani (3:1-14) na tamaa ya mali (6:6-19). Pamoja na hayo wengine waliona Timetheo akiwa kijana sana kwa umri wake (4:12). Timotheo alikuwa miaka 30, lakini wagiriki waliamini kwamba mtu anakuwa mwanaume kamili akiitimu umri wa miaka 40!! Timotheo pia alikuwa na shida ya kuvunjika moyo na kukata tamaa hivyo Paulo anaandika waraka huu kumpa moyo Timotheo. Kwa kumtia nguvu Timotheo, Paulo alijitumia kama mfano wa neema na rehema za Mungu katika maisha yake. Tazama jinsi Mungu amenitendea kwa nehema na Rehema zake kwangu.
Hebu basi tutazame:
I. USHUHUDA WA MWENYE DHAMBI (I Tim.1:13,15)
- Matendo ya mwenye dhambi (v.13)
- Mtukanaji- (Blasphemer) alimtukana Mungu (Matendo 9:4)
- Alikataa kuitii amri ya kwanza (Mathayo 22:37) “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote kwa roho yako yote na kwa akili zako zote”
- Mwenye kuudhi watu, muuaji, Matendo 7:58,8:1, 9:1
- Alikataa kuwapenda wengine, jirani zake (Mathayo 22:39)
- Mwenye jeuri (Warumi 3:10-23)
Hivi ndivyo sisi sote tulikuwa jeuri sana
- Uongo wa mwenye dhambi (V.13)
- Nalitenda hivyo kwa ujinga na kukosa Imani
- Mwenye dhambi ni mjinga, kipofu rohoni (II Wakori. 4:4)
- Hali ya mwenye dhambi (V.15)
- Paulo alijiona mwenye dhambi Zaidi (chief of sinners)
- Lakini nayo neema ya Kristo ni nyingi Zaidi (I Wakorintho 6:9-11)
II. USHUHUDA WA MTAKATIFU (I Timotheo 1:13-14)
- Njia ya kuokoka –Neema ya Bwana, Imani na pendo
- Kwa rehema– Paulo hakuanguka jihanamu
- Kwa neema Mungu alimuokoa hasiyestahili.
- Neema ya Bwana inakuwa nyingi, hatuwezi kumaliza.
- Neema na rehema ya Bwana ndiyo inayo tafuta mwenye dhambi kuokoa (Waefeso 2:8-9, Titus 3:5)
- Neema ilizidi sana pamoja na Imani na pendo.
- Maonyesho ya kuokoka kwake Paulo (V.14)
- Neema inapokuja– huleta Imani na upendo (II WAkori.5:17)
III. USHUHUDA WA MTUMISHI WA MUNGU (I Tim.1:12)
Sababu ya huduma– ni “kuwekwa”
- Huduma ni kwa mapenzi ya Mungu (I Tim.1:17-19)
- Mungu anachangua mahali pa huduma (I Wakorin 12:7-31)
- Nguvu za huduma– Mungu alimtia Paulo nguvu (v.12)
IV. USHUHUDA WA KIELELEZO CHEMA CHA HUDUMA (I Tim.1:16)
- Mungu alipenda kuonyesha dunia yote uvumilivu wake kwetu.
- Kama Mungu anaweza kuokoa Paulo, basi anaweza kuokoa mtu yeyote yule.
- Jinsi Mungu alimwokoa Paulo ni kielelezo cha jinsi atakavyo waokoa wengine, msamaha wa dhambi na Imani katika Yesu Kristo aliyefufuka.
- Kama Mungu aliniokoa anaweza kumwokoa yeyote yule (Waefeso 2:10, Yakobo 2:18)
V. USHUHUDA WA KIONGOZI WA NYIMBO (Song leader) (I Tim.1:17)
- Paulo alipowaza juu ya wokovu wake aliimba wimbo wa sifa na utukufu kwa Mungu wake.
- Tunapoona jinsi Mungu ametutendea, alipotutoa, mahali tulipo sasa na mahali anapotupeleka tunamshukuru sana (Waebrania 13:15, Zaburi 50:23, Zaburi 50:14-15)
Hivyo
- Mungu anaona jinsi tunaweza kuwa (Potentials)
- Mungu hatuhesabii ya kale– bali anatusamehe
- Mungu anao mpango wa ajabu kwako na kwangu.
MWISHO
- Kama umeokoka lazima uwe na ushuhuda kama wa Paulo.
- Kama unaona katika maisha yako, bado hujaokoka kama jinsi Paulo– Basi okoka vizuri
- Usijali maisha ya kale na kitambo. Ibrahimu alindanganya, Nuhu alilewa, Yakobo alikuwa conman, Musa alikuwa muuaji, Samsoni alipenda wanawake, Daudi alifanya usherati, Paulo alikuwa mwenye kuudhi watu na mtukanaji, Magdalene alikuwa na pepo saba, Rahabu alikuwa kahaba– Lakini neema ya Bwana ilikuwa nyingi, ilizidi sana– Amen
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
