MFULULIZO: DANIELI-MUNGU NDIYE MHUKUMU.
SOMO: DANIELI 1:1-21
Mapenzi ya Mungu ni tuwe watu wa kutengeneza historia katika maisha ya watu wengine. Leo tumeanza mfululizo wa jumbe katika kitabu cha nabii Danieli. Mwongozo wa kitabu cha Danieli ni “Mungu anatawala juu ya yote” “God is sovereign.”
Kila mlango katika Danieli unazungumza juu ya ukuu wa Mungu juu ya kila jambo, juu ya kila mtu na kila taifa. Mungu anatawala juu ya kila jambo katika historia jana, leo na hata milele historia ni stori yake Mungu. Hebu tuone:-
- Kwamba tunaona Mungu ni mtawala juu ya mambo yote katika historia ya kila taifa na kila mtu.
- Bwana alimtia Yehokimu mfalme wa Yuda katika mkono wake Nebukadreza mfalme wa Babeli.
- Biblia inaeleza kwamba kila mtu anavuna kile alichopanda.
- Pamoja na kumweka mfalme Yehokimu katika mkono wa Nebukadreza, hekalu la Mungu Yerusalemu liliaribiwa kabisa na vifaa vyote vya hekalu kubebwa na Nebukadreza mpaka Babeli-(1-2).
- Ufalme wa Yuda tayari walikuwa wameishi katika hali ya kumwasi Mungu.
- Yuda alimwabudu sanamu kwa miaka mingi, lakini katika mwaka wa 605BC Mungu alitosheka na dhambi zao.
- Katika historia Mungu kwa ukuu wake anawainua wanaume kwa wanawake na kuwatumia kubadilisha historia.
- Mungu alipopenda kuinua taifa la Israeli alimwinua Ibrahimu.
- Mungu alipopenda kuwakomboa Israeli kutoka kwa utumwa wa Misri alimwinua Musa.
- Mungu alipopenda kuwaleta wana wa Israeli katika nchi ya ahadi alimwinua Yoshua.
- Mungu alipopenda kuwakomboa Wayahudi kutoka mikono ya Hamani alimwinua Esta.
- Mungu anapopenda kutueleza yatakayojiri duniani anamwinua Danieli.
- Je, na wewe unapenda kuwa mtu wa kugeuza na kutengeneza historia katika nchi yako, Katika maisha ya watu?
- Je, tunahitaji nini kuhitimu kuwa watu wanaobadilisha historia ya ulimwengu na pia historia za watu binafsi?
- Masharti ya kuitimu kuwa mtu wa kubadilisha historia yameandikwa-Danieli 1:3-4.
- Lakini katika vyovyote Mungu ni yeye atakayechagua wale watabadilisha historia ya nchi na historia za watu-1 Wakorintho 1:26-29.
- Kila aaminiye amepewa uwezo wa kuwa mbadili historia.
- Tazama wanafunzi wa Yesu Kristo na kuona kwamba kuwa mbadili historia ni kuchaguliwa na Mungu.
- Kutoka kwa ufalme wa Danieli tunaona kuna mambo manne (4) yanayo hitajika tuweze kuwa watu wa kutengeneza na pia kubadili historia ya dunia, taifa na watu binafsi.
Hebu tuone:-
KWANZA TUNAHITAJI KUWEKWA TAYARI (PREPARATION)-Dan. 1:4-5.
- Kulikuwa na mwalimu (Ashpenazi).
- Kulikuwa na mpango wa masomo (curriculum).
- Lugha.
- Masomo na mafunzo ya Babeli (literature).
- Kulikuwa na mipango ya muda na mhula.
- Kulikuwa na kuhitimu kuingia katika utumishi.
- Mungu ametupangia mwalimu mwema na hodari ili tuwe wenye kubadilisha historia ya ulimwengu, yaani Roho Mtakatifu-Yohana 16:13.
- Kila mtu aliyeokoka anaye Roho Mtakatifu ndani yake.
- Kazi ya Roho Mtakatifu ni kutufundisha juu ya Mungu.
- Mungu ametupatia mwalimu mwema na pia ametupa mpango wa elimu yetu.
- Biblia ndio mpango na vitabu vya Mungu.
- Mwalimu aliyeandika Biblia ni Roho mtakatifu.
- Biblia ni elimu tosha kutuweka tayari kuwa watu wa kubadilisha historia ya watu na mataifa-2 Timotheo 3:16-17.
- Tunahitaji:-
- Wakati wa binafsi kusoma neno-Biblia.
- Tunahitaji kusoma Biblia katika vikundi.
- Tunahitaji kusoma Biblia pamoja kanisani-Waefeso 2:10.
- Tunapoitumia Biblia kusoma na kujifunza tutakuwa watu wa kubadilisha dunia, taifa na watu binafsi.
PILI-TUNAHITAJI UTAKATIFU (PURITY)-Danieli 1:6-10.
- Pamoja na vijana kutoka nchi zingine kutoka Yuda palikuwa na Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria.
- Kungekuwa na wengi kutoka Yuda lakini wengi walianguka mitihani na usafi na utakatifu.
- Wengi walijichafua na chakula na pombe za kifalme.
- Kupita mitihani ya Mungu lazima kukataa chakula cha mfalme wa dunia hii kama vile pombe, madawa, madawa ya kulevya na mapocho pocho ya kishetani.
- Kitu cha kwanza Nebukadreza alibadilisha vijana wa Yuda majina yao. Nebukadreza alikuwa anajaribu kugeuza kitambulisho chao (identity).
- Danieli-Mungu ndiye hakimu-Betheshaza Maanake Beli-atakulinda.
- Hanania-Aku-(jua) akunenee.
- Mishaeli-Ni nani kama Yehova-Meshaki.
- Azaria-Yehova ndiye msaada wangu-Abednego-Maanake ni mtumishi na Nego-Mungu wa moto.
- Walipokea majina mapya lakini si utu mpya.
- Nebukadreza anaweza kubadilisha majina tu, lakini si tabia.
- Hili tupate kuishi katika utakatifu ni lazima kufahamu sisi ni mali ya Yehova-Mungu.
- Kupita mitihani ya ulimwengu huu ni lazima kwanza kufahamu wewe ni mali ya Mungu-Mungu ni sehemu yako.
- Danieli aliazimu moyoni mwake hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme wala divai yake.
- Kumwishia Mungu kunaanza na kuazimu moyoni.
- Kuazimu ni uchaguzi wa pale awali kufanya mapenzi ya Mungu kwa vyovyote vile.
- Danieli alisimama na Mungu wakati wa miaka 70 ya uhamisho. Ukisimamia Mungu, Mungu atakusimamia-V. 3-8.
- Watu wengi wanaanguka mitihani ya kuishi takatifu kwa sababu ya kumwogopa mwanadamu, lakini wanakataa kumwogopa Mungu.
TATU-TUNAHITAJI MAZOEZI (PRACTICE)-Danieli 1:11-16.
- Mwenye kutengeneza historia wanazoesha imani yao.
- Hawa hawaongei juu ya neno-lakini wanafanya ile neno-Yakobo 2:22-24.
- Unapotenda neno la Bwana utakuja kufahamu kwamba neno la Bwana ni dhairi-Zaburi 1:1-3.
NNE-TUNAHITAJI NGUVU ZA MUNGU (POWER)-Danieli 1:17-21.
- Hapa tunazidi kuona ukuu wa Mungu-Vs. 17.
- Mungu ni mwenye uwezo wote na pia Mungu anayafahamu yote.
- Mungu anapokuuliza kufanya jambo yeye pia atakupa nguvu na uwezo wa kutekeleza mapenzi yake.
- Mungu hawapi watu wake nguvu sawa, Danieli pekee ndiye alipewa uwezo na ufahamu katika maono yote na ndoto-(dreams and visions).
- Mungu alimtumia Danieli tangu ujana wake mpaka uzee (80).
MWISHO
- Hili tupate kuwa mwenye kutengeneza historia lazima-
- Kuwa tayari.
- Kuwa Watakatifu.
- Kuzoeza neno la Mungu.
- Kupokea nguvu za Mungu.
- Mungu ametuita tuwe watu wa kubadilisha historia na kutengeneza historia katika maisha ya watu, katika taifa na katika dunia yote.
- Je, utakua mmoja wao?
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO. - September 21, 2025
- GOD GUIDES OUR DESTINIES. - September 21, 2025
- GOD OF THE BREAKTHROUGHS - September 10, 2025