Swahili Service

TUNAPOZUNGUKWA NA KIBALI

MFULULIZO: MAFANIKIO

SOMO: RUTHU 1:1-2:18

.

Tunapozungukwa na kibali cha Mungu tunaongozwa kuingia katika hatima yetu. Je, hali yako ikoje? Pengine kwa miaka mingi mambo yako yamekwama, pengine afya yako, hali yako ya fedha zako, jamii na kupenya kwako kumekwama.

Pengine unapotazama siku zako zijazo unaona giza kubwa, pengine unazimia na kuvunjika moyo. Mungu anakwambia leo, “Usife moyo kwa maana Mungu anakuonekania kwa kibali chake-Zaburi 5:12.

Kibali maanake ni kusaidiwa, kupewa nafasi ya kwanza. Kibali ni kupendwa na kupokelewa. Tunapopewa kibali, haijalishi ni nani aliye kinyume chetu. Mungu anapokuwa pamoja nasi hakuna anaweza kutushinda. Katika Ayubu 10:12, “Umenijazi uhai na upendeleo, na maangalizi yako yamenilinda roho yangu.”

Watoto wa Mungu wamezungukwa na kibali cha Mungu usiku na mchana.

Mungu alimwambia Ibrahimu-Mwanzo 12:2, “Nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa na kukubariki, na kulikuza jina lako, nawe uwe Baraka.”

Kibali cha Mungu si kwa mtu mmoja, bali kwa mmoja jamaa zote zinapata kubarikiwa.

Watu wa Mungu wanakuwa wenye kusambaza Baraka zake.

Wewe pamoja nami tu watoto wa Mungu-watoto wa Ibrahimu kwa imani-Tumepewa kibali cha Mungu kwa ajili ya ulimwengu wote.

  • Kibali cha Mungu kinakufanya kupendwa na kukubalika hata wakati wewe hauna cheo au masomo.
  • Kibali cha Mungu kinakufanya kupendwa hata wakati haustahili.
  • Kibali cha Mungu kinakuweka mahali unahitaji kuwa wakati unaokubalika.
  • Kiballi cha Mungu kinakuponya magonjwa yako yote.
  • Leo ninaomba ukapokee kibali cha Mungu kwa maisha yako leo. Hebu tuone:-

MFANO WA KIBALI CHA MUNGU KATIKA BIBLIA.

  • Katika Biblia yote tunapata kuona Baraka na kibali cha Mungu kuwanufaisha watu wake.
  1. Mariamu-Luka 1:28, “Akaingia nyumbani kwake akasema, salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe.”
  2. Samweli-1 Samweli 2:26, “Na yule mtoto, Samweli akazidi kukua akapata KIBALI kwa Bwana na kwa watu pia.”
  3. Nuhu-Mwanzo 6:8, “Lakini Nuhu akapata KIBALI machoni pa Bwana.”
  4. Yesu Kristo-Luka 2:52, “Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akipendwa na Mungu na wanadamu.
  5. Yusufu-Mwanzo 39:4, “Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake.”
    • Mwanzo 39:21, “Lakini Bwana akawa pamoja na Yusufu, akamfadhili, akampa kibali machoni pa mkuu wa gereza.”
    • Ni kibali cha Mungu kilicho mtoa Yusufu kwa kile kisima alipotupwa na ndugu zake.
    • Ni kibali cha Mungu kilicho mpandisha Yusufu kuwa waziri mkuu mle Misri nchi ya utumwa wake.
  6. Wana wa Israeli; Kutoka 3:21 “Nami nitawapa watu hao kufadhiliwa mbele ya Wamisri hata itakuwa, hapo mtakapo kwenda zenu hamtakwenda kitupu.”
  • Kutoka 12:35-36, Mungu anafanya adui zako kukufadhili na kurudishiwa yote uliyenyang’anywa na watu.
  • Huenda kupandishwa cheo kwako kumechelewa, pengine unaona kama umedanganywa, lakini ushindi na kibali cha Mungu kikaribu nawe. Umekubalika.

RUTHU

  • Leo tunaangazia kibali juu ya Ruthu.
  • Jamii ya Ruthu iliadhirika zaidi, katika nchi ya Moabu.
  • Elimeleki, Naomi na wana wao wawili waliamua kwenda Moabu kwa kuwa kulikuwa na njaa nyingi Yuda ya Bethlehemu.
  • Wana wao wawili waliwaoa binti za Moabu.
  • Baada ya wakati, Elimeleki na watoto walikufa, hivyo wajane waliachwa.
  • Naomi aliamua kurudi kwao Bethlehemu.
  • Jamii zinaingia mashakani leo-Ruthu 1:14-16.
  • Naomi aliamua kurudi kwao Bethlehemu.
  • Naomi na Ruthu wafika Bethlehemu, kibali cha Mungu kilimngoja Ruthu-Ruthu 2:1-2.
  • Ruthu aliamini kwamba ameingia katika katika jamii ya kiungu.
  • Ruthu alikuwa na Roho ya kibali-Ruthu 2:3-5.
  • Kibali kinakufanya uonekane.
  • Kibali kinakufanya uwe mahali wakati unaofaa-Ruthu 2:6-8; 2:13.
  • Kibali kinakufanya kutoka “Hustler” na kuwa mtu anayejulikana kote kote.
  • Kibali kinakufanya kupewa heshima, fadhili na upendo kwa watu.
  • Kibali kinamlinda mtu-Ruthu 2:9.
  • Kibali kinakutumikia na kukutosheleza-Ruthu 2:9-12.
  • Kibali kinakulipa ulichopoteza awali.
  • Kibali kinafanya kikombe chako kujaa na kufurika-Ruthu 2:14-18.

JINSI YA KUPOKEA KIBALI CHA MUNGU.

  • Tubu dhambi, ishi katika imani na utakatifu.
  • Mwite Mungu wako.
  • Ishi na akili ya kibali na kukubalika-Ruthu 2:1-2.

MWISHO

  • Mungu wa Ruthu ndiye Mungu wetu.
  • Mungu wa Ibrahimu ndiye Mungu wetu.
  • Lazima kuishi na akili ya kibali, kukubalika na kupendwa-Zaburi 30:5.
  • Kibali cha Mungu kikakuzunguke pande zote leo.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *