Swahili Service

TUWE TAYARI KWA MWISHO WA DUNIA HII

MFULILIZO: YESU KRISTO NI  WA THAMANI SANA

SOMO: I PETRO 4:7-11, LUKA 12:35-43               

Mtume Petro anatupa marsharti ya jinsi ya kuishi tunapongoja mwisho wa dunia hii. Tuko safarini kwenda juu mbinguni. Hivyo Mtume Petro anatoa ushauri wake wa jinsi ya kuishi kwa subira nyingi. Mwisho ya mambo yote umekaribia. Mambo yote yaliyo duniani sasa yaonyesha mwisho wa dunia hii umefika.

Hebu tuone:-

I.  IWENI NA AKILI , MKESHE KATIKA SALA (V.7)

  • Amri ya kwanza ya kutufanya tayari, kurudi kwa Mwokozi Yesu Kristo ni “muwe na akili, mkeshe katika maombi.”
  • Dhambi za kale zilitosha, sasa tuishi kwa utakatifu (4:3-4)
  • Tulete akili zetu pamoja na kukesha sana
  • Tusikubali chochote kile kutuondoa kutoka kwa maombi
  • Tusiache kazi, tamaa za mwili na mapenzi ya nia zetu, kutuweka mbali na Mungu na maombi.

II.  IWENI NA JUHUDI NYINGI KATIKA KUPENDANA (V.8)

  • Upendo husitiri (ufunika) wingi wa dhambi
  • Upendo wa wandugu uzidi zaidi
  • Upendo wa ukweli unasamehe watu wengine
  • Upendo wa kweli unaponya mioyo, upendo wa kweli hautangazi dhambi za wengine
  • Upendo unapokea udhaifu wa wengine (Mithali 10:12, I Wakorintho 13:4-7)
  • Upendo unawapokea wengine bila marsharti kama jinsi Kristo alivyotupokea sisi.
  • Upendo hau hukumu wengine (Mathayo 7:1-5)

 

III. MKARIBISHANE NINYI KWA NINYI (4:9)

  • Amri ya tatu kutuweka tayari kwenda mbinguni ni kukaribishana bila kunung’unika.
  • Kukarimbishana ni kujali sana mahitaji ya wengine miongoni mwetu.
  • Tusinungunike watu wanao tutembelea, hau watu wanapohudumiwa.
  • Wengi wananung’unika kwa sababu ya gharama, kukatishwa sherehe, kazi nyingi,  hakuna asante, wangeni wengine wana mtarajio mengi zaidi (wengine ni kama jinsi samaki wananuka siku ya tatu)
  • Tunaposafiri duniani kwa ajili ya neno la Bwana ukarimu unahitajika sana (wapilisi 2:14)

IV.  KUHUDUMIANA KAMA MAWAKILI WEMA WA NEEMA YA MUNGU (4:10-11)

  • Amri ya tatu, kutuweka tayari kwa wakati huu wa mwisho ni kutumikiana kama mawakili wema.
  • Mungu ametupa karama mbalimbali hili kuhudumiana (Warumi 12, Wakorintho 12)
  • Mungu ametupatia karama ya neno lake (Metendo 7:38, Warumi 3:2, Waebrania 5:12) na nguvu zake, hili kuhudumiana.
  • Mungu ametupa chochote tunachohitaji kuhudumia wengine.

V.  LENGO LA MAISHA KUTAFUTA (4:11)

  • “Katika mambo yote, Mungu atukuzwe”
  • Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele
  • Katika amri zote nne, tunapozitimiza ni utukufu kwa Bwana.
  • Sababu ya kumtumikia Mungu na watu ni hili, Mungu apokee utukufu.
  • Ishi kwa akili, na kukesha na kuomba kwa maana mwisho wa mambo yote umekaribia.
  • Wapende watu, fanya kazi na kutenda mema, siku ni za mwisho.

MWISHO

  • Wakati uliombaki ni mfupi sana, basi tukazifuate amri hizi nne na kukumbuka (Luka 12:35-43)
  • Mungu hawezi kusahau kazi yetu tunaofanya kwa utukufu wake.
  • Pengine umeishi maisha ya ubinafsi na Leo unapenda kumwishia Kristo, basi joo kwake leo.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

1 thought on “TUWE TAYARI KWA MWISHO WA DUNIA HII”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *