Swahili Service

UKUMBUSHO KWA WAPITAJI NA WASAFIRI

MFULILIZO: YESU KRISTO NI THAMANI SANA

 SOMO:  I PETRO 2:9-12

Petro anatukumbusha kama waamini, kwamba sisi ni wapitaji, wageni na wasafiri duniani. Neno, ‘mgeni maana yake ni mtu anayeishi kwa wakati katika inchi isiyo yake. Anaishi hapo kwa mda kiasi kuitaji nyumba ya kuishi lakini si mtu asili kwa hio inchi anayoishi (not permanent resident). Huyu mtu hana haki zake hau haki za uananchi, yeye ni mgeni (stranger). Huyu mtu ni mkimbizi katika inchi ya kigeni “mpitaji” ni msafiri anayepita katika inchi ya kigeni kwa mda mfupi zaidi kuliko mgeni. (pilgrim = temporary traveler on the move). Sisi tuliookoka tuwapita njia kuelekea kwingine.

Basi maneno wapitaji na wasafiri yanaeleza wlaio watoot wa Mungu. Tunaishi hapa duniani, lakini dunia si mahali petu, yaani dunia hii si nyumbani. Wafilipi 3:20 – tuko hapa wakati mfupi, mfupi kiasi kuitaji nyumba ya kuishi na kazi ya kutupa riziki lakini sisi sio wenye inchi. Tunaishi katika wenye inchi asili, tabia zao ni geni kwetu, tuko safarini ya kwenda mbinguni (Wakolosai 3:1-3). Hivyo Petro anatukumbusha jinsi tulivyo na jinsi ya kuishi kama wapitaji wasafiri.

Hebu tuone:-

I.  UKUMBUSHO WA JINSI TULIVYOKUWA HAPO AWALI (V.9-10)

  1. Tulikuwa gizani (V. 9)
  • Tunakumbushwa kwamba Yesu alitupata katika giza ya dhambi (Waefeso 2:1-3)
  • Yesu Kristo alitukuta tukiishi kama tulivyopenda
  • Maisha yetu ilikuwa ya anasa zilizo tufanya watumwa wa dhambi (Mithali 16:25)
  1. Maisha yetu ya kale yalikuwa maisha ya dharau (V.10)
  • Hatukuwa katika taifa lake Mungu (Waefeso 2:12, Wakolosai 1:21)
  • Tulikuwa adui wa Mungu (Warumi 8:7)
  1. Tulikuwa wafu (V.10)
  • Yesu Kristo alipotujia tulikuwa bure kabisa
  • Hatukuwa tumepata rehema za Mungu
  • Hatukuwa tumepata neema ya Mungu
  • Laking katika Kristo tulipewa neema na rehema
  • Ni neema na rehema ya Mungu pekee iliyoleta utofauti katika maisha yetu. (Waefeso 2:8-9, I Wakorin 15:10)

II.  UKUMBUSHO WA JINSI TULIVYO SASA (V.10)

  1. Sisi sasa tu viumbe mpya
  • Sisi ni kizazi teule (chosen generation)
  • Tumechanguliwa na Mungu kutoka kwa wanadamu wengine.
  • Mungu alimwita Ibrahimu atoke kwa watu wake (Mwanzo 12:1-9)
  • Mungu anaunda watu wapya, wateule, watakatifu (I Wakorintho 10:32, 12:13)
  • Dunia hii haituelewi, maana sisi tuwageni kwao, fikira zetu na mwenendo wetu ni tofauti.
  1. Sisi sasa ni hukuani wa kifalme (royal priesthood)
  • Tulipokuwa katika dhambi tulitengana na Mungu
  • Sasa sisi tuliokuwa mbali tumeletwa karibu na Mungu (Waefeso 2:13)
  • Kuta zote zimevujwa, sasa tumepata nafasi kubwa mbele ya Mungu, yaani ukuhani wetu ni wa kifalme (I Tim 2:5, Waefeso 2:14-19, Waebrania 4:16)
  1. Sisi sasa tumepata tabia mpya (Taifa takatifu la Mungu) (Holy Nation)
  • Tumeamishwa kutoka kwa giza na kuingia katika nuru (warumi 3:12, Isaya 64:6, II Petro 1:4, II Wakonritho 5:17)
  1. Sasa sisi tu watu wa ajabu (Peculiar people)
  • Sisi sasa tu watu wa dhamani sana
  • Tunalindwa I Petro 1:5, Yohana 6:39
  • Tunamsifu na kumwabudu Mungu tofauti (Malaki 4:17)

III. UKUMBUSHO WA UTUMISHI WETU SASA (V.9-12)

Sasa sisi ni balozi wa Kristo Yesu (II Wakorintho 5:20)

  1. Tunatangaza fadhili za Mwokozi wetu (V.9)
  2. Tunaonyesha ukweli wa wokovu wetu (V.11-12)
  3. Mwenendo wetu ni wakimbingu (V.11)
  4. Tunashuhudia kwa nguvu wokovu wa Mungu.
  5. Wazungu walipoingia America, waliwapa wahindi pombe kali mpaka leo wahindi wa America ni walevi sungu.

MWISHO

  • Mpaka Yesu Kristo arudi tena sisi tutakuwa wapitaji na wageni duniani.
  • Tukumbuke tumezungukwa na wageni walio na tabia tofauti.
  • Tuka hubiri neno natabia ya mbinguni, tukaache dunia hii bora kuliko jinsi tulivyo ikuta.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *