SOMO: YAKOBO 5:13-16
Dhiki ni kawaida kwa kila Mkristo, lakini Mungu ameahidi na amepanga kila mmoja wetu kupokea ukombozi kutoka kwa kila dhiki.
Maombi ndio njia pekee na dawa pekee ya kushinda kila dhiki. Dhiki inaweza kuwa umaskini, magumu ya maisha, biashara kufifia, magonjwa, shida katika jamii na ndoa, watoto kuvamiwa na shetani, kukataliwa na watu, janga na mikosi. Haya yote yanapotujia tusifadhaike mioyo bali tumwombe Mungu wetu.
Shetani yupo kazini kukuibia amani, furaha na nguvu zako.
Kila wakati wa dhiki Mungu atatenda chochote mpaka tumkaribishe katika hali yetu-Matendo 7:7; Waebrania 11:6.
Dhiki ni sehemu ya ujuzi wa kuwa Mkristo. Tangu kuokoka, ulijitambulisha na Yesu Kristo hivyo majaribu na dhoruba zitakwandama, lakini tumepewa uwezo na mamlaka ya damu, jina, msalaba na maombi. Tumepewa ushindi juu ya kila aina ya dhiki lakini mamlaka tuliyo pewa yanafanyishwa kazi kupitia maombi. Tumepewa mifano ya watu kama sisi waliopewa nguvu na uwezo juu ya dhiki zao.
Hawa wote waliomba Mungu na Mungu hakuwapungukua kamwe.
Hivyo, na sisi pia hatutaachwa, wala kupungukiwa wakati wa dhiki.
Watu kama jinsi Yakobo, Hanna, Yabezi, Ayubu na mitume wa Mwokozi wetu. Hebu tuone:-
MAELEZO JUU YA DHIKI.
- Kuna njia nyingi za kueleza maanake dhiki.
- Dhiki ni janga ambazo zimepangwa na shetani juu ya maisha ya mtu, jamii, kanisa, nchi au dunia.
- Mpango wa dhiki ni kuharibu imani yako na kuing’oa kabisa. Mpango wa dhiki ni kuharibu ujasiri wako ndani ya Mungu, kutekwa nyara na shetani ukafanye mapenzi na mipango yake.
- Wakati shetani alimjia Ayubu, dhiki ilikuja upesi na kwa njia nyingi-Ayubu 2:4-10.
- Dhiki ni mateso ya kuendelea kutoka kwa shetani kazi ngumu ya watesi wa shetani.
- Kila hali ya kunyanyaswa, kazi ngumu bila malipo kutoka kwa wenye nguvu kimwili au kiroho.
- Baada ya kifo chake Yusufu, farao mpya alitawa Misri, aliwafanyisha kazi ngumu na kuwatesa-Kutoka 3:7-10.
- Kuna watu wengi na pia wandugu katika Kristo wanaoteswa chini ya pepo wachafu dhiki zao, maumivu yao na kilio chao ni kingi zaidi.
- Kila aina ya utumwa wa shetani, dhiki chini ya mapepo inafanyika kila siku, ili watu wasitimize mapenzi ya Mungu katika maisha yao.
- Mateso na vita vya kila aina kwa sababu ya Agano na laana zinazoleta kukwama katika maisha, kukosa kibali na kupenya katika maisha-Marko 5:1-6.
- Magonjwa ya kila namna na magonjwa sugu yanaoendelea kwa muda mrefu au kwa maisha yote-Luka 13:11-13.
- Maonyesho yanaofanya na kula mshahara na mapato ya mtu.
- Shetani anachangia pakubwa kwa kuharibu nafaka wakati wa mavuno. Wakati wa mavuno mabaya yanatokea kumaliza mavuno-Luka 8:43-44.
- Kucheleweshwa kwa eneo au maisha yote.
- Baraka zinapochelewa bila sababu-1 Samweli 1:1-6.
- Kukosa amani katika jamii
- Dhoruba katika jamii, ndoa, watoto na kupoteza mali.
- Eli aliteseka ka ajili ya watoto wake kiasi huduma yake ikatatizika-1 Samweli 2:12-17.
KIPIMO CHA DHIKI
- Dhiki zinakuja kwa vipimo vingi na ukubwa, nyakati na majira ya maisha na kwa sababu, na nyakati nyingi.
- Dhiki zinazopinga imani yetu.
- Kunazo dhiki za kupigana na imani yetu ndani ya Yesu Kristo-Warumi 8:35-39.
- Danieli alipitia dhiki-Danieli 3:17-21; 6:11-16.
- Dhiki zinazokuja kutatiza amani-Wafilipi 4:6-7.
- Dhiki zinazotatiza furaha-2 Wafalme 4:16-20.
- Dhiki zinazotatiza kazi na juhudi zetu-2 Timotheo 2:6.
- Dhiki zinazotisha maisha yetu.
- Dhiki za kifo-Esta 3:5-6.
- Dhiki zinazokuja kulipiza kizazi-Matendo 16:16-20.
- Dhiki zinazokuja kutimiza maagano na laana-Marko 9:21-27.
- Mtu anapoishi chini ya laana au anapoishi katika Agano yake na shetani, dhiki Fulani zitafuatana naye ili ziweze kutekeleza maagano.
- Kijana aliyekuwa na roho ya bubu na kiziwi alikuwa chini ya Agano na laana Fulani-Marko 9:21-27.
UKOMBOZI KUTOKA DHIKI.
- Kunao ahadi na Mungu kukomboa wenye haki kutoka kwa kila dhiki.
- Tunahitaji kumlilia Mungu kupitia maombi tupate ukombozi.
- Hili maombi ya ukombozi yapate kufanya kazi lazima kutimiza masharti yafuatayo.
- Ungama dhambi zote.
- Ungama na kutubu dhambi unazojua na usizojua. Ungama dhambi za vizazi na pia za wazazi wako-1 Yohana 1:8-10.
- Furahi katika neno la Bwana na kuzitafakari ahadi zake-Obadia 1:17; Zaburi 34:19.
- Simama katika mamlaka yako kama mwana wa Mungu.
- Tumepwa uwezo na nguvu na mamlaka juu ya kila pepo na agenti wote.
- Lazima kusimama katika haki zake na mamlaka yake ili tupate kupona na kukombolewa-Luka 10:18-19.
- Jisalimishe chini ya maombi ya kanisa na Wazee wa kanisa.
- Kanisa liko na upako wa pamoja.
- Petro alifunguluwa kutoka gerezani kwa maombi ya kanisa jumla.
- Katika kanisa, Wazee wameagizwa na Mungu kuomba kwa imani, kwa uponyaji na kwa ukombozi.
- Jisalimishe chini ya Roho Mtakatifu-Hili kupata ushindi wa kudumu lazima kudumu katika Roho Mtakatifu-Wagalatia 5:16.
MWISHO
- Dhiki ni hali ya kawaida kwa wanaoamini.
- Katika kila dhiki tumehimizwa kuomba na kuombewa.
- Mungu ametupa ushindi na ukombozi tayari kupitia neema ya Kalvari.
- Ukombozi unakuja kupitia maombi makali na imani.
- Leo pokea ushindi, ukombozi na uponyaji juu ya mwili na maisha yako.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
