Swahili Service

USIINGIE KATIKA KOSA LA REHOBOAMU.

MFULULIZO: WASHINDWA WAKUU KATIKA BIBLIA.

SOMO: I WAFALME 12: 1-24; WARUMI 15:4.

 

Utawala wa Rehoboamu juu ya Israeli ulikuja wakati mgumu sana- Israeli. Mfalme Suleimani babaye alikua amewatumia wana wa Israeli vibaya. Alikua amewaweka wana wa Israeli katika kazi ya utumwa (forced labour) na kuongeza ushuru zaidi. Hivi watu wa Israeli walikuwa wamechoka na mfalme Suleimani. Walitarajia mwanawe Suleimani (Rehoboamu) atawatawala watu vyema kuliko babaye.

Mara tu, alipotawazwa Rehoboamu wazee wa makabila ya Israeli walimwendea Rehoboamu na kumsihi kupunguza ule ushuru na kazi nzito aliyoeka juu ya watu, babaye Suleimani.

Kwanza mfalme Rehoboamu alitafuta ushauri kutoka kwenye Wazee wa watu walio kua washauri wa mfalme Suleimani. Baadaye mfalme Rehoboamu aliwaendea vijana wa rika lake kuomba ushauri.

Vijana wenzake walimshauri kuongeza ule ushuru na kuongeza mizigo juu ya wana wa Israeli.

Wana wa Israeli walipoona mfalme Rehoboamu ameongeza, ushuru na mizigo yao, na bei  ya maisha ikapanda zaidi wana wa Israeli walijikata na kujitenga na mfalme Rehoboamu.

Makabila 10 (kumi) walijitenga na kuanza  taifa lao kwa jina Israeli- makao yao makuu yakawa mle samaria.

Rehoboamu alibaki wa kabila mbili, yaani Yuda na Bejamini.

Hivi Rehoboamu alikua mfalme wa mwisho kutawala taifa lote la Israeli.

Kutoka wakati huo kukawa na falme mbili, Israeli na Yuda. Kila jambvo likawa mbili, Wafalme wawili, utawala mbili, ibada mbili, jeshi mbili, makuhani wakuu wawili. Yeroboamu alikua mfalme wa Israeli na Rehoboamu mfalme wa Yuda.

Rehoboamu alifanya makosa tatu yaliyo mfanya mshindwa mkuu katika Biblia. Hebu tuone;

KOSA LA KWANZA: USHAWISHI MBOVU.

  • Vijana Rehoboamu aliowafanya washauri wake walikuwa vijana waliosoma naye Rehoboamu.
  • Hawa vijana hawakua na hekima ya kutosha na ujuzi, maarifa ya kuelewa na jinsi ya kutawala watu.
  • Matokeo yalikuwa ni kugawanya ufalme wa watu wa Israeli.
  • Kila mtu ana watu wakushawishi na wakushawishiwa nao –wazazi, marafiki, walimu, na wasanii.
  • Tunashawishiwa na watu wa kila haina.
  • Katika safari ya maisha watu wa haina nne watachangia sana katika maisha;
  1. Watu wanaoongeza dhamani yetu.
  2. Watu wanaopunguza dhamani yetu.
  3. Watu wanaozidisha dhamani yetu.
  4. Watu wanaogawanya dhamani yetu.
  • Kulingana na watu unaofanya urafiki nao hatima yako itapunguka na yao kuongezeka.
  • Urafiki ni uhusiano wa kutegemea katika watu wawili au zaidi
  • Marafiki wa kweli watakuongoza kufanya mema, lakini marafiki waovu watakupeleka mbali kwa makosa.
  • Marafiki waovu watakueleza yale utakayo kusikia, marafiki wema watakukosoa.
  • Marafiki wengine ni wachoyo, wachungu na wengine hawana usalama wa binafsi.
  • Marafiki wengine wamekuja kuchukua ulicho nacho, amani, furaha na wakati ( I Wakorintho 15:33)
  • Watu unaotumia wakati nao watachangia katika maisha yako kwa mabaya au mazuri-Mithali 27:17

KOSA LA PILI: REHOBOAMU ALIKATAA HEKIMA YA MUNGU.

  • Mfalme Rehoboamu alitafuta ushauri wa wazee waliomshauri mfalme Suleimani, pia Rehoboamu alitafuta ushauri wa vijana wenzake, lakini hakuna kumtafuta Mungu, hakuna maombi, hakuna neno la Mungu.
  • Hekima ni kutekeleza ufahamu na ujuzi.
  • Mtume Yakobo anatueleza aina 4 za hekima (Yakobo 3:15-18)
  1. Hekima ya dunia hii.
  2. Hekima ya mwili.
  3. Hekima ya shetani.
  4. Hekima ya Mungu. Hii ni hekima itokayo juu.
  • Hekima inajenga (Mithali 24:3-4; 9:1)
  • Babaye Rehoboamu (Suleimani) anaeleza juu ya hekima (Mithali 4:5-7)
  • Mwogope Mungu (Mithali 9:10).
  • Penda hekima (Mithali 2:4).
  • Omba hekima (Yakobo 1:5).
  • Nyenyekea kwa hekima (Yakobo 3:13-16).

KOSA LA TATU: REHOBOAMU ALIMWACHA MUNGU (2 MAMBO YA NYAKATI 12:1)

  • Rehoboamu alikana Mungu pamoja na taifa lake-I Wafalme (14:22-24)
  • Kukana ni kukataa, kuacha unayempenda.
  • Kumkana Mungu ni kuendelea maisha yako bila kuomba, unaposhindwa na kusoma Biblia yako, unapoacha ibada yako mbele za Mungu.
  • Unapokataa kuwashuhudia watu Yesu Kristo na upendo wake.

KWANINI WATU WANAMWACHA MUNGU?

  1. Kutafuta mali na fedha, mali inatufanya tusimtegemee Mungu.
  2. Kutumainia watu wa cheo na mamlaka kuliko kumtegemea Mungu.
  3. Kiburi (Kumbukumbu 8:17).
  4. Anasa na tamaa (Yakobo 4:4; I Yohana 2:16)
  • Tutafanya nini tusimwache Mungu kama jinsi Rehoboamu.
  • Kiri hali yako ya kiroho, kana kila miungu ya uongo, tubu dhambi (Hosea 6:1)
  • Mtafute Bwana kwa kua na wakati wa binafsi – tulia mbele zake-(Zaburi 119:97).
  • Dai ahadi za Mungu na urejesho wake.

MWISHO:

  • Rehoboamu alikuwa mshindwa mkuu zaidi.
  • Tujifundishe kwa maisha ya Rehoboamu.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *