Swahili Service

USIONE HAYA KWA BWANA

MFULULIZO: SIONI HAYA

SOMO: 2 TIMOTHEO 1:1-12

 

Paulo anamwandikia mchingaji kijana Timotheo aliyekuwa na woga mara kwa mara zaidi wakati mambo hakuwa mazuri. Mara kwa mara Timotheo aliona haya kwa injili ya Yesu Kristo kwa sababu ya dhiki, majaribu na mateso. Paulo anamweleza Timotheo kwamba kuna vitu na mambo katika maisha hatuitaji kuona haya. Kama wakristo tunapatwa na hali ya kuona haya kwa jinsi tulivyo kama watoto wa Mungu. Tunaona haya kwamba tunampenda Yesu Kristo. Paulo hakuona haya kwamba anampenda Yesu Kristo, hakuona haya kwa injili na msalaba wa Yesu Kristo. Katika kifungu cha leo tunajifunza kwamba kuna Baraka za Bwana mbazo hatuitaji kuona haya. Hebu tujifunze:-

USIMWONEE HAYA MWOKOZI WAKO-2 Tim. 1:8.

Usione haya kwa mateso yake.

  • Usione haya kujitambulisha na msalaba wa Kristo.
  • Msalaba ndio asili ya mema kwako, msalaba ndio ulinunua wokovu wako.
  • Msalaba ndio mpaka wa waliookoka na wenye dhambi-1 Wakorintho 1:18-21.
  • Yaliyo tendeka msalabani siku hiyo ndio ilileta utofauti duniani.
  • Msalaba ndio umekufanya kuja hapa leo.
  • Badala ya kuona haya, tukapate utukufu katika mateso ya Kristo-Wagalatia 6:14.

Usione haya kwa mpango wake.

  • Usione haya kujitambulisha na injili ya Kristo.
  • Huenda injili ikaleta mateso na kutengana, lakini injili ndio ilikuleta msalabani na kwa miguu ya Mwokozi.
  • Injili ndio nguvu za Mungu kuokoa wenye dhambi-Warumi 1:16.
  • Injili ndio njia ya kwenda mbinguni, ndio ahadi ya wokovu-Yohana 14:6.

Usione haya kwa watu wa Mungu.

  • Paulo anamshauri Timotheo asione haya kwa watu wa Mungu, wala wale wamefungwa kwa ajili ya injili.
  • Tusione haya kujitambulisha na wale wanahubiri injili ya Yesu Kristo.
  • Wanaweza kuwa ajabu kwa mavazi yao, umbo wao lakini wao ni familia.
  • Usione haya kumsifu, kuabudu au kumhubiri Yesu Kristo.

USIONE HAYA KWA WOKOVU WAKE-2 Tim. 1:9-10.

  • Usione haya kwamba umeokoka.

Wokovu wake ni mkuu sana.

  • Paulo anamkumbusha Timotheo kwamba “Tumeokoka” na tunakaa katika kuokoka milele.
  • Wokovu ni jambo ambalo limemalizika na kukamilika daima.
  • Ikiwa umeokoka, umeokoka milele na mbinguni ndio nyumbani kwako-Waefeso 2:6; Warumi 8:29-30.
  • Waebrania inatukumbusha kwamba wokovu wetu ni mkuu sana-Waebrania 2:3.

Neema ya wokovu wake.

  • Paulo anaeleza kwamba wokovu ni kwa neema.
  • Hatukustahili wokovu wake lakini neema yake ilikuwa nyingi kwetu.
  • Hata ingawa Mungu alijua maisha yetu ya kale na ya kesho, lakini alitupenda na kutuokoa kwa neema yake-Waefeso 2:8-9; Tito 3:5.
  • Wokovu ni neema kutoka mwanzo mpaka mwisho-Isaya 64:6-8.

Utukufu wa wokovu wake.

  • Paulo anamweleza Timotheo kwamba kwa mateso ya Yesu Kristo msalabani Kristo alimaliza kifo na mauti.
  • Mauti adui mkuu wetu alishindwa na Yesu Kristo alipofufuka kwa wafu-1 Wakorintho 15:55.

USIONE HAYA KUMTUMIKIA KRISTO-2 Tim. 1:11-12.

  • Paulo anamweleza Timotheo kwamba ni Injili inayo mfanya amtumikie Mungu.
  • Ujumbe wa neema ya Mungu unamfanya Paulo kumtumikia Kristo.

Mungu anamweka Paulo kuwa mhubiri na mtume na mwalimu-Vs. 11.

  • Kama mhubiri anawaeleza watu habari njema ya ufalme wa Mungu.
  • Kama mtume anatumwa kwenda mbali kwa ajili ya mfalme.
  • Kama mwalimu anawaeleza watu juu ya mfalme-Zaburi 84:10.

Dhiki katika huduma-Vs. 12.

  • Paulo alikuwa katika dhiki na gerezani kwa sababu ya Injili.
  • Watakao mtumikia Bwana watateseka kwa kudhihakiwa-2 Tim. 3:12; Yohana 16:33.

Dhamana na hakikisho katika huduma-Vs. 12.

  • Paulo alipumzika katika ufahamu na hakika kwamba Mungu anao uwezo wa kuwahifadhi wote anao okoa, anao uwezo wa kulinda.
  • Paulo aliweka amana kwake Bwana.
  1. Nafsi yake na maisha yake.
  2. Dhabihu na nafsi yake.
  3. Huduma yake kwa Bwana.
  • Mungu anao uwezo wa kulinda tulicho weka amana kwake hata siku ile-1st Petro 1:5.
  • Kristo ametupatia uzima wa milele, huduma ya Injili, nasi tumempa ule uzima, huduma na dhabihu kwa maana ni yeye anaweza kulinda amana tulichompa.
  • Kristo hawezi kupoteza tulicho mpa, anao uwezo wa kulinda sisi hatuna uwezo.
  • Kristo amekupa, sasa wewe nawe umpe, ndiye anao uwezo wa kulinda.

MWISHO

  • Je, unaona haya na aibu kwa Bwana?
  • Je, unaona haya kwa wokovu?
  • Je, unaona haya kwa watu wa Mungu?
  • Kristo anao uwezo wa kulinda.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *