Swahili Service

USIUZE URITHI WAKO.

MFULULIZO: YAKOBO; ALIFANYA MIEREKA NA MUNGU.

SOMO: MWANZO 25:27-34; WAEBRANIA 12:14-17.

 

Usiuze urithi wako kama jinsi Esau alifanya. Usiuze ukuhani wako, usiuze ahadi za Mungu, usiuze nguvu zako juu ya dhambi. Lakini kwa imani ukafurahi kwa urithi na haki yako kama mwana wa Mungu. Ishi kama mfalme kwa sababu wewe ni mwana wa mfalme. Esau aliuza urithi wake kwa sababu aliona ule urithi bure. Esau aliuza kitu cha dhamani sana kwa bakuli ya dengu na mkate. Kulingana na desturi za wakati huo, mzaliwa wa kwanza alipata urithi mara dufu. Alipouza ule urithi, Esau alipoteza haki na marupurupu yake yote. Hebu tuone:-

ESAU ALIPOTEZA HAKI YA KUHANI

  • Kuhani ni mtu anayesimama mbele ya Mungu kwa ajili ya watu.
  • Kuhani ni mwombezi kwa niaba ya binafsi na watu, jamii, taifa na dunia.
  • Mungu amepanga kwamba hakuna atakayemjia bila kuhani.
  • Leo hii katika Agano jipya, kila mkristo anao ukuhani wa binafsi, lakini kuhani wetu ni Yesu Kristo- Waebrania 7:26-28; 1st Petro 2:9-10.
  • Mzaliwa wa kwanza alikuwa na haki ya ukuhani, alitolewa kwa Mungu kumtumikia Mungu.
  • Katika wakati wa Esau, ukuhani ulikuwa ni kwa mzaliwa wa kwanza. Esau alipouza urithi wake, alitupa mbali ukuhani.
  • Pia Esau aliuza haki ya kupokea maradufu ya urithi wa ardhi wa babaye.
  • Pia Esau alitupa nguvu na haki ya kuongoza jamii ya babaye. Esau alikuwa na haki ya kumiliki na kusimamia nyumba ya babake baada yake, kutunza mama yake, ndugu zake na dada zake mpaka kuolewa kwao.
  • Usiuze urithi wako kama Esau- Waebrania 12:14-17.

USIUZE AHADI ZA MUNGU

  • Usiuze haki yako kurithi ahadi ya Mungu kwako kwa sababu ya anasa na mapambo ya dunia hii.
  • Ahadi za Mungu ni kutoka kwa neema yake-Waebrania 12:14-17, V.15.
  • Basi nasi tusipungukiwe na neema ya Mungu kama jinsi Esau aliyedharau ahadi za Mungu kwake.
  • Ahadi za Mungu kwako ni zaidi ya fedha na dhahabu.
  • Tumeahidiwa ufalme mwema zaidi ndani ya Yesu Kristo.
  • Usiuze ukuhani wako wala ahadi za Mungu kwako.

USIUZE NGUVU ZAKO KAMA MWANA WA MUNGU

  • Usiuze mamlaka yako kwa sababu ya anasa za dunia hii.
  • Usiache dhambi itawale maisha yako, wala shina la uchungu lisije likachipuka ndani yako.
  • Dhambi inaanza kama mbegu, baadaye shina na mwishowe mti mkubwa.
  • Usiuze nguvu zako, urithi wako kama jinsi Esau.

 

MWISHO

  • Usiuze ukuhani wako, ahadi za Mungu kwako.
  • Usiuze nguvu zako juu ya dhambi.
  • Lakini furahia urithi na haki zako kama watoto wa Mungu. Ishi kama mwana wa mfalme na ahadi zake.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *