Swahili Service

UTAVUNA UNACHOPANDA

MFULULIZO: YAKOBO; ALIFANYA MIEREKA NA MUNGU.

SOMO: MWANZO 29:1-30; WAGALATIA 6:7-10

 

Kwa kawaida mwanadamu ni muovu, mgumu na mdanganyifu. Hii ni kwa sababu ya jinsi mwanadamu alianguka katika dhambi mle Edeni. Hivyo inamchukua Mungu na nidhamu zake kumjenga tena kwa mfano wake Mungu-Warumi 8:28-29.

Mwanadamu kwa kweli anamrudia Mungu na njia zake wakati amegonga mwamba. Mwanadamu anajifundisha mambo kwa njia ngumu tu.

Yakobo alikuwa katika safari ndefu sana kutoka Beer-Sheba mpaka Harani (1200km). Mungu alimsimamisha Yakobo mle Luzu (Betheli) alimpa ahadi zake. Kupokea ahadi za Mungu lazima kujifunza nidhamu zake.

Baada ya siku nyingi, Yakobo alifika Harani. Alipofika kwa Labani mjomba wake, Yakobo alijifunza mambo mawili.

  1. Jinsi ya kumpata mchumba.
  2. Kinacho enda “round” kinakuja “round,” tunavuna tunachopanda. Hebu tujifunze:-

JINSI YA KUMPATA MCHUMBA WA KWELI.

  • Kumpata mchumba wa ndoa ndiyo jambo la maana sana.
  • Kauli ya kwanza muhimu ni kauli ya kumpokea Kristo, ya pili muhimu ni kupata mchumba wa ndoa katika maisha.
  • Mithali 18:22, “Apataye mke apata kitu chema, naye ajipatia kibalikwa BWANA.”
  • Mwanzo 2:18, “BWANA Mungu akasema, si vema hivyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.”
  • Ni jambo la maana sana watoto wakue, wawe watu wazima, wakati ufike wa kuoa na kuolewa.
  • Lakini wengi wanauliza je, ni wakati gani mwema wa kuoa? je, nimwoe nani? Je, nitatafuta mke au mume wapi?
  • Kitu cha kwanza Yakobo aliona ni kisima kilichofunikwa kwa mawe na wachungaji na kondoo zao pembeni pembeni-Mwanzo 29:7-8.
  • Baadaye Raheli binti Labani akaja na kondoo za baba yake-Raheli alikuwa mchungaji-Mwanzo 29:9.
  • Ilikuwa ni mapenzi ya kutizama tu-Mwanzo 29:10.
  • Kutoka pale Yakobo alikaribishwa nyumbani kwa Labani kwa upendo mkuu-Mwanzo 29:11-14.
  • Baadaye Yakobo alianza kumtumikia Labani, lakini alipoulizwa juu ya malipo ya mshahara, Yakobo alisema yuko tayari kutumika miaka saba apate Raheli kama mke wake-contract ya miaka saba-Mwanzo 29:20.
  • Baada ya miaka saba, harusi, lakini badala ya kupewa Raheli alipewa Lea. Kumpata Raheli alipaswa kutumika miaka saba zaidi!!!
  • Kuna kanuni 5 za jinsi ya kumpata mpenzi anayefaa:-
  1. Ngojea wakati unaofaa kuoa au kuolewa.
  • Kwanza lazima kuwa na uhusiano mwema na Mungu wako.
  • Yakobo kwanza kabisa alikutana na Mungu mle Luzu (Betheli) alipopata ngazi ya maisha.
  • Yakobo kwanza alimpata Mungu ndani ya maisha yake. Yakobo alifanya nadhiri na Mungu kwa jinsi atakavyoishi maisha yake.
  • Mtu yuko tayari kuoa na kuolewa tu, anapokuwa na Mungu ndani ya maisha yake.

Pili, uwe na uhusiano mwema na watu.

  • Ndoa ni uhusianao na watu, (social maturity).
  • Yakobo alikuwa ameimika kiasi kufanya urafiki na kuudumisha.
  • Yakobo alikuwa mzima kiasi kuongea na wachungaji kisimani, Raheli na wengine (social skills).

Tatu, lazima uwe na kazi kwa mikono yako.

  • Fanya kazi upate kudumisha jamii.
  • Yakobo alikuwa tayari kufanya kazi miaka saba kabla ya kuoa.
  • Raheli naye alikuwa kazini ya uchungaji wa kondoo.
  • Kijana (Yakobo) alikuwa kazini, msichana (Raheli) alikuwa na kazi ya kufanya. Hivyo wote wawili walikuwa kazini (economic maturity).

Nne, tayari kufanya kazi za nyumbani.

  • Upishi, kutandika kitanda, na kazi zote za nyumbani. Wazazi ni lazima kufundisha watoto wao wa kiume na wa kike kazi zote za nyumbani kabla ya kuoa.
  1. Oa na kuolewa kwa sababu nzuri.

Sababu zifuatazo ni mbaya kwa kuoa:

Kuasi (rebellion)-ndugu yake Yakobo-Esau alioa wake zake wawili kwa sababu ya uasi.

    • Binti za Hethi walikuwa wapagani!!

Kukimbia (escapism)

    • Watu wengi wanaoa kwa sababu ya kukimbia hali mbaya nyumbani. Uhusiano mbaya, shida za nyumbani.
    • Yakobo alikimbia nyumbani lakini alingoja miaka saba kutulia.
    • Wengine wanaoa kwa sababu wazazi wao Wazee wanahitaji mfanya kazi.

Kusurutishwa na watu (social pressure).

  • Usioe kwa sababu ya watu na pressure yao.
  • Ukisema, “nilazima nioe au niolewe kwa sababu kila mtu anaoa na kuolewa.

Urembo-(physical attraction).

  • Yakobo alivutiwa na urembo wa Raheli-Mwanzo 29:17.
  • Raheli alikuwa mrembo (sana)!! Urembo si sababu ya kuoa mtu. Urembo wa nje si wa kudumu.
  • Wanao oa kwa sababu ya urembo wanapata mshtuko wa moyo (fatal attraction).

Mahari (dowry)-usiolewe ili jamii yako wapate pesa na mali.

  • Sababu nzuri za kuoa na kuolewa ni kutimiza mapenzi ya Mungu.
  • Jamii-companionship.
  • Kuzaa-kizazi kinacho mpendeza Mungu (Godly heritage).
  • Kuonyesha upendo wa Kristo ulivyo (demonstrate the love of Christ to the church).

Sikiza ushauri wa watu waaminifu.

  • Katika Mwanzo 28, Yakobo alifuata ushauri wa wazazi wake-29:2.
  • Wazazi wa pande mbili walihusika kwa ndoa ya Yakobo.

Tafuta mchumba mahali panapofaa.

  • Kisimani-mahali kazi, ibada, kanisani-2 Wakorintho 6:14.

Tafuta mtu anayefaa.

KINACHO ZUNGUKA KINAKUJA KWA MZUNGUKO, (What goes around comes around).

  • Tunavuna tunacho panda- Wagalatia 6:7.
  • Yakobo alipanda udanganyifu sasa udanganyifu utamfikia yeye mwenyewe.
  • Mjombake Yakobo (Labani) ataenda kufundisha Yakobo adabu na somo la maisha.
  • Yakobo alifanya kazi miaka saba apewe Raheli baadaye amepewa Lea- Mwanzo 29:25-26. Mungu anajua jinsi ya kuwatuma watu wake Harani- mahali pa majaribu na magumu.
  • Harani yako ni mahali pa shida, kazini, uhusiano, ndoa, kukosa kazi, fedha au afya yako.

 

MWISHO

  • Kumbuka Mungu ndiye anayetutuma “Harani” kwa sababu zake.
  • Barabara ya kuingia katika nchi ya ahadi inapitia Harani.
  • Mungu aliyekuwa na Yakobo atakuwa nawe katika Harani yako.
  • Mungu aliyemfanya Yakobo kufaulu mle Harani, atakufanya kufaulu katika maisha yako.
  • Je, ujumbe huu umekupata wapi katika maisha yako?

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *