MFULULIZO: VITA VYA KIROHO
SOMO: MATHAYO 3:1-12; MARKO 16:17-18
Katika Mathayo 3:7, tunalo neno la mtu mmoja wa Mungu aliyetumia maneno yake kwa makini sana. Mtu huyu ni Yohana aliyekuja duniani kutengeneza njia ya kupitia Bwana Yesu Kristo. Mathayo 3:7- “Hata alipoona wengi miongoni mwa mafarisayo, na Masadukayo wakiujia ubatizo wake aliwaambia, enyi wazao, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayo kuja?”
Yohana aliwaita Mafarisayo na Masadukayo uzao wa nyoka (fira) (Vipers- Fira).
Katika Marko 16:17-18- “Na ishara hizi zitafuatana na hao waminio, kwa jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya, watashika nyoka, hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa, wataweka mikono yao juu ya wagonjwa nao watapata afya.”
Ishara tano katika kifungu hiki ni:-
- Watatoa pepo.
- Watasema kwa lugha mpya.
- Watashika nyoka.
- Wataweka mikono yao juu ya wagonjwa na watapata afya.
- Hata wakinywa kitu cha sumu, hakitawadhuru kabisa.
Leo tunaangazia juu ya ishara ya tatu.
- Ishara hii ya tatu haieleweki na watu wengi.
- Haimaanishi kubeba nyoka kama jinsi waganga.
- Maanake ni kwamba sisi kama watu wa Mungu tutakabidhi nyoka na roho za nyoka.
- Yesu Kristo alisema maneno haya (Marko 16:17-18) baada ya kufufuka kwa wafu. Yohana naye aliwaita watu wa kizazi chake (uzao wa nyoka), nyoka aina ya fira (viper).
- Kuna aina nyingi ya fira katika wanadamu.
- Ishara ya nne haimaanishi tujaribu kunywa sumu bali wanadamu wanapojaribu kutupea sumu, haitatudhuru kamwe.
- Katika Matendo ya Mitume 28:1-10, mtume Paulo alipata kuumwa na nyoka aina ya fira (viper).
- Mtume Paulo hakupata madhara yoyote ya ile fira.
- Shetani alipanga juu ya maisha ya mtume Paulo.
- Shetani alipanga mauti na kushindwa kwa mtume Paulo bila kufaulu.
- Shabaha ya shetani ilikuwa kumwaibisha Paulo mbele ya watu.
- Shetani alificha nyoka (fira) katika kuni alizo okota mtume Paulo.
- Hivi leo shetani yuaficha nyoka katika kuni kila siku ili kutushinda.
- Fira anaweza kuishi katika mwili, roho na nafsi ya mtu.
- Kulikuwa na fira katika roho ya Gehazi. Siku moja huyo nyoka alionekana katika maisha ya Gehazi.
- Gehazi alikuwa mtu hodari katika kazi ya Mungu chini ya nabii Elisha.
- Gehazi angeliweza kuwa nabii wa nguvu mara nne nguvu za nabii Elijah.
- Lakini roho ya nyoka ilikuwa ndani yake Gehazi. Hebu tuone:-
MAANAKE NYOKA (FIRA) KATIKA KIROHO
- Fira ni nyoka aliye na sumu mbaya zaidi katika nyoka zote.
- Kiroho, fira ni roho hatari zaidi.
- Shetani ni mfano wa nyoka, Lucifer ndiye adui wetu mkuu.
- Shetani kwa maana hana mwili, yeye anaishi katika miili ya watu, wanyama, viumbe na vitu vya kila aina.
- Nyoka ya fira inaishi na chakula chake ni nge (Scorpions).
- Nge ni kiumbe chenye sumu sana, lakini ndio chakula cha fira!! Hivyo fira anayo sumu kali zaidi ya nge.
- Fira ni pepo mkuu anayepata nguvu zake kutoka kwa pepo walio chini (lower demons).
- Fira anayo ngozi maridadi sana lakini ndani yake sumu nyingi zaidi.
- Fira ni picha ya watu wanaonekana wazuri na warembo zaidi, lakini ndani yao ni sumu na mauti.
- Fira (vipers) wanakula mama zao kupitia kwa tumbo zao, fira anakuwa mtoto hana huruma.
- Mtu anapoumwa na nyoka ya fira wa kiume, anapata mashimo mawili, fira wa kike anaacha mashimo manne.
- Shetani ameficha fira za kila aina katika njia na ngazi za watu wasiweze kufaulu.
- Fira za uasherati, tamaa mbaya, kiburi, hasira na ghadhabu, kuteta na wivu.
- Mtu anapoumwa na fira hawezi kuinuka tena.
FIRA (VIPER) KATIKA MATENDO 28:1-10
- Huyu nyoka alikuwa na shabaha ya kumwangusha mtume Paulo mbele ya watu wa Melita.
- Fira ni roho wa dharau na aibu.
- Shabaha ni Paulo akose heshima mbele ya:-
- Warumi waliokuwa katika meli kwenda Roma.
- Wafungwa kama Paulo waliokuwa pamoja nao.
- Mbele ya watu wa kisiwa cha Melita.
- Kumbuka Paulo alikuwa amewahubiri hawa Waroma na pia wafungwa (prisoners).
- Shetani anajua kuaibisha watu.
- Shetani aliaibisha Samsoni mbele ya Wafilisti.
- Shetani alimwaibisha Musa mbele ya watu wa Israeli jangwani.
- Shetani alipanga kumwaibisha mtume Paulo mele ya watu lakini Mungu alimwaibisha yule nyoka.
- Watu wa Melita walimwita mtume Paulo muuaji, lakini baadaye walimwita Paulo mtumishi wa Mungu au Mungu.
- Unapotambua kuwa kuna fira ndani yako, unaitaji kumtupa katika moto.
- Leo shetani aweze kuaibika kwa maisha yako.
- Nyoka anamaanisha mauti, upinzani, changamoto na utumwa wa shetani.
KWA NINI (FIRA) NYOKA ANAWEZA KATAA KUACHA MKONO WA MTU?
- Kukosa ukombozi au ukombozi usio kamilifu.
- Ukombozi kamili ni hatua sita (6).
- Kuzaliwa mara ya pili- kuokoka kabisa.
- Kutambua kuna shida, taabu katika maisha.
- Kung’oa ile shida, taabu katika maisha.
- Kutoa na kusafisha takataka yote ya shetani.
- Kutengeneza na kutibu majeraha yote ya shetani.
- Kufunga kila njia aliyopitia adui.
- Kutotii sauti na maagizo ya Mungu.
- Mungu anafanya kazi yake panapo utii.
- Wana wa Israeli walipokosa utii wote isipokuwa Yoshua na Kalebu, walikufa jangwani.
- Samsoni alipokosa utii aling’olewa macho yake baadaye kufa mikononi mwa adui.
- Sauli mfalme alikufa vitani.
- Eli alikufa mauti ya aibu kwa kutotii.
- Akani alikufa pamoja na jamii yake na mali yake yote kwa kutotii.
MWISHO- MAOMBI
- Ninawasamehe wote walionikosea, walioniudhi katika jina la Yesu Kristo.
- Bwana nisamehe makosa na dhambi zangu zote katika jina la Yesu Kristo.
- Ninavunja kila nguvu na agano za shetani maishani, najifungua kutoka kwa mamlaka yake katika jina la Yesu Kristo.
- Ninakemea na kuvunja kila uhusiano wangu na kila roho ya nyoka, mume na mke wa kiroho katika jina la Yesu Kristo.
- Katika jina la Yesu Kristo, ninakataa na kuvunja kila roho chafu.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025
