MATHAYO 25:1-13
Mfano wa wana wali kumi ulipeanwa na Yesu Kristo. Kristo alipenda kueleza jinsi ufalme wa mbinguni ulivyo. Mfano huu unajulikana sana duniani. Kristo alitoa mfano huu siku chache kabla ya kumaliza kazi yake hapa duniani. Kristo alipenda sana wate waweze kuelewa kwamba mlango wa neema ya Mungu unafungwa ghafla. Siku ya neema imekuwa refu miaka 2000, lakini siku ya neema inao mwisho wake. Siku ya Bwana inakuja upesi sana. Historia inasonga ukingoni, haitaendelea kuwa kawaida.
Yesu Kristo alikuwa hodari sana kwa kueleza hadithi. Kila mtu upenda sana arusi. Arusi za wayahudi na watu wa mashariki ya kati zinachukua wakati. Muda wake ulikuwa wiki mbili, hau zaidi kulingana na utajiri wa Bwana Arusi. Kristo alitumia mfano huu kuonyesha umuhimu wa kuwa tayari na kukesha kwa sababu hatujui siku wala saa ya kurudi kwa Yesu Kristo duniani.
Katika Arusi za dunia hii, kila mtu anamtazamia Bibi-Arusi. Mapambo yake, sura yake, umbo wake, kila mtu anasimamia heshima Bibi-Arusi. Lakini Arusi ya mbinguni, macho yote yanakazana kumtazama na kumgojea Bwana-Arusi.
Yesu Kristo ndiye Bwana-Arusi, kanisa lake ndio Bibi-Arusi wa Kristo.
Yesu Kristo yuarudi kumchukua bibi arusi wake, yaani, Kanisa lake (Ufunuo 19:7) kanisa lake na bibi-arusi wa Yesu ni wale tu majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima (Ufunuo 21:27). Hebu tuone jinsi mlango ulifungwa ghafla.
- KURUDI KWA YESU KRISTO NI HAKIKA (MATHAYO 25:1)
- Tumeelezwa kwamba wanawali kumi walitwaa taa zao.
- Walitoka kwenda kumlaki Bwana-Arusi
- Hawa wanawali walijua kwamba Bwana Arusi alikuwa jiani, walimgoja kwa subira nyingi sana.
- Yesu Kristo akiisha maliza kazi yake ya ukombozi wetu hapa duniani, alikufa kifo cha msalabani, akazikwa, akafufuka siku ya tatu, akapaa mbinguni.
- Yesu Kristo yuaja tena. Wanafunzi wake waliambiwa “enyi watu wa Galilaya mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni, atakuja jinsi io hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni” (Matendo 1:11)
- Kuja kwa Yesu Kristo mara ya kwanza kulikuwa ni kuanzilisha ufalme wa Mungu duniani, kuvunja nguvu za shetani na kuanza utawala wa Mungu.
- Kuja kwa Yesu Kristo mara ya pili ni kuikamilisha kazi yake na ushindi wake juu ya dhambi na uovu na kurudisha kabisa utawala wa Mungu juu duniani.
- Wakristo wa kila kizazi wamengojea kwa hamu kuja kwa Yesu Kristo mara ya pili kama jinsi mtume Paulo anatueleza katika (Warumi 8:19-21)
- Yesu Kristo ndiye Historia na siku zote za usoni.
- Ni lazima kutazama kwa hamu kurudi kwa Yesu Kristo hapa duniani.
- KURUDI KWA YESU KRISTO NI FURAHA
- Arusi zote duani ni wakati wa furaha.
- Karamu za Arusi, kula pamoja, kukutana tena jamii na marafiki ni jambo la furaha.
- Yesu Kristo alipenda Arusi. Kristo aliaza kazi yake duniani katika arusi pale Kana-Galilaya.
- Hapo Kristo alitenda muujiza wake wa kwanza alipogeuza maji yakawa divai (Yohana 2:1)
- Lakini karamu kuu zaidi itakuwa Arusi ya Mwana-Kondoo (Ufunuo 19:6-9)
- Huku tutasherekea ushindi wa Yesu Kristo juu ya dhambi na uovu wote.
- Itakuwa siku ya furaha nyingi zaidi kwetu tumpendao Kristo.
- Arusi nyingi huwa na shida mbali mbali na kuchelewa, hata hivyo Arusi hii ya Yesu Kristo inaonekana kukawia na kuchelewa?
III. KURUDI KWA YESU KRISTO NI KAMA KUKAWIA
- Sasa yapata miaka 2000 tangu Kristo kwenda mbinguni. Lakini alisema tukeshe na kuomba, hivyo akatoa mfano huu wa jinsi ufalme wa mbinguni ulivyo.
- Wakristo wengi wameingia katika mashaka mengi wanapo ngojea kurudi kwa Kristo.
- Mtume Paulo aliwaandikia waraka wakristo pale Thesalonika, kwa maana wengi wao walikataa kwenda kazi kumgojea Kristo.
- Hivyo Paulo anawaambia juu ya uzembe, ukawaambia sharti kufanya kazi na kula chakula cha kazi ya mikono yao. (II Wathesalonike 3:12-15)
- Mtume Petro alituonya juu ya waalimu wa uongo, waliofundisha kwamba Kristo amechelewa kurudi (I Petro 3:4-8)
- Yesu Kristo pia alitufundisha na kutuonya juu ya kuweka ratiba, siku ,saa na mwaka wa kurudi kwake (Mathayo 24:36)
- Yesu Kristo haja chelewa kurudi, lakini yeye yuko katika ratiba yake. Dalili zote zaonyesha Kristo amekaribia leo kuliko jana.
- KURUDI KWA YESU KRISTO KUNATENGANISHA WATU
- Kristo ametufundisha umuhimu wa kuwa tayari kila saa kwa kurudi kwake hau kutenganishwa na kifo na mauti.
- Katika dhoruba za maisha, dhiki ni nyingi lakini katika vyovyote lazima kuwa tayari kuingia milele naye ajapo.
- Basi katika mfano huu wa Yesu Kristo, kulikuwako na wanawali wa haina mbili.
- Watano wao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara.
- Hawa wanawali ni picha ya kanisa la Kristo duniani.
- Katika huu wakati wa kungoja wanawali wote kumi walionekana sawa.
- Leo hii ni vigumu sana kujua ni nani mkristo wa kweli na yule feki.
- Lakini kelele za kuja kwake Kristo zitakapo sikika ndio tutaona utofauti.
- Leo tunaanza kusikia kelele za Bwana Arusi akija. Tunaendela kuona utofauti.
- Saa hii ya korona, kanisa limefungwa hapa Kenya.serikali inasema tufungue kanisa kwa maana ibada ni haki ya binadamu. Wakuu wengine wa kanisa na dini wanaenda kwa serikali kusema “Hapana, msifungue, hata mkifungua sisi hatutafungua ile yetu” Hebu tuwaone hawa wanawali tena;
- Wanawali wapumbavu
- Wanawali wote kumi walijua kwamba Bwana Arusi yuaja.
- Wapumbavu walikuwa na taa zao, lakini hawakujaza mafuta taa zao.
- Katika Biblia, mafuta ni ishara ya Roho Mtakatifu.
- Upako wa Roho mtakatifu dio nguvu za mkristo (Waebrania 1:9, I Yohana 2:20,27)
- Walikuwa na mafuta kidogo, kumaanisha kuna uwezekano kuoja kipawa cha Roho mtakatifu mbila kukaa kamilifu katika upako wa Roho mtakatifu.
- Hawa wapumbavu walikuwa na jina na tabia ya wanawali.
- Hawa wapumbavu walikuwa na taa zao za wanawali wa kweli.
- Hawa wapumbavu walikuwa marafiki na wenye busara.
- Hawa wapumbavu walikuwa na tabia , sura na uniform kama wenye busara.
- Hawa wapumbavu walikuwa waombaji sana “Tupeni mafuta yenu kidogo maana taa zetu zinazimika.
- Hawa wapumbavu hawakuwa tayari kuingia na mfalme.
- Hawa wapumbavu hawakuwa na Imani timilifu ya kuwa tayari kusubiri.
- Hawa wapumbavu walichezea Arusi ya Mwana wa Mfalme.
- Hawa wapumbavu waligojea kufanya usiku yale wangalifanya mchana.
- Hawa wapumbavu walikataliwa wote “Mlango ulifungwa “wale wako dani walifungiwa ndani, wale walikuwa inje walifungiwa inje.
- Huu mlango ulipofungwa haukufunguliwa tena.
- Watu wengi wanasema “Mungu akifunga mlango moja atafungua mwingine”
- Ndio akifunga moja atafungua mwingine wa kuingia jehanamu na ziwa la moto.
- Lazima tuwe tayari kabla ya mlango kufungwa.
- Mlango wa neema hufungwa haraka sana.
- Leo wewe huko na fursa ya kuokoka, kuoshwa dhambi, kifo kinakuja. Huenda mbao za geneza yako ziko tayari store, hau geneza yako iko tayari.
- Usikawie kuokoka leo, akwitapo Mwokozi.
- Wanawali wenye Busara.
- Hawa ni wale wameokoka na kujazwa Roho matakatifu.
- Kwa neema ya Bwana wanamwishia Yesu Kristo siku kwa siku, saa kwa saa, wanao hakika wamekwisha okoka.
- Hawa wenye Busara wamepatanishwa na Mungu kwa kifo cha Yesu Kristo msalabani.
- Hawa wenye busara wanakaa katika hali ya kujazwa, wako na njaa ya kweli na utakatifu.
- Hawa wenye busara wanaishi katika utakatifu na ushirika mkuu na Mungu wao.
- Hawa wenye busara wako tayari kumwishia Kristo, wako tayari kufa, wako tayari kwa yoyote yale, wanajua chochote chaweza kutokea.
- Bwana-Arusi alipokuja waliingia mara moja na yeye.
- Mlango ulifungwa mara moja walipoingia.
- Mlango wa milele unafungwa mara moja.
- “Yeye anafunga na hakuna afunguaye” (Ufunuo 3:7)
- Wote watano waliingia kibinafsi, hakuna mtu anaweza kuingia kwa niaba yako. Kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe.
- Wokovu wa wazazi wako, ndungu, watoto, dada zako hauwezi kukuhesabia.
- Yesu Kristo anatenganisha, watu wa ndani wanafungiwa ndani, na inje wanafungiwa inje.
- Wapumbavu kwa kweli walinunua mafuta wakarudi kukuta mlango umefungwa.
- Walipo omba sana kufunguliwa, Bwana-Ariusi alisema “Amini nawaambia, siwajui ninyi”
MWISHO
- Je wewe uko tayari Bwana Arusi anapotokea.
- Je uhusiano wako na Yesu Kristo ukoje?
- Je, Imani yako ni ya kweli, umeokoka kwa kweli?
- Je, umejazwa Roho Mtakatifu? Leo jazwa kwa Imani. Uwe na hakika umeokoka, tubu kila dhambi zako zote, omba kwa Imani kujazwa.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DAMU YA UTAKASO. - October 26, 2025
- KEY TO DIVINE SPEED. - October 26, 2025
- LEVELS OF THE ANOINTING. - October 22, 2025

Nimefurahia sana fundisho hili kuu katika maisha yangu je naweza patq nakala zingine za mafundisho yako?