Swahili Service

YESU NI NANI?

MFULULIZO: SAFIRI NA YOHANA

SOMO: YOHANA 1:1-36

 

Yesu Kristo ni Mungu, muumba, uzima, nuru na kondoo wa Mungu.

Yohana Mbatizaji alitokea dunia kama jinsi umeme kwa nchi ya Israeli.

Huyu Yohana Mbatizaji alikuwa akihubiri katika nyika ya Yordani na watu wa tabaka zote, wakuu kwa wadogo walienda nyikani kumwona na kusikia aliyosema Yohana Mbatizaji.

Wengine walisadiki neno na ujumbe wake hivyo walibatizwa na Yohana, huku walitubu dhambi zao.

Yohana Mbatizaji alikuwa mtu wa kutisha sana, hakuwa mtu wa kawaida.

Kwanza Yohana Mbatizaji alikuwa Mnazarene, hivyo nywele yake ilikuwa refu zaidi, nguo zake zilikuwa kutoka kwa singa za ngamia. Yohana pia hakula chakula cha kawaida, lakini asali na nzige, sauti yake ilikuwa kali sana. Ujumbe wake Yohana ulikuwa ni TUBU DHAMBI.

Mafarisayo na waandishi na pia mazadukayo wote walienda nyikani kumsikia Yohana Mbatizaji. Wakuu wao walitumana na swali, “Je, wewe ni nani?”- Yohana 1:19-20.

Yohana hakusitasita kujibu swali lao. Aliwaambia, “mimi siye Kristo”, lakini “mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani inyoosheni njia ya Bwana” kama alivyosema nabii Isaya- Yohana 1:23.

Walipomuuliza Yohana, “wewe ni nani” Yohana naye aliwaeleza “Yesu ni nani”. Haya maswali mawili ni ya maana sana katika maisha yako.

“Wewe ni nani?” na “Yesu ni nani?”

Hebu tujaribu kuyajibu haya maswali mawili hivi leo kutoka kwa Biblia:-

YESU KRISTO NI MWENYEZI MUNGU

  • Je, Yesu ni nani? Yesu ni Mungu.
  • Yohana 1:1- Hapo mwanzo, Mwanzo 1:1.
  • “Neno” ni Mungu, Yesu Kristo- Yohana 1:34.
  • Yohana Mbatizaji alikuwa akimtambulisha Yesu Kristo kwa watu- Yohana 1:15. Yesu Kristo ndiye Mungu wa milele.
  • Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu isipokuwa Yesu Kristo- Yohana 1:18.
  • Yesu Kristo ndio Ufunuo wa Mungu.

YESU KRISTO NI MUUMBA- Yohana 1:3

  • Hata ingawa Yesu Kristo ndiye muumba wa yote, ulimwengu haukumtambua- Yohana 1:10.
  • Yesu Kristo ni muumba wa yote isipokuwa dhambi.

YESU KRISTO NDIYE UZIMA

  • Uzima ni mtu- Yohana 1:4, 14:6.
  • Mungu alipoumba mwanadamu, alimpulizia uzima wake Mungu, mwanadamu akawa na nafsi- Mwanzo 1:26-27.
  • Yesu Kristo alimpa mwanadamu uzima- Yohana 10:10.
  • Hivyo Yesu Kristo ni Mungu, ni muumba na ni uzima.

YESU KRISTO NI NURU- Yohana 1:4-5

  • Yesu Kristo ndiye nuru na ule uzima ni nuru ya watu.
  • Nuru yake inang’aa ulimwenguni wote, ulimwengu unakaa katika giza.
  • Giza hii ni giza ya dhambi lakini giza hii haiwezi kushinda ile NURU.
  • Giza haitambui ile nuru.
  • Yesu Kristo alikuja kuwa nuru ya mwanadamu, Yesu Kristo ndiye habari njema.
  • Yesu Kristo anamtia nuru kila mtu ajaye duniani- Yohana 1:9.
  • Yesu Kristo ni NURU ya ulimwengu- Yohana 8:12.

YESU KRISTO NI KONDOO WA MUNGU- Yohana 1:29, 1:36

  • Yesu Kristo ndiye kondoo wa Pasaka.
  • Yesu Kristo ndiye dhabihu yetu.
  • Yesu Kristo alichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake.
  • Hivyo, Yesu Kristo ni Mungu, muumba uzima, nuru na kondoo wa Mungu- kuondoa dhambi zetu.
  • Pasipo na Mungu, giza inatawala.
  • Giza iliyo kuu zaidi ni giza ya kutookoka- 2 Wakorintho 4:4.
  • Jehanamu ni mahali pa giza kuu- Kutoka 10:21; Ayubu 17:13; Yohana 3:19.
  • Yesu Kristo alikuja kama nuru , lakini watu walikataa ile nuru- Yohana 1:10.
  • Ulimwengu ulimkataa Kristo na NURU aliyoleta- Matendo 4:11.
  • Wengine walimpokea Kristo, Nuru ya ulimwengu- Yohana 1:12-13.
  • Kumpokea Kristo Maanake ni:-
  1. Kutambua Yesu Kristo ni nani.
  2. Kutegemea ukamilifu wa kazi yake Yesu Kristo msalabani.
  3. Kupokea uzima wake kwa kumpa nafsi yako.
  4. Kuamua kabisa kumwishia Yesu kama Bwana na mkombozi wako.
  • Tunapompokea Yesu Kristo kama Bwana na mkombozi wa maisha yetu, tunafanyika kuwa wana- Waefeso 2:19; Wagalatia 4:6-7; 1 Yohana 3:5; Wagalatia 4:4; 1 Yohana 5:4-5.

MWISHO

  • YESU KRISTO ni Mungu, muumba wetu, uzima wa milele, nuru na kondoo wa Mungu.
  • Je, umepokea uwezo wa kuwa mwana wa Mungu?
  • Yesu Kristo ni neema na utukufu wa Mungu- Yohana 1:14-18.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *