MFULULIZO: YUSUFU
SOMO: MWANZO 38:1-30.
Ikiwa unapenda kuwa kiongozi wa watu na kuwa na usemi juu ya watu, basi kuwa mtu wa msimamo, usiwe kama dunia. Chukua jukumu juu ya jamii yako, anagalia sana maisha na tabia yako na zaidi ya yote tazamia neema ya Mungu.
Katika Mwanzo 38, tunaona ni kwa nini Mungu hakumchagua Yuda na Reuben kuwa kiongozi juu ya nyumba ya Israeli. Yuda alikosa nguvu za kuongoza. Katika sura hii ya 38 tunaona kwa nini Mungu alimchagua Yusufu kuongoza Israeli, hata ingawa Yusufu alikuwa mzaliwa wa mwisho katika Mwanzo 38:1.
- “Wakati ule, Yuda akashuka kutoka kwa ndugu zake, akamfikia mtu mwadulami jina lake Hira.”
- Yuda alikuwa mtu wa kushuka chini kiroho.
- Yuda alikuwa mtu wa kwenda zake katika bonde la maovu.
- Yuda hakupenda njia za Mungu, ndipo anatafuta mke kutoka Kanaani watu wasio mcha Mungu.
- Yuda hakupenda kutembea katika njia za haki-Kutoka 23:2; Waamuzi 9:3; 1 Samweli 8:3; Ayubu 31:7.
- Yuda alikataa njia ya haki, akachagua njia ya ulimwengu.
- Mwanzo 38:2, “Yuda akaona huko Binti wa mtu Makanaani jina lake Shua, akamtwaa, akaingia kwake.”
- Maana ya Shua ni utajiri au mwenye kupenda anasa na maisha ya raha, (affluence).
- Shua naye akamzaa Eri na Onani na Shela.
- Mwanzo 38:3-4 maana ya jina Eri-“kujifurahisha nafsi,” maana ya Onani ni “nguvu za kiume” (manly vigor).
- Maana yake Shela ni ‘kuburudika” au kustawi maana ya mji wa Kezibu ni udanganyifu.
- Yuda alikuwa amevutwa na anasa za ulimwengu kiasi alitoka njia za Mungu na kufuata ulimwengu huu.
- Maisha ya Yuda ilijaa kutafuta fedha, mali na anasa ya uasherati.
- Yuda hangeweza kuongoza ndugu zake katika njia za haki, alikuwa mbali zaidi na Mungu wa Israeli na njia za Mungu.
- Leo hii maisha kama ya Yuda inatufanya mtu asiweze kuwa kiongozi wa nyumba yake na watu.
- Unapochukuliwa na tabia hii ya Yuda hauna nguvu za kuwaeleza watu wokovu, wacha kuwaongoza.
- Wana wanne wa Yakobo walio wa kwanza walikuwa waasi. Reuben na Yuda walikuwa washerati wasio na mipaka, Simioni na Lawi walikuwa wenye hasira, ghadhabu na mauaji.
- Wote wanne walikuwa hawawezi kuwasaidia ndugu zao na maisha yao.
- Ikiwa unataka sana kuwasaidia watu na maisha yao basi:-
USIFUATE ANASA ZA DUNIA HUU.
- Usipotee katika kufuata vitu vya dunia kama mali, fedha na tamaa-badala yake mtafute Mungu.
- Wacha shabaha ya maisha yako iwe Mungu-Mathayo 6:33.
- Usiende na kushuka chini na kuenda kando kama jinsi Yuda.
- Lakini panda juu katika nguvu za Roho Mtakatifu.
- Ikiwa kwa kweli utapenda kuwa na mamlaka na usemi juu ya watu usipende ulimwengu na tamaa zake.
JALI SANA MAMBO YA JAMII YAKO.
- Kwanza uwe kiongozi kwa nyumba na jamii yako kabla hujajaribu kuongoza watu wengine.
- Ongoza kwanza watoto wako kabla hujakuwa kiongozi juu ya watoto wa wengine.
- Yuda hakuwaongoza watoto wake vyema, hivyo hangeweza kuwaongoza ndugu zake Israeli.
- Kwa kufuata anasa na mali na furaha ya ulimwengu Yuda alipoteza watoto wake-Mwanzo 38:6-8.
- Jukumu za ndugu katika siku za Agano la Kale ilikuwa ni kumzalia ndugu marehemu watoto watakao itanishwa kwa jina la ndugu marehemu (Hii inaitwa Levirate marriage” “Levir” Maanake ni ndugu ya mume” “husband’s brother.”
- Hii ilikuwa ni jukumu mtu anachukua kwa kujitoa kwa manufaa ya ndugu marehemu.
- Utamaduni huu baadaye uliingia katika sheria na amri za Musa-Kumbukumbu 25:5-6 miaka 500 baadae.
- Onani alijua jukumu hizi juu ya mke wa nduguye Eri.
- Mwanzo 38:9-10 lakini Onani alijua kwamba watoto watakao zaliwa hawatakuwa wake, bali wa nduguye marehemu Eri.
- Mungu alimuua Onani si kwa sababu ya kumwaga mbegu chini (withdrawal method of family planning) lakini ni kwa sababu ya ubinafsi wake na uchoyo wake kutojali nyumba na jamii ya nduguye Eri.
- Onani hakupenda ndugu yake Eri aweze kuwa na jamii na jina duniani Mungu hakupendezwa. Yuda naye alifikiria shida ni Tamari, pengine alifikiri Tamari ni laana kwa jamii yake, mchawi au black widow.
- Lakini shida haikuwa wanawe-hawakumpendeza Mungu.
- Wanawe Yuda walizidi kumwasi Mungu, hivyo Yuda hakuitimu kuwa kiongozi juu ya Israeli-1 Timotheo 3:4-5.
- Ikiwa Ukristo wako haufanyi kazi nyumbani kwako, basi usidhubutu kuusambaza.
- Watoto wanaiga wazazi wao, Yuda alitafuta anasa, mali, fedha na ulimwengu, wanawe pia walifuata baba yao.
UWE KIELELEZO CHEMA KWA JINSI UNAVYOISHI MAISHA YAKO.
- Ishi maisha yako kwa uadilifu na ukweli.
- Mwenendo wako uende sambamba na maneno ya kinywa chako.
- Yuda aliishi maisha ya unafiki-Mwanzo 38:12.
- Katika mila za Kanaani msimu wa kukata kondoo manyoya ulienda pamoja na sherehe za uasherati mwingi sana, uzinzi na nguvu za uzazi zilifanya kuwa na Malaya wa hekalu (temple prostitutes).
- Yuda alikuwa amepoteza mke wake, Binti Shua. Yuda na marafiki zake walikuwa washerati-Mwanzo 38:13-14.
- Yuda anamkashifu Tamari kwa tabia zake, tabia alizokuwa nazo Yuda-Mwanzo 38:15-24.
- Yuda ni picha ya watu wanaodhulumu wenzao kwa dhambi wanaozifanya wenyewe-Mwanzo 38:25-26.
- Ikiwa unapenda kuwa kiongozi mwema, usiifuate dunia hii, tumikia jamii yako kwa uaminifu, uwe kielelezo chema.
- Lakini ikiwa tayari umekwisha anguka, kumbuka kunao tumaini katika Mungu wa mbinguni-Mwanzo 38:27-30.
- Neema ya Mungu ni yakushangaza-Mathayo 1:3.
- Miaka 2,000 baadae, uzao wa Yuda ulibarikiwa kiasi Mwokozi Yesu Kristo akazaliwa katika nyumba ya Yuda.
- Mungu anaweza kukutumia, Mungu anaweza kunitumia kwa neema yake.
- Neema ya Mungu inatosha kwa kila anayenyenyekea, mbele zake Mungu.
MWISHO
- Leo mtumaini Mungu kwa maisha yako.
- Wacha Mungu akufanye kiongozi ampendaye.
- Omba sana Mungu akaokoe jamii yako.
- Nyenyekea mbele zake Mwokozi wako!!
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO. - September 21, 2025
- GOD GUIDES OUR DESTINIES. - September 21, 2025
- GOD OF THE BREAKTHROUGHS - September 10, 2025