MWENYE HAKI ATAISHI KWA IMANI Swahili Service

JINSI YA KUMALIZA VYEMA

WAEBRANIA 12:12-17

UTANGULIZI

Mwandishi wa waebrania anataka tuweze kufahamu kwamba safari ya Imani ni ngumu na ni vyema kuelewa na binu za kumaliza vyema. Mtume Paulo alijua kwamba mtu anaweza kuanza vyema lakini mwisho wake kutupwa inje. Hivyo katika Waebrania 12, mtume ametueleza kwa maisha dani ya Kristo ni kama jinsi mbio za masaba marefu yaani Marathoni. Ni lazima kuweka uzito na dhambi mbali nasi, huku tukimtizama Yesu Kristo na kustahimili mpaka mwisho. (I Wakorintho 9:27)

Hebu tujifunze:-

 

I.  KWANZA, INYOSHENI MIKONO ILIYOLEGEA NA MAGOTI YALIYOPOOZA (V.12)

  • Kuna wakristo wengi wenye ugonjwa wa mikono na miguu.
  • Mikono yao imelegea kufanya kazi ya Bwana.
  • Magoti yao imepooza kutembea na Kristo.
  • Musa alilegea mikono yake hivyo (Kutoka 17:10-12)
  • Kazi ya Bwana inahitaji kila mmoja wetu. (Waebrania 3:13)
  • Mtume Paulo mwenye alikata tamaa (II Wakorintho 7:6-7)

 

 

 

II.  PILI, MKAIFANYIE MIGUU YENU NJIA YA KUNYOKA (v.13)

  • Kaa mahali pako katika hizi mbio.
  • Fanya bidi usiwe kikwazo kwa wakimbiaji wezako.
  • “Kitu kilichokiwete” ni watu wale bado kuokoka , wasipotoshwe– bali wapate kuokoka.

 

III. TATU, TAFUTENI SANA KWA BIDII KUWA NA AMANI NA UTAKATIFU (v.14)

  • Amani ni njia mbili– hivyo Amani haitengemei wewe pekee (Warumi 12:18)
  • Katika dunia hii tunahitaji kujua vita vitakuwa bila wewe kupenda.

 

IV. NNE, USIPUNGUKIWE NA NEEMA YA MUNGU (v.15)

  • Kila mtu, angalia sana usipungukiwe neema.
  • Usikatae msamaha wa Mungu, hau usikatae kuwasamehe wengine.

 

V.  TANO, SHINA LA UCHUNGU LISIJE LIKACHIPUKA NA KUWASUMBUA WATU WENGI.

  • Uchungu ni sumu ya kujiua wenyewe.
  • Uchungu kila mara utawafikia watu wale wengine kama jamii, watoto wako, marafiki, washirika.
  • Uchungu huleta udanganyifu, masengenyo, mashitaki, watu wanaposhiriki sumu ya uchungu, basi.

 

 

VI.  SITA, USIDHIHAKI MAMBO NA NENO LA MUNGU (v.16-17)

  • Esau alidharau neon la Mungu, alicheza na urithi wake. Alipenda kuwida, chakula na wanawake.
  • Esau alikuwa mtu asiye na Mungu (bebelos) “godless”
  • Esau aliishi maisha ya anasa, kujipendeza mwenyewe (Hedonism)
  • Esau aliishi maisha ya machozi, hakuweza kuyabandilisha yaliyopita na ya kale.
  • Esau alidhihaki Mungu, Mungu hadhihakiwi, (Wagalatia 6:7)
  • Usidhihaki mambo ya Mungu kamwe.

 

 

MWISHO

¨ Hata wewe na mimi tunaweza kumaliza vyema.

¨ Hakikisha umeokoka na unapita katika njia iliyonyoka.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *